Serikali yawaahidi neema watumishi

Serikali yawaahidi neema watumishi

Watumishi tutangulize Uzalendo kwanza mi mshahara ninaolipwa nikiongezewa utakua mkubwa sanaa wakati kuna watanzania wanaishi katika mazingira magumu
Mkuu watumishi wamejikaza mno, hakuna cha uzalendo. Wengine wanagawana posho na mishahara minono, halafu watumishi wanaendelea kusota, inatosha.
 
Watumishi tutangulize Uzalendo kwanza mi mshahara ninaolipwa nikiongezewa utakua mkubwa sanaa wakati kuna watanzania wanaishi katika mazingira magumu
Sasa shida ni ya watumishi ama serikali unayoipigia debe bila kutumia akili.

Tuipende nchi yetu.
 
Leadership is a body which you cannot carry everybody along.....
punguza chuki utaishia kupata stress na magonjwa ya moyo
jioni njema
Nilimchukia zaidi alipokuwa hai! Kwa sasa chuki zangu ndiyo zinaelekea kaburini bila shaka. So don't worry.

Na kwako pia jioni njema.
 
Watumishi tutangulize Uzalendo kwanza mi mshahara ninaolipwa nikiongezewa utakua mkubwa sanaa wakati kuna watanzania wanaishi katika mazingira magumu
Acha kujishaua basi. Hao Watanzania wanao ishi katika mazingira magumu, ndugu zao wanao wasaidia kika siku/mwezi, siyo hao watumishi wa umma?

Au huwa unawasidia wewe?
 
Who cheated you?? Evil monsters like your man will still come back to haunt innocent people in the name of a ghost or ancestor!!!! Dictators never rest. God always punish them by turning their sad dead selves into ghost
 
Kikubwa watumishi wana subilia kwa hamu kubwa Mei Day 2021 ,ili wasikie Kauli ya Mheshimiwa Rais then kusubilia utekelezaji wa maelekezo yake.
 

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Mohamed Mchengerwa, amesema atazingatia maslahi ya watumishi wa umma ikiwamo nyongeza ya mishahara, malipo ya wastaafu na kupandiswa kwa madaraja kwa mujibu wa sheria.

Mchengerwa alisema hayo juzi jijini hapa alipokuwa akizungumza na watumishi wa wizara hiyo katika kikao kazi pamoja na kujitambulisha rasmi.

Alisema akiwa katika nafasi hiyo, moja ya vipaumbele vyake itakuwa kuhakikisha maslahi ya watumishi wa umma yanazingatiwa ili kuongoza ufanisi na kuleta tija katika maeneo mbalimbali.

Masuala kama nyongeza ya mishara, kupandishwa kwa madaraja ya watumishi, malipo ya wastafu, alsiema ni mambo ambayo yapo kwa mujibu wa sheria hivyo utekelezaji wake ni wa lazima na si hiari.

“Mtumishi kuongezwa mshahara, kupandishwa madara au kupandishwa vyeo haya yapo kwa mujibu wa sheria na si ombi wala huruma ya mwajiri wake, hivyo tutahakikisha tunatekeleza kwa mujibu wa sheria inavyoelekeza,” alisema Mchengerwa.

Pia alsiema alisema pamekuwapo na malalamiko ya watumishi wa umma juu ya kupandishwa madaraja kazini na wengi wao kukaimu nafasi kwa muda mrefu.

“Sheria inatutaka kupadisha madaraja mtumishi kwa muda fulani lakini wengi bado hawajapatiwa haki yao, hivyo tutahakikisha tunafanya kwa kuzingatia sheria,” alisema.

Waziri pia alipiga marufuku watumishi kukaimishwa nafasi moja kwa zaidi ya miezi sita kama ambavyo imekuwa mazoea katika utumishi wa umma katika maeneo mbalimbali.

“Sheria inakataza mtumishi kukaimishwa katika nafasi kwa miezi sita lakini leo hii kuna maeneo wako watu wamekaimu kwa zaidi ya miaka sita, hivyo kuanzia leo (juzi) ni marufuku mtu kukaimu zaidi ya miezi sita” alisisitiza Mchengerwa.

Pia alisema moja ya maeneo ambayo watayafanyia kazi pia ni pamoja na malalamiko ya malipo ya wastaafu kucheleweshwa na kuwapa wakati mgumu kumudu maisha yao na familia zao.

Alisema watumishi wengi ambao wamemaliza muda wao wa kulitumikia taifa na kustaafu kwa mujibu wa sheria, bado wamekuwa wakikumbana na kero ya kucheleweshewa malipo kinyume cha sheria.

“Haki hizi kwa mtumishi aliyefanya kazi kwa kuzingatia kanuni na maadili ya utumishi wa umma ni jambo la lazima na si la kuomba, hivyo ni lazima azipate kama sheria inavyoelekeza” alisema Mchengerwa.

Kadhalika alisema kuwa katika uongozi wake atahakikisha stahiki zote za mtumishi zinapatiknaa kwa wakati ili kuongeza morali kwa kujituma katika maeneo yao.

Vilevile, aliwataka wakuu wa wilaya wa mikoa ambao wamekuwa na tibia ya kutumia mamlaka yao vibaya kwa kuwaweka ndani watumishi, kuacha mara moja na kutumia busara.

“Serikali inazingatia sheria na utawala bora. Niwaombe viongozi wenzangu kutumia busara pale inapobidi kwani kumekuwapo na viongozi ambao wanafanya mambo ambayo yanakiuka hata katiba ya nchi. Viongozi wote wanatakiwa kufanya mambo kwa kuzingatia kanuni na sheria,” alisema Mchengerwa.

Mama ana nia njema Sana ila baadhi ya genge la mwenda zake majizi ndo yanataka kumuangusha, ila yatashindwa KWA jina la Tanzania na Mungu alie hai
 
Back
Top Bottom