Serikali yatakiwa kuwadhibiti wanaouza sukari nje

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,861
30,278
Serikali imeombwa kuwabana wafanyabiashara wanaosafirisha sukari nje ya nchi na hivyo kusababisha uhaba wa bidhaa hiyo hapa.
Rai hiyo ilitolewa jana na Afisa Mtendaji Utawala wa Kiwanda cha Sukari cha TPC cha mjini Moshi, Jaffary Ally, wakati akizungumza na NIPASHE juu ya hali ya
uzalishaji wa sukari kiwandani hapo na hofu iliyopo ya bei ya bidhaa hiyo kuendelea kupanda.

Alitahadharisha kuwa, kama serikali haitawadhibiti wafanyabiashara hao upo uwezekano wa sukari kufika bei ya Sh. 5,000 kwa kilo wakati kiwanda kitakapokuwa hakipo katika uzalishaji kuanzia mwezi Machi hadi
Juni mwakani.

Alisema kwa sasa kiasi cha sukari yote inayozalishwa kiwandani hapo inanunuliwa yote, lakini upungufu wa bidhaa hiyo bado ni mkubwa kiasi cha mfuko mmoja wa kilo 50 kwa mkoa wa Arusha kuuzwa kwa Sh. 120,000.

Alisema hali hiyo inasababishwa na baadhi ya wafanyabiashara kununua sukari kwa wingi na kuiuza nje ya nchi na hivyo kusababisha uhaba wa bidhaa hiyo nchini.

“Nina taarifa kuwa nchi za Sudan Kusini, Somalia, Kenya na Uganda kuna mahitaji makubwa ya sukari na nyingi inatoka hapa nchini, pia bei ya sukari katika soko la dunia imepanda sana, bila udhibiti wa serikali ni wazi wananchi wataendelea kuumia sana” anasema.

Ally aliishauri serikali kupitia maafisa biashara, polisi na
Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kuwabana wafanyabiashara ili sukari ibaki hapa nchini kama inavyofanya kudhibiti biashara ya mahindi.

Naye, Afisa Mkuu Mtendaji wa TPC, Robert Biasaac, alisema kampuni hiyo imetoa bei elekezi kama ilivyotangazwa kwenye tangazo lake la Agosti
19 mwaka huu, likielekeza kuwa mfuko wa sukari wa kilo 50 uuzwe kwa Sh.75,000, kilo 25 kwa Sh. 37,000 na kilo 20 kwa Sh. 32,000.

Alisema kiasi cha sukari kinachozalishwa na kiwanda hicho ni zaidi ya kiwango kinachohitajika, lakini wanashangaa kwanini bidhaa hiyo inakuwa adimu huku ikiuzwa kwa bei kubwa ya Sh. 2,500 kwa kilo moja.

SOURCE: NIPASHE

 

Mwita25

JF-Expert Member
Apr 15, 2011
3,836
1,164
nimekusikia, nitawaambia.....
jumbe kuwafikia, hawatakimbia...
wewe utabakia, kuwashuhudia...
wao wakisimamia, bei kuridhia....
 

mdeki

JF-Expert Member
Mar 28, 2011
3,301
463
serikali haiko makini katika suala la bidhaa mbalimbali hapa nchini siyo sukari pekee
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom