Serikali yatangaza bei ya kuuzia pamba 2018/2019

Duuh! Kiukweli nimewaonea huruma mnoo wakulima,,,,,hapo anunuaye atapata mafuta, mashudu na pamba kwa 1100
 
Kwa nini sisi wakulima hatuna mtetezi? Hao wanaokaa kupanga bei Nina mashaka kama wanajua pamba inavyotutesa.
 
Serikali ya awamu hii inafanyia kazi kwenye Mic tu...ni mwendo wa kutangaza na kutoa statisitics tu.
 
Bodi ya pamba msaidie kutoa ufafanuzi kanuni kukokotoa bei elekezi kuondoa ukakasi huu.
 
Mi sielewi hata mnalalamika nini anayepanga bei ni soka ama waziri siajabu hapo wasingepanga bei soko lingeamua iuzwe sh 500 kwa kilo

Ache kutumia kilakitu kama slope kisiasa
Kweli huwezi kujua watu wanalalamikia nini?
Bei ya pamba msimu ulopita 2017/2018 ilikuwa 1200tsh kwa hapa Tanzania.
Ni kweli bei ya zao lolote huwa inategemea soko lake la ndani na nje pia, pamba tunayolima soko lake huwa ni nje. Na kwa sasa soko la nje(India) la pamba limepanda.
Iweje mwaka huu ishuke bei wakti soko la nje limezidi kuimarika?

Haya ndo madhara ya Monopoly Market.
Tanzania mwaka huu wamezuia soko huria kwa maana ya makampuni mengine ya pamba kuja kununua pamba kwa wakulima, na kuwa mamlaka vya ushirika kama NYANZA COPERATIVE UNION, SHIREKU na vingine ambapo hv vyama vilikuwa vmekufa.
Unazuiaje soko huria wakati hawa ndo walikuwa wanachochea bei kupanda kwa sababu ya ushindani.
Naona dhahiri serikal haina nia njema na watu wake
 
Kama tutaanzisha viwanda vya nguo basi pamba inatakiwa ishuke mpaka ifikie Sh.500/-
Kinachotakiwa ni kuongeza uzalishaji na soko la uhakika.
Hii itasaidia viwanda vyetu viweze kuzalisha nguo nyingi na kuziuza kwa bei nafuu.
Then mitumba itakua ni historia.
Tanzania itageuka kuwa kama Thailand kwa kuuza nguo kwa bei nafuu, majirani wote waje kununua nguo Tanzania.

Viwanda vinapokuwa vingi wakulima wanapaswa kuongeza uzalishaji sio kupandisha bei za mazao.
Vinginevyo tutafute mwekezaji tumpe ardhi alime pamba kisasa kwa ajili ya kiwanda chake ili apate faida.
Haya ndiyo yanayosababisha ndoto za viwanda kwa nchi maskini kufa mana wanasiasa wengine wanawahamasisha wakulima wapandishe bei za nazao bila kuangalia uwekezaji wa viwanda na ajira nyinginezo na kodi juu.
 
Kweli huwezi kujua watu wanalalamikia nini?
Bei ya pamba msimu ulopita 2017/2018 ilikuwa 1200tsh kwa hapa Tanzania.
Ni kweli bei ya zao lolote huwa inategemea soko lake la ndani na nje pia, pamba tunayolima soko lake huwa ni nje. Na kwa sasa soko la nje(India) la pamba limepanda.
Iweje mwaka huu ishuke bei wakti soko la nje limezidi kuimarika?

Haya ndo madhara ya Monopoly Market.
Tanzania mwaka huu wamezuia soko huria kwa maana ya makampuni mengine ya pamba kuja kununua pamba kwa wakulima, na kuwa mamlaka vya ushirika kama NYANZA COPERATIVE UNION, SHIREKU na vingine ambapo hv vyama vilikuwa vmekufa.
Unazuiaje soko huria wakati hawa ndo walikuwa wanachochea bei kupanda kwa sababu ya ushindani.
Naona dhahiri serikal haina nia njema na watu wake
Asante kwa kunielewesha
 
Kama watauza kwa njia ya mnada wanaweza kupata zaidi.ila hapa tanzania ni usanii mwingi,maana zao la pamba lilivyopewa promo na wanasiasa mwaka uliopita wakati wao si wanunuzi.Kwa stahili hii graduate wachache ndo watalima,bora utafute mtaji ununue mzigo
 
Back
Top Bottom