Serikali yataja mafanikio ya Mkongo wa Taifa

Serikali yataja mafanikio ya Mkongo wa Taifa

mshihiri

Senior Member
Joined
Jul 15, 2011
Posts
138
Reaction score
89
SERIKALI imetaja manufaa ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano (NICTBB) na tayari yameongeza ubora na kasi ya matumizi ya intaneti, data na utoaji wa huduma za elimu mtandao kwa baadhi ya taasisi za elimu.

Kauli hiyo ilitolewa Dar es Salaam jana na Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), Dk. Ziapuna Yonah.

Alisema ongezeko la matumizi na faida za mkongo zinaongezeka siku hadi siku na kukidhi matarajio ya Serikali ya kuziba pengo la matumizi ya Tehama kwa wananchi katika maeneo mbalimbali.

“Mkongo wa Taifa una umuhimu mkubwa hata kwa nchi jirani za Rwanda, Burundi, Malawi, Zambia na hata Uganda kwa kuwa zinautegemea katika kuunganishwa na Mikongo ya Kimataifa ya Mawasiliano ya Baharini (SEACOM and EASSy Submarine cables) yenye vituo vilivyo jengwa Dar es Salaam.

“Kampuni za mawasiliano katika nchi ya Kenya tayari zimeanza kuunganishwa katika Mkongo huu wakati kampuni zilizopo Msumbiji zikikamilisha taratibu za ujenzi kuelekea mpakani, huku ambapo Mkongo wa Taifa umefika na hatimaye ziweze kuunganishwa,” alisema Dk. Yonah.

Alisema kukamilika kwa ujenzi wa Mkongo wa Taifa kutaleta mabadiliko makubwa ya utendaji na ufanisi wa kazi serikalini hasa katika maeneo ya elimu mtandao, afya mtandao, kilimo mtandao na huduma nyinginezo.

Alisema Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), imeteuliwa na Serikali kuwa meneja wa Mkongo huo kwa kuusimamia, kuuendesha na kuuendeleza kwa vigezo vya utaalamu walionao pamoja na miundombinu yake ambayo imeenea nchi nzima.

Alisema changamoto kubwa iliyojitokeza ni usalama wa miuondombinu hiyo ambayo imepitia maeneo mbalimbali ya makazi ya watu

gazeti la mtanzania leo 1/2/2013
 
mwalimu wangu alikua ananiambia tofauti ya mtanzania na mkenya ni kua mtanzania computer ikiharibika amepata nafasi ya kupiga story ndo hafany kaz tena wakati mkenya yeye atachukua laptop yake binafsi na kazi zitaendelea kama kawaida.

Hapa yani akili yangu inanambia wakenya/warwanda watafaidika sana na hii project na sisi watanzania tutabaki tunaangalia tu...

Mimi bado sijakua aware na hii ishu so hao ttcl wamepewa kazi ya kusuply je wao watakua monopoly kwa kutoa wao tu au wanatakiwa wawe kama wauzaji wa jumla kusuply reja reja kwa makampuni mengine?

Na kama wanasuply wanaruhusiwa kuuza kwa kampuni kama voda, tigo na airtel au wanauza kwa wale wanaosambaza kwa cable?

Je cost zao zipoje? Kucompare na isp wengine duniani kama nokiasiemens?

Kama kuna mtu ana source mkongawataifa ulipoelezewa vizuri aitoe
 
Back
Top Bottom