Serikali yatikiswa

Serikali yatikiswa

Serikali yatikiswa
• Muungano wa wapinzani watisha vigogo

na Waandishi wetu
Tanzania Daima


MTIKISIKO mkubwa umeikumba serikali huku Rais Jakaya Kikwete akibanwa pande zote kutokana na mvutano mkubwa unaodaiwa kuibuka baina ya mawaziri na viongozi waandamizi wa CCM.
Habari za kuaminika kutoka ndani ya serikali na Chama Cha Mapinduzi, zimebainisha kuwapo kwa kutoelewana na kusukumiana lawama miongoni mwa watendaji wa serikali, kuhusu kile kilichoitwa ‘kusalitiwa' kwa makubaliano yaliyofikiwa juu ya msimamo wa chama hicho, kuhusiana na suala zima la mabadiliko ya Katiba.

Katika msuguano huo, baadhi ya vigogo ndani ya CCM wamekaririwa wakisukuma lawama kwa Mwenyekiti wao, Rais Kikwete kwa kukubali haraka kusikiliza hoja za wapinzani huku akijua kuwa walifikia uamuzi wa pamoja kama chama na kukubali kupeleka muswada huo bungeni unaotokana na maoni ya wanachama.

Mmoja wa vigogo hao alikaririwa akisema Jumamosi ya wiki iliyopita kuwa hakutegemea kama Rais Kikwete angekiuka makubaliano hayo, kwa sababu yamewapa ‘kichwa' viongozi wa vyama vya upinzani.
"Tumejimaliza wenyewe bila sababu. Hakukuwa na haja ya kurejea mazungumzo na hawa watu (wapinzani) kwa sababu, kila kitu kilitendeka kisheria na wao ndio waliosusia mjadala.

"Tunawakatisha tamaa wanachama wetu, na hawataweza kutuelewa wala kutupokea tena tutakapowaendea na jambo jingine, kwa sababu tunaamua hivi na kutenda vile," alikaririwa akizungumza mmoja wa viongozi wa chama hicho katika mazungumzo yasiyo rasmi yaliyowakutanisha viongozi watano waandamizi katika moja ya hoteli za kitalii jijini Dar es Salaam.


Mbali na msuguano huo, baadhi ya watendaji wa serikali kwa upande wao wamesigana vikali, wengine wakiwasukumia lawama wenzao wanaodaiwa kutoa matamshi kuhusiana na madai ya wapinzani ya kutaka kuwepo meza ya mazungumzo.
Mawaziri, Stephen Wassira na Mathias Chikawe, walikaririwa hivi karibuni wakisema kuwa hakuna nafasi kwa Rais Kikwete kukutana na wapinzani katika jambo lililopitishwa kisheria na Bunge.
Wassira kwa upande wake alikwenda mbali zaidi na kutoa kauli ya kejeli kwamba, rais hana muda wa kukutana na wapinzani waliokuwa na hamu ya kwenda kunywa juisi Ikulu.

Mmoja wa mawaziri anayedaiwa kuchukizwa na kauli za watendaji wenzake, inadaiwa amekuwa akihaha kuwashawishi wenzake kumshauri Rais Kikwete awatimue ama awaombe mawaziri Wassira na Chikawe wajiuzulu ili kulinda heshima yao, ya serikali na chama kutokana na kauli zao.
Hata hivyo, kuna habari kuwa baadhi ya vigogo wa CCM wameanza kuingiwa hofu baada ya kuwapo taarifa za mipango ya kuungana kwa wapinzani katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Hata hivyo, uchunguzi wa Tanzania Daima Jumatano umebaini kuwa hadi sasa hakujafanyika mazungumzo yenye mwelekeo wa kuungana kwa vyama hivyo katika suala la kumsimamisha mgombea mmoja wa urais ama kushirikiana na kuweka mtu mmoja katika nafasi za ubunge.

Msimamo wa wapinzani
Wakati hali ikiwa hivyo, Umoja wa Vyama vya Upinzani vya NCCR-Mageuzi, CUF na CHADEMA, umetangaza kusitisha maandamano ya kisiasa yaliyokuwa yafanyike kesho.
Kusitishwa kwa maandamano hayo kumetokana na kauli ya Rais Jakaya Kikwete kupitia vyombo mbalimbali vya habari kwamba atakutana nao kati ya Oktoba 13 au 15 ili kuzungumzia madai ya kasoro walizoziona kwenye Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2013 yaliyopitishwa bungeni hivi karibuni.

Lengo la maandamano hayo ilikuwa kumshinikiza Rais Kikwete asisaini marekebisho ya sheria hiyo iliyopitishwa na wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuwa vipengele vingi vimewekwa kwa masilahi yao badala ya taifa.

Akitoa tamko hilo kwa waandishi wa habari kwa niaba ya wenyeviti wenzake, Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lupumba, alisema umoja huo kupitia Kamati yake ya Ufundi umesitisha maandamano hayo baada ya Ikulu kutoa taarifa kwamba ipo tayari kukutana nao.
"Tumesikia kupitia vyombo vya habari ambavyo navyo vimenukuu taarifa kutoka Ikulu kwamba Rais Kikwete amepanga kukutana na viongozi wa upinzani kuanzia Oktoba 13 hadi 15 ili kujadili na kupata muafaka wa suala la Katiba kwa vipengele tunavyovipinga.

"Tunaamini kuwa taarifa hizi ni sahihi kabisa, hivyo tumeamua kusitisha maandamano yetu yaliyolenga kushinikiza nguvu ya umma kuungana nasi katika kudai mchakato wa kuipata Katiba shirikishi na kushinikiza rais kutosaini kabisa muswada huo wa Katiba kwa kuwa una upungufu," alisisitiza.

Alisema kutokana na nia aliyoionesha Rais Kikwete ya kulipatia ufumbuzi suala hilo, vyama hivyo havina budi kusitisha kwanza mchakato mzima wa maandamano na mikutano hiyo ya hadhara hadi pale mazungumzo na rais yatakapokamilika na kutoa dira ya kinachoendelea.

"Pamoja na kusitisha maandamano haya tunapendekeza huo mkutano ulioahidiwa na rais ufanyike mapema ili mchakato wa Katiba unaosuasua kwa sasa uendelee kwa ufanisi na kuwezesha kupatikana kwa Katiba iliyoandaliwa na Watanzania wote," alisema.

Alisema madai ya umoja huo ni kuwapo kwa mchakato wa Katiba shirikishi, utakaoheshimu matakwa ya Watanzania wote wa Bara na Visiwani ili kuweza kupata Katiba iliyotengenezwa na wananchi wenyewe.

Hata hivyo, pamoja na umoja huo kuyasitisha maandamano hayo, tayari Jeshi la Polisi kupitia Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alishayapiga marufuku, kwa madai kuwa yatasababisha usumbufu kwa wasafiri wengine na kupendekeza wafuasi wa vyama hivyo wakutane katika viwanja vya Jangwani bila maandamano.
Nadhani hii njia aliyoitumia JK ni ya busara sana ili kuweza kuondoa sintofahamu kwani inaelekea dhahiri wasaidizi wake wana hulka ya kufanya mambo kwa papara bila kujua adhari zake. Kauli ya wasira ilinisikitisha sana ,siku zote amekuwa kiongozi asiyetumia busara na kutoitambua nafasi yake katika kulitumikia Taifa. Ngoja tusubiri tuone nini kitajiri
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mzee msolwa, makundi kwa sasa tusiyape nafasi.Kumbuka muungano wao ndiyo uliofungua njia ya majadiliano ya mezani kati yao na serikali.Acha waende kama muungano wa vyama vya upinzani na si kama chama cha upinzani ukinzani wa chama kimojakimoja ni rahisi kufutika kuliko wa muungano wa vyama vya upinzani.

Naomba Mh Raisi akutane na wapinzani na kulimaliza hili suala. Nitafurahi zaidi kama atakutana nao kimakundi kwa maana kwamba akutane na Chadema pekee yao, CUF pekee yao na NCCR-Mageuzi pekee yao. Asikutane nao wote kwa wakati mmoja.

Mh Raisi kiukweli ana nia nzuri kabisa ya kutupatia katiba ya Tanzania na wala si ya chama.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
mkuu, wananchi unaowasema ni hawa machadema ambao wanatafuna fedha za ruzuku kila kukicha na kutotoa mapato na matumizi ya fedha tunazowachangisha?

....OUT OF POINT!!. I think your brain is suffering from disease called "Wassirensis''.
The patient with this disease talks nonsense, use a lot of energy to convince people on small issues, his brain can't accept new things and believe that xmple of person with the same disease is Steven Wassira.

Pole sana, wahi hospital kabla haijawa too late!
 
Ng'wamapalala siku zote siasa ni dynamic kwahiyo usije ukadhani kwamba hawa viongozi wa vyama vya Chadema, Cuf na Nccr hawajui usanii wa Kikwete na ccm yake. Wanaujua sana lakini na wao wanajua namna ya ku deal na msanii na aina yoyote ya usanii.
Mwita Maranya , Hakuna sehemu ambayo nimesema siasa hazibadiliki. Makosa ya kisiasa yanayofanyika siyo kwa sababu siasa hazibadiliki. Moja ya makosa ya kisiasa ni pale kiongozi anaposubiri siasa zimubadilishe (out of control).

Kama waswahili wasemavyo, kutenda kosa siyo kosa bali kurudia kosa. Hiki ndicho kinachotokea kwa sasa kwa wanasiasa wa vyama vya upinzani kwenye mchakato wa katiba mpya ambapo wanasubiri Rais Kikwete na CCM yake iwabadilishe badala ya kuibadilisha.

Kwa sasa Ratiba za kisiasa zimekuwa 'pending' au go haywire kwa sababu mwenye maamuzi ni Rais Kikwete na CCM yake.
Yes walikutana nae mwaka 2011 kuzungumzia mchakato wa katiba mpya baada ya kuwepo na mkwamo na kukubaliana baadhi ya mambo ambayo kuna baadhi yalitekelezwa na kuna baadhi hayakutekelezwa. Kwakuwa ni heri nusu shari kuliko shari kamili basi kilichotekelezwa pamoja na kuwa kidogo lakini kilisaidia kulisogeza Taifa mbele japo kwa hatua chache.
Hivi unafahamu kama CCM wako na furaha sana kuhusiana na mchakato kwenda kwa kuchechemea na hasa ikichukuliwa kuwa wanapenda 'kumuongezea' Rais Kikwete muda kisheria pamoja na kwamba wanakanusha kutokana kutokukamilika katiba mpya na pia uchaguzi wa Madiwani taifa kufanyika chini ya katiba ya 1977 "inayoipa" CCM ushindi sunami.

Kuchechemea kwa mchakato kumeifanya hata CHADEMA kushindwa kutekeleza sera yake ya majimbo Zanzibar kwa sababu haifahamu matokeo ya mchakato wa katiba yatakuwaje(serikali mbili au tatu).

Wakati CHADEMA mambo yao yamesimama au yanachechemea huku wakikabiliwa na chaguzi kuu mbili 2014, huku uchaguzi mkuu wa ndani ya chama ukiwa political hot potato. CCM wao wanajiandaa na chaguzi kuu moja huku wakizidi ku-consolidate more political and economic power.

Najua baadhi ya watu kama wewe mlitarajia viongozi wetu wakatae mwaliko wa kukutana raisi JK mkitarajia kwamba wangeendelea kuhamasisha maandamano lakini imekuwa kinyume chake na hapo ndipo pamewapa shida sana wahafidhina kama wewe.

Ikiwa raisi amewaomba kukutana nao hakuna hasara yoyote kumsikiliza. Akishindwa kutekeleza makubaliano basi hapo vyama vya upinzani vitaamua nini cha kufanya na wananchi watakuwa wameiona dhamira njema yao na kuuona uhuni wa ccm na usanii wa raisi JK!
Watu kama mimi ninaangalia kwa pembeni jinsi viongozi wa vyama vya upinzani wakikosa mwerekeo na nguzo imara katika political case yao kuhusiana na mchakato wa katiba huku Rais Kikwete na CCM yake waki-dictate terms and condition na pia mwerekeo wa upatikanaji wa katiba mpya.

Ni viongozi hawa hawa walisema hawaweI tena kwenda kuonana na Rais kuhusiana na swala la katiba mpya kwa sababu ni "msanii" na katika masaa 24, walichokisema kikawa ni useless baada ya hotuba ya Rais.

Yangu macho na masikio.
 
Kiukweli rais kikwete anapaswa kuwa makini sana kwa sasa,achague kati ya chama au taifa.
s
Hapo hakuna suala la Chama au Taifa ila kilichopo hapo ni kikundi cha manyang'au wachache wanatokata kutumbukiza nchi kwenye matatizo wakijua wazi kuwa wao wana mahali pa kukimbilia. Hebu fikiri mtu anateuliwa na kupewa mkate wake wa kila siku anafika mahali anasema rais hana muda wa kukutana na wapinzani waliokuwa na hamu ya kwenda kunywa juisi Ikulu kwa maneno mengine ni kuwa milango ya Ikulu imefungwa! Huyo anayesema hivyo siyo Rais wa nchi ni mteule tu wa Rais, anajipachika madaraka makubwa hivyo ya kusema Rais hana muda! Rais hana muda! Rais hana muda wa kushughulikia jambo linalopasua nchi! Rais hana muda wa kukutana na kushughulikia kero za wananchi! Kweli aliyesema sentensi hiyo anapaswa kujiuzulu haraka kwa kujivika madaraka ya kumsemea Rais tena vibaya.

Wako manyang'au wachache ndani ya CCM ambao ukiangali utaona wazi wana mpango wa kuhujumu mchakato wa Katiba mpya. Wengine wamekemewa waziwazi na Mwenyekiti wa Tume ya Katiba na tumewasikia. Sasa hao ndio wanaomshinikiza Rais wa nchi kwa kigezo tu kuwa ni mwenyekiti wa CCM. Tukiangalia maslahi mapana ya Taifa ambayo mimi ninaamini wako watu ndani ya CCM wenye uwezo wa kuona maslahi hayo mapana ya Taifa wakiongozwa na Mwenyekiti wao hao ni wakati wao kujibainisha na kumtia nguvu Mwenyekiti wao ili afanye lile ambalo litajali maslahi ya Taifa hili kwa miaka zaidi ya hamsini ijayo. Manyang'au hawa wanaobweka bila kuwaza wala kupewa ruhusua ya kubweka wakipewa nafasi watalichanachana hili taifa. Na hilo likitokea wao watakua wa kwanza kwenda ughaibuni kwa kuwa tayari wamejiwekea mazingira huko.
 
Mwita Maranya , Hakuna sehemu ambayo nimesema siasa hazibadiliki. Makosa ya kisiasa yanayofanyika siyo kwa sababu siasa hazibadiliki. Moja ya makosa ya kisiasa ni pale kiongozi anaposubiri siasa zimubadilishe (out of control).

Kama waswahili wasemavyo, kutenda kosa siyo kosa bali kurudia kosa. Hiki ndicho kinachotokea kwa sasa kwa wanasiasa wa vyama vya upinzani kwenye mchakato wa katiba mpya ambapo wanasubiri Rais Kikwete na CCM yake iwabadilishe badala ya kuibadilisha.

Kwa sasa Ratiba za kisiasa zimekuwa 'pending' au go haywire kwa sababu mwenye maamuzi ni Rais Kikwete na CCM yake.

Hivi unafahamu kama CCM wako na furaha sana kuhusiana na mchakato kwenda kwa kuchechemea na hasa ikichukuliwa kuwa wanapenda 'kumuongezea' Rais Kikwete muda kisheria pamoja na kwamba wanakanusha kutokana kutokukamilika katiba mpya na pia uchaguzi wa Madiwani taifa kufanyika chini ya katiba ya 1977 "inayoipa" CCM ushindi sunami.

Kuchechemea kwa mchakato kumeifanya hata CHADEMA kushindwa kutekeleza sera yake ya majimbo Zanzibar kwa sababu haifahamu matokeo ya mchakato wa katiba yatakuwaje(serikali mbili au tatu).

Wakati CHADEMA mambo yao yamesimama au yanachechemea huku wakikabiliwa na chaguzi kuu mbili 2014, huku uchaguzi mkuu wa ndani ya chama ukiwa political hot potato. CCM wao wanajiandaa na chaguzi kuu moja.


Watu kama mimi ninaangalia kwa pembeni jinsi viongozi wa vyama vya upinzani wakikosa mwerekeo na nguzo imara katika political case yao kuhusiana na mchakato wa katiba huku Rais Kikwete na CCM yake waki-dictate terms and condition na pia mwerekeo wa upatikanaji wa katiba mpya.

Ni viongozi hawa hawa walisema hawaweI tena kwenda kuonana na Rais kuhusiana na swala la katiba mpya kwa sababu ni "msanii" na katika masaa 24, walichokisema kikawa ni useless baada ya hotuba ya Rais.

Yangu macho na masikio.
siasa za tanzania unapaswa kuzifatilia kwa styl hii,hazina maana wala heshima
 
Nakuheshimu hivyo nisingependa kujibu hili bandiko lako kisha hitimisho lako likawa, nimekuvunjia heshima yako. Uwe na mchana mwema.

[B BAK bado sana kwa upinzani kupewa nchi;
bado hamjakomaa kuweza kuongoza nchi BAK[/B]
 
Kikwete hana pa kujificha ni ama afanye kazi ya wananchi au awafurahishe watu wake akina ndio sasa amezingirwa na saikolojia ya kumkoroga watu wamemtangalia hatua mia mbele yeye anadhani ujanja ujanja utamsaidia , ni bora akatulia na kuanza kuhakikisha wananchi tunapata katiba nzuri ya kutmika miaka mingi ijayo badala ya kujitegesha kusikilizia upepo halafu ndio atoe maamuzi manake sikio moja liko kwa mACCM aliowatuma kukanusha na kutoa kashifa linguine liko kwa wananchi wanaotaka akome kuendesha mchakato wa katiba kwa njia ya usanii
 
Impact ya Rais kukutana na viongozi wa upinzani itakuwa kubwa kwa upande wa CCM sababu walijiapiza hakuna nafasi ya kukutana na Rais au kuwa na majadiliano tena.Kunaweza kukawa na kutokuelewana kati ya pande mbili za wahafidhina ndani ya CCM na wale wenye mlengo wa kati.Imani kwa mwenyekiti wao na viongozi wa serikali itashuka pia.
 
Back
Top Bottom