Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 2,437
- 5,235
Mkoa wa Tabora umeanzisha oparesheni maalamu ya kukabiliana na ugonjwa wa mlipuko wa mpox kwa kuandaa vituo tengefu kwenye Hospitali za Wilaya zote za mkoa huo pamoja na vituo vya afya ili kuwahudumia kwa kina wagonjwa wa mlipuko huo endapo watabainika, huku wataalamu wa afya ngazi ya mkoa wakiendelea kutoa elimu kwa jamii na kufanya uchunguzi wa kubaini kama kuna mgonjwa yeyote mkoani hapo ili wachukue hatua stahiki.
Soma Pia: Wizara ya Afya yathibitisha uwepo wa wagonjwa wawili wa Mpox nchini
Katika hatua nyengine japo hakuna kisa chochote cha ugonjwa huo kwa Mkoa wa Tabora lakini Katibu Tawala wa Mkoa wa huo Daktari John Mboya amesema Serikali haitamvumilia mtu yeyote wakiwemo Mganga wa kienyeji atakayebainika kushiriki kumficha Mgonjwa wa Mpox kwa sababu za Imani za Kiahirikina