Serikali yatangaza bei ya kuuzia pamba 2018/2019

PAZIA 3

JF-Expert Member
Jan 30, 2018
1,075
1,864
Bei ya Pamba msimu huu ni Tsh 1100 kwa kilo,hii nikwamjibu wa waziri wa kilimo,Tizeba
My Note: Mpaka sasa sijamjua mtanzania mnyonge anayesaidiwa, maana si mwalimu, mkulima, mfugaji, mvuvi ama mfanyanya biashara, wote WANABAMIZWA tu

========

Serikali imetangaza kushuka kwa bei ya pamba msimu huu, lakini ikawapa habari njema wakulima kwa kufuta deni la zaidi ya Sh30 bilioni kwa wakulima wa zao hilo linalolimwa katika mikoa 17 nchini.

Chanzo: Mwananchi
 
Bei ya Pamba msimu huu ni Tsh 1100 kwa kilo,hii nikwamjibu wa waziri wa kilimo,Tizeba
My Note:Mpaka sasa sijamjua mtanzania mnyonge anayesaidiwa,maana si mwalimu,mkulima,mfugaji,mvuvi ama mfanyanya biashara,wote WANABAMIZWA tu
Kutoka 1,300 ya msimu uliopita!!! Bora soko huria tu
 
kwa wakulima wao bei ikiwa hairidhishi wana haki ya kuchagua kulima au kuacha zao kama wakulima wa mbaazi
 
Mi sielewi hata mnalalamika nini anayepanga bei ni soka ama waziri siajabu hapo wasingepanga bei soko lingeamua iuzwe sh 500 kwa kilo

Ache kutumia kilakitu kama slope kisiasa
 
Na mwaka huu watu wamelima pamba usipime, walijua bei itakuwa nzuri kwa mchepuo wa viwanda
Pamba imezidiwa na mvua za msimu huu...
Kuna uwezekano kwamba mavuno hayatakidhi matarajio ya Watanzania wanyongwe...! Bei nayo ndiyo hiyo ya Tanzania ya wanyonge...
 
Hata korosho mlibeza hivi hivi
Mkuu mvua ni nyingi sana...pamba haijazaa....bei nayo sio nzuri madawa yanayoletwa Na shirika sio mazuri tunajinunulia ya bei ghali.....

Hiyo bei ya kuuzia unaona sawa?

Kuna wazee hata ukiwaambia kilo sh 5,000 hawalimi sababu ni hizi.

Unalima kwa jasho mwisho Wa siku unapangiwa bei...Na huna pengine pa kuuza.....
 
Bei ya Pamba msimu huu ni Tsh 1100 kwa kilo,hii nikwamjibu wa waziri wa kilimo,Tizeba
My Note:Mpaka sasa sijamjua mtanzania mnyonge anayesaidiwa,maana si mwalimu,mkulima,mfugaji,mvuvi ama mfanyanya biashara,wote WANABAMIZWA tu
Mkulima hawezi kunufaika na mazao yake mpaka wanasiasa waingie katika kilimo ndipo wakulima watanufaika, hii ni kwasababu hawana mtu anae waonea uchungu kwa jasho lao, viongozi na wafanyabiashara wote wanyonyaji tu.
 
Back
Top Bottom