boaz mwalwayo
JF-Expert Member
- Jan 27, 2015
- 5,793
- 4,214
Kama kawaida serikali ya media nunueni kwanza dawa alafu ndo mmje kwenye media
Nyumbu ni nyumbuZilongwa mbali zitendwa mbali
Sasa kama hela ya dawa imepelekwa leo vipi wagonjwa wa juzi je walipaswa kuvumilia ugonjwa hadi hii leo ambapo serikali itanunua hizo dawa au zilitakiwa zipewe kipaumbele kwa kununuliwa kabla hata ya vitu vingine?
Tatizo lako unaongea kwa kukurupuka. Utakua una matatizo kichwani. Be careful! Utakuja toa bomu la mwaka ambalo litakupeleka lupango very soonTatizo ni kuongea bila kutenda....
Hivi mngenunua dawa kimya kimya watu wakazikuta hospital si wangekuja hapa kuwasifia wenyewe bila kujitangaza.......
Masikini majaliwa naye kaambukizwa kuongea sana bila kutenda......
Sasa yale madeni yao pale MSD wamelipa ? Kumbuka hiyo ni hela imetolewa , sasa ukiambiwa 85% imelipa deni usirushe ngumi .Najua kuna kikundi fulani kitakuja na kukejeli hatua hii. Mungu ibariki serikali hii ya awamu ya tano kwani ni wewe ee Mwenyezi ulie iweka madalakani kama njia za kuikomboa Tanzania.
Labda na za Kagera zimeunganishwa humo!Serikali hii kwa uongo. Hivi wana ccm mnaijua trillion??
Mmejiuliza bajet ilikua sh ngap ya wizara ya afya? Nakataa mpaka nakufa hakuna uwezekano wa serikali hii kutoa trillion moja tena kwa wakati mmoja kununulia dawa ni uongo!! Subirin mtajua haya!!
Safi sana Mh. waziri mkuu...pigeni kazi hatimaye wenye maneno watakosa cha kuongea watakapo ongea vyote vikaisha
AHADI ya serikali ya kuanza kusambaza dawa katika hospitali zote nchini kutokana na madai ya kuwepo kwa uhaba wa dawa za aina mbalimbali, imeanza kutekelezwa.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa ziarani mkoani Arusha amesema Serikali imetoa Sh trilioni moja kwa ajili ya ununuzi wa dawa na kuhakikisha pia madaktari 8,000 wanasambazwa kwenye hospitali mbalimbali za mikoa na wilaya ili kutatua changamoto za afya na utoaji wa huduma bora kwa wananchi.
Katika hatua nyingine, Majaliwa amewataka watendaji wa Idara ya Uhamiaji kufanya misako kwenye nyumba za wageni na kudhibiti wageni wanaoingia kwenye mipaka mbalimbali nchini kutokana na kushamiri kwa wahamiaji haramu.
Aliyasema hayo jana wakati alipokuwa akizungumza na watumishi wa idara na taasisi mbalimbali za serikali ikiwemo watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha na Wilaya ya Arusha.
Ukosefu wa dawa.
Akizungumzia upatikanaji wa dawa, Majaliwa alisema serikali imetoa Sh trilioni moja kwa ajili ya ununuzi wa dawa za aina mbalimbali ili kuondoa upungufu wa dawa kwenye hospitali nchini.
Akieleza namna serikali ilivyo na nia ya dhati ya kumaliza tatizo la dawa nchini, Majaliwa alisema; “Awali tulitoa Sh bilioni 40 kwa ajili ya dawa na sasa tumeongeza fedha hadi kufikia shilingi trilioni moja.
“Tunataka kero ya upungufu wa dawa hospitalini iishe. Naagiza kila hospitali kuhakikisha inakuwa na dirisha la huduma za bure kwa wazee pamoja na duka la dawa,” alisema.
Chanzo: ITV
Hivi kulalamika siku hizi imekuwa sifa?Zilongwa mbali zitendwa mbali
Sasa kama hela ya dawa imepelekwa leo vipi wagonjwa wa juzi je walipaswa kuvumilia ugonjwa hadi hii leo ambapo serikali itanunua hizo dawa au zilitakiwa zipewe kipaumbele kwa kununuliwa kabla hata ya vitu vingine?
Bajeti Wizara ya Afya 2016/17 ni kizungumkuti
Bajet ya afya ni billion 800 , msiwe wenda wazimu. Mnataka kuniambia serikali safari hii imevuka lengo??
Tunadanganywa wadanganyika kwa mara nyingine tena
Kwa hiyo kwa hatua hii siri-kali imekiri kwamba ulikuwepo uhaba wa dawa?Najua kuna kikundi fulani kitakuja na kukejeli hatua hii. Mungu ibariki serikali hii ya awamu ya tano kwani ni wewe ee Mwenyezi ulie iweka madalakani kama njia za kuikomboa Tanzania.
Dawa ni consumables, siyo fixed assets!!Hii serikali inaongoza kwa uongo. Walikataa kuwa kuna uhaba wa madawa,leo wamekubali na kutenga hela.