Serikali yetu na majumba ya kifahari!

Kumbe wote hata sita ni mafisadi??? Nani kasalia jamani kuugua ugonjwa huo wa ufisadi usiotibika nchini?
 
Nashangaa!!!kwa hiyo tutakuwa tunajenga nyumba mpya kila tutakapopata spika mpya?
Yeah, bado kuna mawaziri hawana nyumba kwa sababu serikali ya Mkapa iliamua kubinafsisha nyumba za serikali.
 
Labda nidurufu ile kauli ya mwanajf mmoja hivi karibuni aliposema:

Tulieni mnyolewe vizuri..
 
''Íf you want to live straight life in africa, you die a poor man''
 
Halafu baada ya uspika wake kuisha anauziwa moja kwa moja at a discounted price?!
 
Msekwa na Sitta walikuwa wanaishi wapi?


...si waliuziwa nyumba wajameni....labda tuweke sheria na huyu anne asijiuzie......sinayeye anayo nyumba nyingine aliyonunuaga kwenye utumishi wa umma..?

sioni ubaya kuwa na official residents kwa ajili ya spika,jaji mkuu.,wakuu wa idara nyeti.,meya wa jiji etc..lakini wazuiwe wasijiuzie..please....

angalieni spika sitta ameondoka hadi na ofisi ya kifahari ya hadhi ya uspika urambo..tena iliyofunguliwa na Rais...
 


Kwa kulinganisha umuhimu wa hizo picha za nyumba hapo juu, Je yule Prof. wa Marekani aliyesema sisi Waafrica akili yetu huenda ina mushkeli alikosea?
 
Bongo sasa hivi ulimbukeni wa kuweka swimming pool umeingia kwa kasi sana, hao wanaowekewa usikute kuogelea mzozo.
 
NGESEWA WANAVIMBIWA HALAFU WANAKWENDA TAPIKIA MIGUUNI MWA WAZUNGU,Kazi ya MKWERE ni kututukanisha kwa wazungu kuwa Watanzania ni maskini wakti huu umaskini wanautengeneza wao na mabasha wao
 
NGESEWA WANAVIMBIWA HALAFU WANAKWENDA TAPIKIA MIGUUNI MWA WAZUNGU,Kazi ya MKWERE ni kututukanisha kwa wazungu kuwa Watanzania ni maskini wakti huu umaskini wanautengeneza wao na mabasha wao
Du!
Polepole ndugu
Umeambiwa utulie unyolewe vizuri!:frusty::frusty::frusty:
 

Hii ni nyumba ya Gavana wa benki kuu kati ya nyumba mbili zilizo gharimu bilioni 5.7,ilizuwa manunguniko mengi kutoka kwa wananchi kutoka na gharama kubwa kupita kiasi.

Aisee!!!! Nina uhakika huyu bwana watoto wake wote wako US/Europe. Sasa atakuwa anaishi na nani humo? Kwli kama wewe ni mzalendo halisi huwezi kubali jengewa nyumba ya 6 Billion ukijua fika temeke hospital, mwananyamala etc wato wanakufa kwa kukosa dawa za shs 2000. Sawa bwana waendelee kutumbua tu.
 
Wakati wananchi wa jiji la Dar es salaam wanapoteza masaa 6 kwenye foleni barabarani kila siku, serikali imeshawanunulia ma wasiri magari ya harama, wanawajengea wengine mahekalu? Ni kweli hawa mawaziri hawana uwezo wa kununua hata magari yao wakaenda nayo kazini? Hivi huyu anayejengewa nyumba alikuwa anaishi kwenye mitaro? Kwa nini wasianze kujenga hizo barabara za juu walizoahidi ili kupunguza msururu wa magari na kuokoa muda unaopotea? Jamani humu jamvini hakuna vibaraka wao wawapelekee haya malalamiko yetu!
Kweli serikali yetu inajali watu wachache!
 

na usikute nyumba anayodaiwa kupangishiwa ilikua yake.so akawa anatafuna kodi za raia huku amekaa kwenye nyumba yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…