Serikali yaunda Tume kuchunguza Ufisadi Tanesco | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yaunda Tume kuchunguza Ufisadi Tanesco

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BelindaJacob, Jul 29, 2009.

 1. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #1
  Jul 29, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 476
  Trophy Points: 180
  Na Kizitto Noya, Dodoma

  SIKU moja baada ya Mbunge wa Sumve (CCM), Richard Ndassa kuibua ufisadi wa Sh1.4 bilioni ndani ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), serikali imeunda tume kuchunguza tuhuma hizo.

  Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja aliliambia gazeti hili jana kuwa tuhuma hizo ni nzito na hawezi kuacha zikapita bila kuzifanyia kazi.

  "Mimi ndiyo kwanza nilizisikia bungeni na kimsingi nilipigwa butwaa, lakini sasa nimeanza kulishughulikia suala hilo kwa kuunda kamati ya uchunguzi," alisema Ngeleja na kuongeza;

  "Ninaamini kazi kubwa, lakini haitakuwa nzito sana kwani mheshimiwa mbunge ametusaidia kwa kutaja namba za nyumba zinazohusika".

  Ngeleja ambaye hakutaja idadi ya wajumbe wanaounda kamati hiyo wala muda watakaotumia kukamilisha kazi hiyo, alisema anaamini uchunguzi huo hautachukua muda mrefu.

  Alisema kwa kuwa suala hilo limeibuliwa bungeni, ataweka matokeo ya uchunguzi huo hadharani ili wananchi wajue ukweli wake.

  "Of Course (kwa ujumla) tuhuma hizo ni nzito, lakini siwezi kusema lolote zaidi ya kueleza kuwa ninazifanyia uchunguzi. Kazi imeanza leo (jana) na kwa sababu suala hilo limeibuliwa bungeni, tukimaliza kazi tutaijulisha jamii," alisema Ngeleja.

  Juzi jioni wakati akihitimisha mjadala wa wizara yake ya Nishati na Madini, Waziri Ngeleja aliliambia Bunge kuwa tuhuma hizo ni changamoto kwake na kwamba anajipanga kuishughulikia mara moja.

  Aliliambia Bunge kuwa anathamini mchango wa mbunge huyo na kwamba isingekuwa rahisi kwake kufahamu jambo hilo kwa kuwa kinachoiunganisha wizara yake na Tanesco ni Bodi ya Wakurugenzi wa shirika hilo.

  Juzi mbunge wa Sumve Richard Ndassa aliibua ufisadi katika Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na kulieleza Bunge kuwa shirika hilo liko katika harakati ya kuiuza kwa Sh60 milioni nyumba namba 13 iliyoko Oysterbay jijini Dar es Salaam, mtaa wa Toure/Chaza line baada ya kuikarabati kwa Sh 600 milioni.

  Sambamba na ufisadi huo, pia Shirika hilo linatuhumiwa kutumia Sh1.4 bilioni kukarabati nyumba sita za wakurugenzi kinyume na taratibu.

  Ndasa alitoa tuhuma hizo alipokuwa akichangia bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini iliyowasilishwa Jumamosi iliyopita na waziri wake William Ngeleja.

  More : www.mwananchi.co.tz

  BJ: Tume, Tume, Tume kila mara bila matokeo ya hizo tume!.Inakera
   
 2. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #2
  Jul 29, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Hivi wenzetu huko majuu wanafanyaje maanake hapa ni tume mtindo moja na inaboa kweli kweli. Kila serikali ikibanwa tume huundwa na mara nyingi hizi tume huishia kutafuna mamilioni ya shilingi na ripoti yake kufungiwa makabatini.

  Pamoja na hayo naamini tume nyingi zimeundwa kihila na wafanyacho si kuchunguza bali kuwasafisha watuhumiwa - hivyo hujikita zaidi katika kufukia badala ya kufukua ushahidi. Haya tumeshuhudia yakifanyika, kwa mfano, kwenye tume za EPA na Richmond.

  Ni serikali ya kipuuzi na isiyo makini inayobakia kuchapa usingizi huku hujuma zinafanyika halafu kama mlevi vile na bila mpangilio hukimbilia kuunda tume inapogutushwa - ni aibu !!
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Jul 29, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,921
  Likes Received: 83,432
  Trophy Points: 280
  Kwanini huyu fisadi Idrissa Rashid ambaye ameshathibitishwa kwamba ni fisadi asifukuzwe kazi? Ni kwanini anaogopwa hivi? :confused:

  Kuna ushahidi wa kuhusika na ufisadi wa Rada ambaye naye alikatiwa vijisenti na Mzee wa Vijisenti na pia alionyesha jinsi alivyokuwa fisadi na mtetezi wa fisadi alipowatishia Watanzania kwamba kama mtambo wa Richmond usiponunuliwa basi TANESCO isilaumiwe nchi itakapoingia kizani.

  Sasa ameibuka na ufisadi mwingine wa kuikarabati nyumba yake kwa shilingi milioni 600 ili ainunue kwa 10% tu ya gharama hizo.

  Halafu Kikwete na Pinda wanapita huku na kule huku wakijipiga vifua kwamba wanapambana na ufisadi uliokithiri nchini wakati hata recommendations za tume zilizoundwa kuchunguza ufisadi mwingine hadi hii leo haujatekelezwa!!! Hii serikali ni aibu tupu halafu wanataka Kikwete agombee tena 2010 na hali kuna ushahidi wa kutisha kwamba kazi imemshinda!!!

  Mungu inusuru nchi yetu!
   
 4. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #4
  Jul 29, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Mkaguzi Mkuu alisema, TANESCO kuna uozo na uharamia katika mahesabu, Wizara na Serikali kuu kimya kama vile ni viziwi. Sasa Ngeleja anadai eti ndio kwanza kasikia habari za hujuma mpya Bungeni. Who keeps tabs on these companies and their books?

  Kwa nini wasi Micromanage haya makampuni na kutaka mahesabu kila mwezi kama si kila wiki kwa miezi 6 mfululizo?
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Jul 29, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,921
  Likes Received: 83,432
  Trophy Points: 280
  Rev, Ngeleja, Management yote ya ya juu ya TANESCO na Bodi ya Wakurugenzi wote hawa wanastahili kufukuzwa kazi mara moja kutokana na uozo uliojaa pale TANESCO, lakini tuna Rais ambaye ni muoga anaogopa kufanya maamuzi mazito ambayo yataungwa mkono na Watanzania walio wengi.

  Halafu mwenyewe haoni kama kazi imemshinda ili akae pembeni katika kinyang'anyiro cha 2010 na wako wasioitakia mema nchi yetu wameshaanza kumpigia debe pamoja na kuwa kuna ushahidi wa kutosha unaoonyesha jamaa kazi imemshinda kabisa.
   
 6. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #6
  Jul 29, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  Yaani huko Tanesco kuna uozo kweli kweli wa ufisadi, naomba tu hiyo tume iundwe ili angalau ufisadi upungue. Japo hautaisha 100%.
   
 7. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #7
  Jul 29, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Back to square one. Tume juu tume, zidi ya tume, kuichunguza tume iliyoundwa kuichunguza tume ya tume. Hii ndiyo Tanzania.

  Ama kweli bongo tambarareeee
   
 8. M

  Mong'oo Member

  #8
  Jul 29, 2009
  Joined: Oct 13, 2008
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tume ni muhimu sana kwa upande wa kurekebisha mfumo wa utendaji. Haya mambo hutokea mara nyingi kwa sababu ya 'Bad system'. Inawezekana hizi hela hazikupitishwa na board au hata Mkurugenzi Mkuu hakushishirki kiundani. Naomba tuangalie mfumo mzima wa utendaji. Inawezekana CEO wa pale akawa na nguvu kuliko hata board.

  Nachotaka kusema ni tuachie tume ifanye kazi ya kuangalia mfumo uliotumika mpaka ikafikia hapo.

  Watu walio kwenye sehemu ya mfumo mbovu huwezi kuwabana, ndiyo maana ripoti nyingi zinaishia hewani.

  Kwanza turekebishe mfumo wa utendaji na uwajibikaji uwe nzuri halafu watu walio kwenye huo mfumo nzuri wakikosea wawajibishwe.

  Ukiwa na mfumo mbovu bwana hata uweke watu wazuri kama nini hamna deliverables..
   
 9. k

  kaka2002 Member

  #9
  Jul 29, 2009
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 30
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 15
  Mimi nadhani mtu wa kulaumiwa katika mambo yote haya ni mkuu wa kaya. Kama angekuwa na nia ya kupambana na ufisadi, angeweza kuwawajibisha wateule wake badala ya kuwatetea kama ilivyo sasa.
   
 10. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #10
  Jul 29, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Mi napingana na hizi tume kila kukicha tume zinaundwa alafu report inatoka hakuna kinacho fanyika wanajaza kwenye masanduku mareport kwanini wasifukuze hawa jamaa wakae pembeni kisha uchunguzi ufanyike.
   
 11. M

  Mong'oo Member

  #11
  Jul 29, 2009
  Joined: Oct 13, 2008
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni nashauri tume ziendelee ili kurekebisha pale utaratibu uliyowekwa kama una makosa basi ubadilishwe halafu ndiyo lifuatie la kushughulikia watu waliokiuka huo utaratibu nzuri uliowekwa.

  Tume kazi yake sio kushauri kuchukuliwa(kushauri tu. Kuhusu hatua ni jeshi la polisi maana kama kutenda haki lazima waliohusika uwape nafasi ya kujitetea) hatua watu fulani tu bali kushauri wapi mfumo wa utendaji na uwajibikaji umekosewa.
   
 12. C

  Chief JF-Expert Member

  #12
  Jul 29, 2009
  Joined: Jun 5, 2006
  Messages: 1,490
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Acha kichekesho. Yaani nyumba unayoishi mwenyewe inafanyiwa ukarabati mkubwa eti hukushirikiswa kiundani. Huulizi?
   
 13. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #13
  Jul 29, 2009
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kwa mtindo huu, hata ikihisiwa nyumba ndogo ya mkulu imetoa mimba tume itaundwa!!!!!!!! Hivi Ngeleja anashindwa nini kuwapigia wajumbe wa bodi na huyo Idris japo kupata clues of the story??????????
   
 14. L

  Lione Senior Member

  #14
  Jul 29, 2009
  Joined: Dec 1, 2007
  Messages: 115
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  hivi jamani,kuna ulazima gani wa kuunda tume hapo?idrisa si yupo?kwanini wasimuite tu na kumuwajibisha after the natural justce?mbona simple tu!
   
 15. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #15
  Jul 29, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Hizi tume zimekuwa too much huko Tanzania
   
 16. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #16
  Jul 29, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Mkuu Barubaru, hako ni ka mchezo fulani ka kuwazuga mabwege. Kila kitu Tz kinafanyika ili kusogeza muda mbele. Na kwa kuwa watanzania wana vichwa vya kuku, basi watasahau na hilo suala linakuwa limezikwa bila sanda!! Huku kwetu uraiani, mtuhumiwa wa wizi anakimbizwa mzobe mzobe kwenda kwa afande huku kapigwa Tanganyika jeki. Lakini serikalini mtuhumiwa anapewa nyongeza ya mshahara kwa kuundiwa timu (tume) ya washikaji kuja kumpa kampani; wakati huo wakikomba uchache zaidi. Labda kama hujui, kila kikao cha wakubwa hata kama ni cha nusu saa kinaanzia 40,000/- hadi 80,000/- (sitting allowance). Wakikaa siku 10 tu, mtu anakomba mshahara wa mwezi, akiongeza na pesa ya soda na vocha ataandika ripoti gani kama siyo kuzuga tu? Bongo bwana, wajinga ndio waliwao!!:confused:
   
 17. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #17
  Jul 29, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,921
  Likes Received: 83,432
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  The TANESCO mansion that got a 600m/- facelift: A one-storey residential building located at plot number 13 along Toure-Chaza Roads in Oysterbay, Dar es Salaam, belonging to the state-run Tanzania Electric Supply Company (TANESCO), is pictured yesterday in its current state after reportedly undergoing major renovation work worth a staggering 600m/-, courtesy of public funds. According to Sumve MP Richard Ndassa, the house is now in the process of being `quietly` sold to none other than the incumbent TANESCO Managing Director, Dr Idris Rashidi (INSET), for a mere 60m/-. Picture from THIS DAY​
   
 18. SILENT WHISPER

  SILENT WHISPER JF-Expert Member

  #18
  Jul 29, 2009
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 2,231
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  tume itatumia bil 2 kuchunguza bil 1.4 , ulaji juu ya ulaji.
   
 19. K

  KIMBOYA VUMILIA Member

  #19
  Jul 29, 2009
  Joined: Apr 24, 2009
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ikumbukwe huyu Boss wa Tanesco kuna wakati aliomba kuachia ngazi lakini JK akamwomba asifanye hivyo ... hivi yeye ni nani kiasi anaogopwa?..anasiri gani moyoni mwake?..hakuna shaka hili ndilo linampa kiburi ya kufanya analotaka!
   
 20. m

  montero New Member

  #20
  Jul 29, 2009
  Joined: Apr 2, 2009
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa nchi kama Tanzania ambapo kuna kuogopana sana linapokuja suala la wahalifu kuwajibishwa hasa wahalifu hao wanapokuwa ni vigogo, tume zitaendelea kuwa kiini macho kwa walalahoi. Huwa nasikitika sana ninapoona aina hii ya usanii tunaofanyiwa kila siku kama watu tusio na uwezo wa kuchanganua mambo na kujua lipi ni kweli na lipi ni uongo, na nasikitika zaidi kwa sababu sioni ni kwa jinsi gani hali hii itaisha kwani watu hao hao wanatuongoza kwa mazingaombwe, wanawaandaa watoto wao kwa nguvu ya pesa hizo wanazochoteana serikalini na kuanza kuwaridhisha madaraka ili mara watakapoondoka madarakani watoto wao waendeleze pale walipoishia!

  Kinachofanywa na serikali yetu iliyokithiri katika kukumbatia ufisadi ni kuwa mara inapobainika kwa jamii kuwa kuna mchezo mchafu wa ufujaji wa pesa za umma umefanywa na wakubwa basi, hukimbilia kuunda tume kwa ajili ya kuwafanya watu waamini kuwa suala hilo litashughulikiwa na hatua stahiki kuchukuliwa lakini in actual fact, ni kwamba tume zinaundwa ili ku-buy time ili watu wasahau ili baadae serikali itakapokuja na majibu ya 'hovyo hovyo' kuhusiana na ripoti ya tume hizo, suala lenyewe liwe limeishapungua makali au hata limeishajitokeza jingine ambalo limehamisha mawazo ya wananchi.

  Twende mbele turudi ni nyuma tume ngapi zimeundwa nchi hii na zikatoa ripoti ambayo serikali ili-act upon accordingly, siku zote kama wajumbe wa tume watakuwa na ujasiri wa kutofanya kazi ya kuwasafisha watuhumiwa, basi ripoti yao kama haitatupwa kapuni bila kufanyiwa kazi kama ripoti ya tume ya Jaji Rugakingila, basi matokeo yake yatapindishwa na kufanya wajumbe wa tume waonekane wamefanya kazi kwa kuwaonea na kuwasingizia watuhumiwa kama tume ya akina Mwakyembe!

  Oooh, Tanzania nchi yangu! Ni lini tutapata Ukombozi wa Kweli ili wananchi tutambua uzuri wa kuwa huru, mbona hata nchi ambazo zipo kwenye machafuko miaka nenda miaka rudi zimepiga hatua sana kimaendeleo na kutuacha mbali huku zikiwa hazina rasilimali kama tulizonazo sisi. Au ndio tuamini kwamba TUMELOGWA, na aliyetuloga AMEKUFA!
   
Loading...