Wewe, Ndugu au Rafiki mmewahi kukosa Matibabu bora kutokana na kushindwa kutoa 'chochote'?

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,282
Rushwa inapokuwa jambo la kawaida kwenye Jamii, huwafanya Watu kuona ni lazima kutoa Rushwa ili kupata huduma bora, na hivyo kuendeleza tatizo.

Kwenye Vituo vya Afya, Zahanati na Hospitali baadhi ya Wagonjwa hujikuta wakiteseka kwa kukosa Matibabu bora kutokana na kushindwa kutoa Hongo hasa Makundi yanayotakiwa kupewa Huduma bure (Watoto chini ya Miaka 5, Wajawazito na Wazee).

Kutokana na upendeleo na unyanyasaji wa rushwa, inaweza kusababisha kuongezeka kwa matatizo ya kijamii na kiuchumi. Wale wasioweza kutoa rushwa wanaweza kubaki bila huduma sahihi za afya.

Rushwa inaweza kusababisha mianya katika ununuzi wa vifaa tiba na rasilimali nyingine. Hii inaweza kuathiri upatikanaji wa vifaa muhimu na hivyo kusababisha uhaba katika huduma za afya.
 
Kuna hospital nliwahi kwenda wale waliokua wanalipa cash walikua wanahudumiwa chap wale wa bima tulikua tunasotea bench.
 
Kuna vitu watu wengi wanachanganya.

1. Kuna rushwa (corruption) yaani zawadi itolewayo kwa nia ya kutaka upendeleo. Hili ni kosa kijamii na kisheria.

2. Kuna takrima (bribery) ambayo nayo ni aina ya rushwa.

3. Kuna speedy money. Hela ambayo hutolewa ili mtoaji apate huduma nzuri mfano keep change n. k.

Katika utafiti na utaalamu wangu wa sheria za jinai, speedy money haijawahi kuwa kosa la jinai bali ni mtaka huduma anajiongeza ili apate huduma Bora zaidi.

Tofauti kati ya rushwa na speedy money ni kama kupanga kodi na kukwepa kodi ambapo kupanga kodi si kosa bali kukwepa ndiyo kosa
 
Back
Top Bottom