Serikali yatoa Bei mpya elekezi ya sukari, yafikia 2,200 kutoka 1,800

mwembemdogo

JF-Expert Member
Feb 28, 2016
2,282
1,252
Nimeshtushwa Na tamko la Waziri Mkuu Bw.Majaliwa Juu ya bei ya sukari.Wakati akitangaza kusambazwa Kwa tani 20,000 za sukari na kutangazwa kuuzwa Kwa Tsh.2,200/= Kwa kilo 1 badala ya bei ya Tsh.1 800/= bei ambayo ilitangazwa Kwa bwembwe Na kushangiliwa Na wananchi.

Najiuliza inakuwaje Serikali inashindwa kuwasaidia wananchi wake kuipata huduma ya sukari kwa unafuu?
 
Inatakiwa serikali iombe radhi! Magamba yanayoshangilia kila kitu sasa yataelewa! Hapo kima cha chini walishangilia sana sasa namba itasomeka! Tusipobadili fikra zetu Magamba yatatawala milele!
 
saiv wanawaomba wafanyabiashara tena sio amri,pm alisema ktk mfungo sukari haitakuwa shida,saiv ndg zetu waislamu wanaendelea kuumia
 
Bei elekezi ya kwanza: 1,800/-
Bei elekezi ya pili: 2,2000/-
Hali halisi kitaa: 3,0000/-

Sehemu zenye uhitaji zaidi: 3,000/-+

Tamko la waziri:"Nitahakikisha sukari haiadimiki kipindi cha mfungo wa ramadhani"

Hali halisi: Wiki ya nne sasa mtaani haipatikani"
Sarakasi time
 
Sio 2200 juzi Majaliwa kasema "wakuu wa mikoa simamieni sukari isiuzwe zaidi ya 2300" hapo ndo unabaki kushangaa kabla ya katazo la kutoagiza sukari njee tulikuwa tunapata hata kwa 1700 bila shida sasa bei juu na shida kuipata ndo maana nasema serekali ipo kwa ajili ya kuwapa shida wananchi na si kuwasaidia
 
Hivi serikali imerejea tena kufanya biashara?

Inawezekanaje iendelee kupanga bei ya bidhaa wakati walisharuhusu soko huria?

Wao wanajua principle kuu ya free market ni demand and supply

Sasa kama atatokea mfanyibiashara ambaye atauza sukari aghali wakati imejaa bwelele mitaani, automatically atakuwa ameamua kufilisika, kwa kuwa hiyo sukari itamdodea kwenye magodown yake.
 
Hivi hii sukari iliyoagizwa Na serikali Nani anaisambaza Na anafanya biashara ya kuiuza maana atuoni ofisi za wilaya au kata au kijiji zikifanya biashara ya sukari zaidi ya wafanyabiashara wale wale na je serikali si haifanyi biashara kwa hiyo wanagawa bure au
 
CCM nchi imewashinda hii ila hawataki kukubali. Kama miezi kadhaa kabla ya wao kuleta matamko ambayo hayana maslahi na nchi yetu ndio hatma yake tumefika huku.
Mimi kama mtanzania sijaona faida yoyote kwa mbwbwe na matamko yao.
 
Busara ni kutopanga bei elekezi tena, maana sidhani kama kuna mtu atawalazimisha kutaja bei elekezi kwa sababu ni elekezi ambayo haijawahi kufanya kazi
 
Wakati ule wimbo wanaimba "mtaisoma number" mlizani ni wakenya ndyo wataisoma number?
 
Hivi serikali imerejea tena kufanya biashara?

Inawezekanaje iendelee kupanga bei ya bidhaa wakati walisharuhusu soko huria?

Wao wanajua principle kuu ya free market ni demand and supply

Sasa kama atatokea mfanyibiashara ambaye atauza sukari aghali wakati imejaa bwelele mitaani, automatically atakuwa ameamua kufilisika, kwa kuwa hiyo sukari itamdodea kwenye magodown yake.
Nia yao ilikuwa njema ya kuvisaidia viwanda vya ndani,ila strategy waliyoitumia haikuwa sahh
 
Nimeshtushwa Na tamko la Waziri Mkuu Bw.Majaliwa Juu ya being ya sukari.Wakati akitangaza kusambazwa Kwa tank 20,000 za sukari Na kutangazwa kuuzwa Kwa Tsh.2,200/= Kwa kilo 1 badala ya bei ya Tsh.1 800/= bei ambayo ilitangazwa Kwa bwembwe Na kushangiliwa Na wananchi.Najiuliza inakuwaje Serikali inashindwa kuwasaidia wananchi wake kuipata Huduma ya sukari Kwa unafuu?
Hapa tungeomba uwazi utumike katika kuitangaza hiyo bei ya Tshs. 2,200. Isije ikawa wajanja wachache wametumia huu mwanya wa uhaba wa sukari kujinufaisha. Hebu tujiulize sheria na taratibu za manunuzi ya umma zilifuatwa? Ni kampuni gani ilipewa hiyo tenda ya kununua sukari? Je walinunua sukari kwa bei gani?
 
Mara ya Kwanza 1800/= Tena 2,300/= Halafu 2,200 Sasa sijui ni nini maana mitaani tunanunua 3000 au 3500
 
Back
Top Bottom