comrade igwe
JF-Expert Member
- Jan 12, 2015
- 7,295
- 3,945
Serikali imewaonya kuwachukulia hatua kali waajiri wote nchini wenye tabia ya kuchelewesha au kutowasilisha michango ya watumishi wao kwenye mifuko ya Hifadhi za jamii nchini, kauli hiyo imetolewa na Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan jijini Mwanza Mh Makamo wa Rais ametoa onyo hilo wakati wa kuongea na wastaafu watarajiwa, mifuko ya jamii na baadhi ya waajiri amesema kumekua na usumbufu mkubwa sana wanaopata wastaafu wakiwa wanafuatilia mafao yao katika baadhi ya mifuko ya Hifadhi jamii na wamekua wakiambiwa baadhi ya michango yao haikuwasilishwa na waajiri waokwenye mifuko hiyo hivyo amezionya taasisi za serikali, taasisi nyingine, mashirika ya umma, wakala wa serikali na waajiri wote wawe waangalifu kwani ikibainika uzembe huo hatua kali zitachukuliwa dhidi yao