Serikali Yawatelekeza Wanafunzi Nchini Ujerumani

JeanPrierre

Member
Feb 4, 2012
91
30
Wanafunzi wa Tanzania wanaosoma Master na PhD nchini Ujerumani kwa ufadhili wa Wizara ya Elimu (MoEVT) Tanzania na Exchange Program (DAAD) ya Ujerumani mpaka sasa hawajatumiwa hela ya kujikimu ya kila mwezi kutoka MoEVT ambayo walitakiwa kuipata kabla ya tar 1 December.
Inasemekana wengi wao mpaka sasa wameshatakiwa kuondoka kwenye nyumba wanazoishi kutokana na kutolipa kodi ya nyumba na wengi kutishiwa kuchukuliwa hatua za kisheria zaidi.

Pamoja na wanafunzi hao kwa wingi wao kuandika email kwenda kwa mtu anayeshughulikia masuala yao na kumcopy mtu anayeshughulia masuala yao kwa upande wa ujerumani, lakini mpaka sasa hajawajibu kueleza chanzo cha kuchelewa kwa allowance zao.

Chakushangaza, alipotafutwa kwa njia ya simu na mtu kutoka DAAD(Exchange Program), alisema kuwa hakuwa ofisini kama wiki moja kwahiyo alikuwa hajui kama wanafunzi hao hawajatumia allowance zao.

My take: hapo ndo tumefikia, ofisi za Serikali kugeuzwa za watu binafsi
 
We unaongelea posho kuchelewa kwa siku tatu loh! mi namjua mtu aliyecheleweshewa kwa miaka mpaka akafia hukohuko ulaya, piga evening class hapahapa bongo huku ukiendelea kuchanga ada kwenye biashara ya vitumbua, huko mtoni ni kwenda kuteseka mwishowe utaishia kusukumwa no kusukuma maviTU.
 
Kweli nyerere ali2lea vibaya sisi watanzania,yani mtu yuko masters nd phd bado nae analia njaa kama mtoto wa undergraduate!
 
Back
Top Bottom