Serikali yatikiswa

Serikali yatikiswa

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,769
Reaction score
288,283
Serikali yatikiswa
• Muungano wa wapinzani watisha vigogo

na Waandishi wetu
Tanzania Daima

MTIKISIKO mkubwa umeikumba serikali huku Rais Jakaya Kikwete akibanwa pande zote kutokana na mvutano mkubwa unaodaiwa kuibuka baina ya mawaziri na viongozi waandamizi wa CCM.
Habari za kuaminika kutoka ndani ya serikali na Chama Cha Mapinduzi, zimebainisha kuwapo kwa kutoelewana na kusukumiana lawama miongoni mwa watendaji wa serikali, kuhusu kile kilichoitwa ‘kusalitiwa' kwa makubaliano yaliyofikiwa juu ya msimamo wa chama hicho, kuhusiana na suala zima la mabadiliko ya Katiba.

Katika msuguano huo, baadhi ya vigogo ndani ya CCM wamekaririwa wakisukuma lawama kwa Mwenyekiti wao, Rais Kikwete kwa kukubali haraka kusikiliza hoja za wapinzani huku akijua kuwa walifikia uamuzi wa pamoja kama chama na kukubali kupeleka muswada huo bungeni unaotokana na maoni ya wanachama.

Mmoja wa vigogo hao alikaririwa akisema Jumamosi ya wiki iliyopita kuwa hakutegemea kama Rais Kikwete angekiuka makubaliano hayo, kwa sababu yamewapa ‘kichwa' viongozi wa vyama vya upinzani.
"Tumejimaliza wenyewe bila sababu. Hakukuwa na haja ya kurejea mazungumzo na hawa watu (wapinzani) kwa sababu, kila kitu kilitendeka kisheria na wao ndio waliosusia mjadala.

"Tunawakatisha tamaa wanachama wetu, na hawataweza kutuelewa wala kutupokea tena tutakapowaendea na jambo jingine, kwa sababu tunaamua hivi na kutenda vile," alikaririwa akizungumza mmoja wa viongozi wa chama hicho katika mazungumzo yasiyo rasmi yaliyowakutanisha viongozi watano waandamizi katika moja ya hoteli za kitalii jijini Dar es Salaam.

Mbali na msuguano huo, baadhi ya watendaji wa serikali kwa upande wao wamesigana vikali, wengine wakiwasukumia lawama wenzao wanaodaiwa kutoa matamshi kuhusiana na madai ya wapinzani ya kutaka kuwepo meza ya mazungumzo.
Mawaziri, Stephen Wassira na Mathias Chikawe, walikaririwa hivi karibuni wakisema kuwa hakuna nafasi kwa Rais Kikwete kukutana na wapinzani katika jambo lililopitishwa kisheria na Bunge.
Wassira kwa upande wake alikwenda mbali zaidi na kutoa kauli ya kejeli kwamba, rais hana muda wa kukutana na wapinzani waliokuwa na hamu ya kwenda kunywa juisi Ikulu.

Mmoja wa mawaziri anayedaiwa kuchukizwa na kauli za watendaji wenzake, inadaiwa amekuwa akihaha kuwashawishi wenzake kumshauri Rais Kikwete awatimue ama awaombe mawaziri Wassira na Chikawe wajiuzulu ili kulinda heshima yao, ya serikali na chama kutokana na kauli zao.
Hata hivyo, kuna habari kuwa baadhi ya vigogo wa CCM wameanza kuingiwa hofu baada ya kuwapo taarifa za mipango ya kuungana kwa wapinzani katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Hata hivyo, uchunguzi wa Tanzania Daima Jumatano umebaini kuwa hadi sasa hakujafanyika mazungumzo yenye mwelekeo wa kuungana kwa vyama hivyo katika suala la kumsimamisha mgombea mmoja wa urais ama kushirikiana na kuweka mtu mmoja katika nafasi za ubunge.

Msimamo wa wapinzani
Wakati hali ikiwa hivyo, Umoja wa Vyama vya Upinzani vya NCCR-Mageuzi, CUF na CHADEMA, umetangaza kusitisha maandamano ya kisiasa yaliyokuwa yafanyike kesho.
Kusitishwa kwa maandamano hayo kumetokana na kauli ya Rais Jakaya Kikwete kupitia vyombo mbalimbali vya habari kwamba atakutana nao kati ya Oktoba 13 au 15 ili kuzungumzia madai ya kasoro walizoziona kwenye Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2013 yaliyopitishwa bungeni hivi karibuni.

Lengo la maandamano hayo ilikuwa kumshinikiza Rais Kikwete asisaini marekebisho ya sheria hiyo iliyopitishwa na wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuwa vipengele vingi vimewekwa kwa masilahi yao badala ya taifa.

Akitoa tamko hilo kwa waandishi wa habari kwa niaba ya wenyeviti wenzake, Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lupumba, alisema umoja huo kupitia Kamati yake ya Ufundi umesitisha maandamano hayo baada ya Ikulu kutoa taarifa kwamba ipo tayari kukutana nao.
"Tumesikia kupitia vyombo vya habari ambavyo navyo vimenukuu taarifa kutoka Ikulu kwamba Rais Kikwete amepanga kukutana na viongozi wa upinzani kuanzia Oktoba 13 hadi 15 ili kujadili na kupata muafaka wa suala la Katiba kwa vipengele tunavyovipinga.

"Tunaamini kuwa taarifa hizi ni sahihi kabisa, hivyo tumeamua kusitisha maandamano yetu yaliyolenga kushinikiza nguvu ya umma kuungana nasi katika kudai mchakato wa kuipata Katiba shirikishi na kushinikiza rais kutosaini kabisa muswada huo wa Katiba kwa kuwa una upungufu," alisisitiza.

Alisema kutokana na nia aliyoionesha Rais Kikwete ya kulipatia ufumbuzi suala hilo, vyama hivyo havina budi kusitisha kwanza mchakato mzima wa maandamano na mikutano hiyo ya hadhara hadi pale mazungumzo na rais yatakapokamilika na kutoa dira ya kinachoendelea.

"Pamoja na kusitisha maandamano haya tunapendekeza huo mkutano ulioahidiwa na rais ufanyike mapema ili mchakato wa Katiba unaosuasua kwa sasa uendelee kwa ufanisi na kuwezesha kupatikana kwa Katiba iliyoandaliwa na Watanzania wote," alisema.

Alisema madai ya umoja huo ni kuwapo kwa mchakato wa Katiba shirikishi, utakaoheshimu matakwa ya Watanzania wote wa Bara na Visiwani ili kuweza kupata Katiba iliyotengenezwa na wananchi wenyewe.

Hata hivyo, pamoja na umoja huo kuyasitisha maandamano hayo, tayari Jeshi la Polisi kupitia Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alishayapiga marufuku, kwa madai kuwa yatasababisha usumbufu kwa wasafiri wengine na kupendekeza wafuasi wa vyama hivyo wakutane katika viwanja vya Jangwani bila maandamano.
 
Mkuu Azimio Jipya....wewe pamoja na kuwa umejiweka wazi hapa jamvini kwamba ni CCM siku zote naheshimu sana msimamo wako kwa kuwa huweka mbele maslahi ya nchi badala ya yale ya CCM. Hongera zako nyingi Mkuu. Kikwete machale yamemcheza kama hii katiba italeta mgogoro wa kikatiba nchini watakaolaumiwa na Watanzania wengi si akina Wassira, Chikawe au Lukuvi bali ni yeye Kikwete. Ngoja tuone kama ataamua kutoyumbishwa na wale ambao wanataka maslahi ya CCM yapewe kipaumbele kwenye hili zoezi badala ya yale ya Tanzania na Watanzania na hivyo kuhakikisha katiba mpya itayopatikana itakuwa ni ile ambayo inakubaliwa na Watanzania walio wengi.

Rais, anaagalia picha kubwa ya Tatizo na hasa kusimamia UMOJA WA TAIFA badala umoja wa chama kimoja. Rais aheshimwe kwa hilo!! Sitaki kusikia manunguniko yasiyo na msingi!!!!!!
 
Anacheza na nguvu ya umma eh!!!!!

102_6487.jpg
 
Kiukweli rais kikwete anapaswa kuwa makini sana kwa sasa,achague kati ya chama au taifa.
 
Katiba ni mali ya wananchi wote, wenye vyama na wasio na vyama,wenye dini na wasio na dini, masikini na matajiri, makabila yote,wasukuma,wanyamwezi,wachaga,wamatengo,wangoni, wanyakyusa., nk. Wa pande zote bara na visiwani, na mikoa yote. Ccm na viongozi wake wanapaswa kulijua hili vizuri, wanapaswa kufikiri zaidi ya uccm,uchadema na hata ucuf. Tanzania itaendelea kuwepo, vyama vinaweza kufa. Kikwete endelea kukomaa, taifa kwanza!
 
Tanzania Daima, mind a slanted article.

Tanzania Daima linataka kutuaminisha kuwa Rais Kikwete anashughulikia swala la mchakato wa katiba akiwa isolated from his political party na baadhi ya maofisa waandamizi serikalini. Please, give us a break.

Rais Kikwete, Serikali na chama chake wanajua vizuri wanachokifanya kama historia inavyobainisha.

Nilisema mapema ndoana ya kisiasa aliyoirusha Rais Kikwete kwenye hotuba yake ya mwisho wa mwezi wa tisa itanasa tu samaki wa kisiasa ili kuziua hoja zao kisiasa. For future reference, watch this space!.

Ni Rais huyu huyu ambaye hakutekeleza makubaliano ya awali kwa mujibu wa wale waliohudhuria vikao Ikulu tarehe 26 Novemba, 2011 ambaye kwa sasa wanasiasa wa vyama vya upinzani wanaenda tena kukaa naye kwenye meza ya maongezi.

Ni Rais huyu huyu ambaye wanasiasa wa vyama vya upinzani wanafahamu ni 'Msanii' lakini wanaenda kukaa naye kwenye meza ya maongezi kiasi kwamba hata ratiba zao za kisiasa kwa sasa zimekoma kusubiri ratiba ya kukutana na Rais ambaye ndiye political centre of gravity.

Hivi hawa viongozi wa vyama vya upinzani wanategemea nini kilichotofauti na maamuzi ambayo yamefanyika kwenye baraza la mawaziri na huku CCM wakiwa na lungu bungeni. Kama wanategemea kupata hisani, siamini kama hisani inaweza kupatikana kutoka CCM kupitia wabunge wake kwa sababu swala la katiba kwa sasa limekuwa partisan politics

Hii ndiyo akili kubwa kuongoza akili ndogo and hopefully, viongozi wa vyama vya upinzani watakuwa wamejiandaa kwenye plan B ikichukuliwa kuwa muda hauwasubiri
 
Naomba Mh Raisi akutane na wapinzani na kulimaliza hili suala. Nitafurahi zaidi kama atakutana nao kimakundi kwa maana kwamba akutane na Chadema pekee yao, CUF pekee yao na NCCR-Mageuzi pekee yao. Asikutane nao wote kwa wakati mmoja.

Mh Raisi kiukweli ana nia nzuri kabisa ya kutupatia katiba ya Tanzania na wala si ya chama.
 
huu ni muungano wa opposing parties mkuu,.akutane nao kwa pamoja awasilize
 
Ni vizuri tumeamka, lakini mpaka lini tutakuwa tunashtuka usingizini wakati mtoto tayari kashalowesha tandiko?????!!!!
 
Naomba Mh Raisi akutane na wapinzani na kulimaliza hili suala. Nitafurahi zaidi kama atakutana nao kimakundi kwa maana kwamba akutane na Chadema pekee yao, CUF pekee yao na NCCR-Mageuzi pekee yao. Asikutane nao wote kwa wakati mmoja.

Mh Raisi kiukweli ana nia nzuri kabisa ya kutupatia katiba ya Tanzania na wala si ya chama.

That is a wastage of time. Kwa nini kama kuna nia nzuri wasikutane wote kwa pamoja wakajadiliana kwa uwazi na kuelewana? Tatizo tumezoea maisha ya ujanja ujanja. Divide n rule
 
Tanzania Daima, mind a slanted article.

Tanzania Daima linataka kutuaminisha kuwa Rais Kikwete anashughulikia swala la mchakato wa katiba akiwa isolated from his political party na baadhi ya maofisa waandamizi serikalini. Please, give us a break.

Rais Kikwete, Serikali na chama chake wanajua vizuri wanachokifanya kama historia inavyobainisha.

Nilisema mapema ndoana ya kisiasa aliyoirusha Rais Kikwete kwenye hotuba yake ya mwisho wa mwezi wa tisa itanasa tu samaki wa kisiasa ili kuziua hoja zao kisiasa. For future reference, watch this space!.

Ni Rais huyu huyu ambaye hakutekeleza makubaliano ya awali kwa mujibu wa wale waliohudhuria vikao Ikulu tarehe 26 Novemba, 2011 ambaye kwa sasa wanasiasa wa vyama vya upinzani wanaenda tena kukaa naye kwenye meza ya maongezi.

Ni Rais huyu huyu ambaye wanasiasa wa vyama vya upinzani wanafahamu ni 'Msanii' lakini wanaenda kukaa naye kwenye meza ya maongezi kiasi kwamba hata ratiba zao za kisiasa kwa sasa zimekoma kusubiri ratiba ya kukutana na Rais ambaye ndiye political centre of gravity.

Hivi hawa viongozi wa vyama vya upinzani wanategemea nini kilichotofauti na maamuzi ambayo yamefanyika kwenye baraza la mawaziri na huku CCM wakiwa na lungu bungeni. Kama wanategemea kupata hisani, siamini kama hisani inaweza kupatikana kutoka CCM kupitia wabunge wake kwa sababu swala la katiba kwa sasa limekuwa partisan politics

Hii ndiyo akili kubwa kuongoza akili ndogo and hopefully, viongozi wa vyama vya upinzani watakuwa wamejiandaa kwenye plan B ikichukuliwa kuwa muda hauwasubiri

Mkuu, hii ndiyohali halisi ya mwendo wa katiba mpya kwasasa. Hata mimihuwa nashangaa watu ambao huwa wanamtenga na kumtofautisha rais na ccm halafu wanamuona kama anafanya tofauti na makubaliano ya chama chake ccm. Thubutu..........."like a daddy like a son"..........
 
[B BAK bado sana kwa upinzani kupewa nchi;
bado hamjakomaa kuweza kuongoza nchi BAK[/B]
 
Last edited by a moderator:
Maccm yataka kupola HAKI ya wananchi wengi ya kupata katiba bora
 
Maccm yataka kupola HAKI ya wananchi wengi ya kupata katiba bora

mkuu, wananchi unaowasema ni hawa machadema ambao wanatafuna fedha za ruzuku kila kukicha na kutotoa mapato na matumizi ya fedha tunazowachangisha?
 
Rais, anaagalia picha kubwa ya Tatizo na hasa kusimamia UMOJA WA TAIFA badala umoja wa chama kimoja. Rais aheshimwe kwa hilo!! Sitaki kusikia manunguniko yasiyo na msingi!!!!!!
Kumshawishi raisi kwa namna yoyote kusaini ule mswada ni sawasawa na kumshawishi kuwasha utambi wa bomu ambalo likilipuka madhara yake ni makubwa. Raisi anaona hilo ambalo baadhi ya wenzake ndani ya system hawaoni.
 
Ng'wamapalala siku zote siasa ni dynamic kwahiyo usije ukadhani kwamba hawa viongozi wa vyama vya Chadema, Cuf na Nccr hawajui usanii wa Kikwete na ccm yake. Wanaujua sana lakini na wao wanajua namna ya ku deal na msanii na aina yoyote ya usanii.

Yes walikutana nae mwaka 2011 kuzungumzia mchakato wa katiba mpya baada ya kuwepo na mkwamo na kukubaliana baadhi ya mambo ambayo kuna baadhi yalitekelezwa na kuna baadhi hayakutekelezwa. Kwakuwa ni heri nusu shari kuliko shari kamili basi kilichotekelezwa pamoja na kuwa kidogo lakini kilisaidia kulisogeza Taifa mbele japo kwa hatua chache.

Najua baadhi ya watu kama wewe mlitarajia viongozi wetu wakatae mwaliko wa kukutana raisi JK mkitarajia kwamba wangeendelea kuhamasisha maandamano lakini imekuwa kinyume chake na hapo ndipo pamewapa shida sana wahafidhina kama wewe.

Ikiwa raisi amewaomba kukutana nao hakuna hasara yoyote kumsikiliza. Akishindwa kutekeleza makubaliano basi hapo vyama vya upinzani vitaamua nini cha kufanya na wananchi watakuwa wameiona dhamira njema yao na kuuona uhuni wa ccm na usanii wa raisi JK!
 
Last edited by a moderator:
[B BAK bado sana kwa upinzani kupewa nchi;
bado hamjakomaa kuweza kuongoza nchi BAK[/B]

Kwakuwa magamba mmekomaa hadi mmeshindwa kuiongoza nchi hii basi mnadhani kila chama ni dhaifu kama mlivyo ninyi?

Anza kujiandaa kuhama nchi kwakuwa wenye nchi yao wameshatuamini na 2015 wanatukabidhi usukani wa kuiongoza magamba mtalia na kusaga meno.
 
Last edited by a moderator:
Awali na pongeza uamuzi sahihi wa viongozi wa vyama vya upinzani nchii kwa kuahirisha maandamano na mikutano yao ili kutoa nafasi ya majadiliano[meza ya duara] ili kukwamua mkwamo wa kupata katiba ya wananchi na sio ya watawala.
pia nampongeza rais wetu kwa kuona umhimu wa haraka wa kukutana na wapinzani pamoja na kwamba baadhi ya makada wenzake hawapendi.rais ametimiza kwa vitendo ushauri aliompa P.Kagame.
Nasi watz wa dini zote tuyaombee majadiliano hayo yawe na tija.
 
Tanzania Daima, mind a slanted article.

Tanzania Daima linataka kutuaminisha kuwa Rais Kikwete anashughulikia swala la mchakato wa katiba akiwa isolated from his political party na baadhi ya maofisa waandamizi serikalini. Please, give us a break.

Rais Kikwete, Serikali na chama chake wanajua vizuri wanachokifanya kama historia inavyobainisha.

Nilisema mapema ndoana ya kisiasa aliyoirusha Rais Kikwete kwenye hotuba yake ya mwisho wa mwezi wa tisa itanasa tu samaki wa kisiasa ili kuziua hoja zao kisiasa. For future reference, watch this space!.

Ni Rais huyu huyu ambaye hakutekeleza makubaliano ya awali kwa mujibu wa wale waliohudhuria vikao Ikulu tarehe 26 Novemba, 2011 ambaye kwa sasa wanasiasa wa vyama vya upinzani wanaenda tena kukaa naye kwenye meza ya maongezi.

Ni Rais huyu huyu ambaye wanasiasa wa vyama vya upinzani wanafahamu ni 'Msanii' lakini wanaenda kukaa naye kwenye meza ya maongezi kiasi kwamba hata ratiba zao za kisiasa kwa sasa zimekoma kusubiri ratiba ya kukutana na Rais ambaye ndiye political centre of gravity.

Hivi hawa viongozi wa vyama vya upinzani wanategemea nini kilichotofauti na maamuzi ambayo yamefanyika kwenye baraza la mawaziri na huku CCM wakiwa na lungu bungeni. Kama wanategemea kupata hisani, siamini kama hisani inaweza kupatikana kutoka CCM kupitia wabunge wake kwa sababu swala la katiba kwa sasa limekuwa partisan politics

Hii ndiyo akili kubwa kuongoza akili ndogo and hopefully, viongozi wa vyama vya upinzani watakuwa wamejiandaa kwenye plan B ikichukuliwa kuwa muda hauwasubiri

Mkuu mchango wako unamantinki na ni kweli rais ndiye mwenyekiti wa ccm[kitu ambacho mm nakipinga rais kuwa m/kiti wa chama fulani]pia 2011 wapinzani walienda magogoni na walikubaliana mchakato huu uende hatua kwa hatua lakini cha msingi majadiliano ndiyo silaha pekee na mhimu binadamu wanapotofautiana[kwenye majadiliano kuna kupata na kupoteza cha msingi umepata kiasi gani na umepoteza kiasi gani] hivyo wapinzani wajipange sawa sawa maana akili ndogo zinaongoza akili kubwa.
 
Back
Top Bottom