Serikali yataka wananchi watoe taarifa za hospitali zinazotoa matibabu ya wajawazito kwa fedha

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,512
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto imewataka wananchi kutoa taarifa kwa hospitali yeyote inayotoza fedha kwa ajili ya matibabu ya wajawazito wanaokwenda kupatiwa matibabu kwa kuwa huduma hizo zinatolewa bure.

Tamko hilo limetolewa na Naibu wa Waziri wa wizara hiyo Dkt. Faustine Ndugulile, katika mkutano wa 10 kikao cha tano cha Bunge kinachoendelea mjini Dodoma wakati alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa viti maalumu Hawa Mchafu Chakoma alipotaka kujua serikali ili kuwa ina maana gani kusema matibabu kwa wamama wajawazito ni bure.

"Mama wajawazito ni moja ya makundi maalum wanaopaswa kupata huduma za matibabu bure kama ilivyoainishwa katika muongozo wa uchangiaji wa huduma za afya mwaka 1997. Wakina mama wajawazito ni haki yao kupewa huduma zote bila ya malipo na sio zile tu zinazohusu ujauzito", amesema Dkt. Ndugulile.

Pamoja na hayo, Dkt. Ndugulile ameendelea kwa kusema "katika muungozo uliopitiwa mwaka 2009-2010 imetamkwa bayana huduma ya afya kwa mama wajawazito ni bure ikiwa inamaana mara tu mwanamke anapokuwa mjamzito huduma zote kuanzia kliniki ya wajawazito, pale atakapougua maradhi yeyote pamoja na huduma ya kujifungua sanjari na kumuona daktari, kupatiwa vipimo, kupatiwa dawa, kufanyiwa upasuaji pale itakapo hitajika kufanyika hivyo".

Aidha, Dkt. Ndugulile amesema wizara ya afya imeandaa bajeti ya kununua vifaa wanavyotakiwa kutumia wanawake wajawazito ili kuwaondolea adha wafika hospitalini.

"Wizara imeandaa bajeti kutumika kwa ununuzi wa vifaa vinavyohitajika wakati wa kujifungua kwa maana 'delivery parts'. Vifaa hivyo watapewa wakina mama wajawazito wanapokaribia kujifungua ili wawe wanatembea na vifaa hivyo na kupunguza kero kwa kina mama kujinunulia vifaa vyao wao wenyewe", amesisitiza Dkt. Ndugulile.

Kwa upande mwingine, Dkt. Ndugulile amesema serikali inazikumbusha halmashauri kusimamia kikamilifu utekelezaji wa sera hiyo ili wakina mama wajawazito wapate huduma ya kujifungua bure kama muongozo wa uchangiaji wa mwaka 1997 na sera ya afya ya mwaka 2007 inavyoelekeza.

Muungwana
 
Nadhani anamaanisha hospitali za Serikali, hongera sana kwa hili
 
Haya tuko ktk changamoto za elimu bure, tunaletewa jingine. Akili ya kuazima changanya na za shemeji yako aliye na digrii tatu na anasubiria kuajiriwa Kwa zaidi ya miaka 3.
 
Tutoe taarifa hizo basing kwenye hospital zipi,za serikali au pamoja na zila za binafsi?Sidhani kama serikali inapeleka fungu maalumu kwa hospital zote za binafsi kwa ajili ya huduma kwa wajawazito.
 
Hongera sana ,lngefaa sana haya matamko yakitolewa sabamba na uhimizaji wa watu kujitolea damu, kumbuka si dawa pekee inayoweza kuokoa maisha ya kinamama Bali damu nikitu cha mhimu sana hivyo nivema jamii pia ikakumbushwa kuchangia damu, tusijikite tu kusema bure kila kitu ,mzungumzie na vitu vya kuchangia kama damu ili kuondoa mkanganyiko unaoweza kujitokeza
 
Kwani hili nalo la kuuliza, kwani intelijensia wanafanya kazi gani kama si pamoja na hizi, wanataka kujifanya hawajui kama ile ya traffic police wanapokea rushwa openly lakini hakuna mamlaka inawakamata
 
Kuweni makini na hii taarifa. Tangazo hili linazihusu hospitari zote za serikali zilizoko chini ya halmashauri mbalimbali tanzania. Hospitali za mikoa na hospitali za rufaa za mikoa utaratibu wao ni tofauti kabisa. hospitali hizo za mikoa mama mjamzito anatakiwa aende akiwa na barua ya rufaa kutoka katika kituo chochote cha afya au hospitali ya wilaya.Then akifika mkoani ndipo atapata huduma hizo bure. Lakink akija yeye mwenyewe bila utaratibu wa hiyo barua ya rufaa atawajibika na malipo yoyote kama mgonjwa mwingine yeyote
Naomba muwaambie vyema wasije wakaenda na kulianzisha zogo then wakaishia kuaibika.
 
Back
Top Bottom