Lole Gwakisa
JF-Expert Member
- Nov 5, 2008
- 4,735
- 2,265
Mara nyingi kama si zote, wana react kwa matukio, na wako nyuma ya ku pre empt matukio.
Agenda ya maendeleo kazi yake ni kuboresha maisha kwa kuyafikiria matukio yanayoweza kutokea baadaye.
Mto Msimbazi ni moja ya matatizo ambayo miaka nenda rudi, mafuriko yake hayajaweza kupatiwa ufumbuzi.
Miaka 40 iliyopita mto Msimbazi ulifurika mara moja kila miaka mitano.
Leo hata mvua ndogo mto huu unafurika kiasi cha barabara kubwa inayokatiza ,Morogoro rd, kutopitika.
Miaka yote hii, outlet ya mto ni daraja la Selander, daraja ambalo ni takriban mita 40 hivi.
Yale maji yooote ya msimbazi yanapitia hapo, upenyo wa mita 40.
Kwa wale watakao nielewa kihandisi, kwa nini kwa hali hii kusiwepo na back up ya maji pale maji ya mto yakiwa mengi?
Sasa hivi tumeambiwa kingo za daraja la Selander zimeanza kuliwa na mto.
Kuna siku itatokea maji ya mto yatakuwa mengi hadi kupita juu ya sehemu dhaifu ya daraja la Selander!
Hapo hadi Rais, Makamu wa Rais,Waziri Mkuu, na mawaziri wote watahamia Selander "kujionea " mafuriko!
Natoa tahadhari tu.