Serikali yasitisha mafunzo ya JKT

Serikali yasitisha mafunzo ya JKT

Kichwa Ndio Mtu

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2014
Posts
3,079
Reaction score
1,719
Tuesday, January 27, 2015



jkt3-640x360.jpg

Baadhi ya vijana wanaochukua mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)
Serikali imesitisha mafunzo ya JKT kwa mwaka huu. Kwa hiyo wale vijana waliokua wanategemea kuanza mafunzo hayo mwezi wa pili (tano) mwaka huu, mafunzo hayo hayatakuwepo tena.

jkt1-640x360.jpg


Wahitimu mafunzo ya awali ya kijeshi kenye kambi ya JKT Ruvu kikosi cha singe wakiwa katika maonyesho ya kivita kwenye sherehe za kuhitimu mafunzo hayo
Sababu ya kusitisha mafunzo hayo ni ukata unaoikabili serikali.


jkt-600x360.jpg



Vijana waliohitimu mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) katika Kikosi cha Ruvu, Kibaha, mkoani Pwani kwa mujibu wa sheria wakionyesha umahiri wao wa kuruka moto

Chanzo:
Gazeti la Jamhuri


Maoni yangu:

Mafunzo haya ya JKT yapigwe marufuku kabisa na yafutwe maana hayana faida yoyote wala tija katikaTaifa hili. Binafsi natamani serikali ifilisike kabisa ili isiweze kufadhili mafunzo hata tena.

=================

Kanusho la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kuhusu kusitisha mafunzo ya Jeshi kwa mujibu wa Sheria.
jkt.png

 
nani kadunganya serikali imeshndwa hela za kuifandili jakata?
 
Kuna faida na hasara za kupeleka vijana wengi JKT na kuwatupa uraini bila ajira... siku hawa wakiasi itakuwa ni mtafutano, iko wazi kwamba police hawataweza kupambana nao na hivyo kupekea kupambana na wanajeshi wenzao

Ni bora yasitishwe kwa mstakabali mwema wa taifa
 
Serikali ya CCM haina priority kila kiongozi akija anakuja na mambo yake tena kwa kukurupuka,kama ni kweli wala haitashangaza.
 
Wameshtuka eeh. Vijana wakakamavu kuundamana kuelekea ikulu kudai ajira si jambo dogo. Lazima status qou ishituke. Mikakati ni kupromote bongo flava siyo mafunzo ya kijeshi.
 
Msemaji wa hiyo kauli wa kusitisha ni nan?
 
Wenzetu wanaweka mkazo kufudisha vijana wao ujasiliamali na tecnolojia, sisi tumekazana kuifundisha jamii uasikali!
 
itakuwa maajabu ukisema serikali haina hela wakati watu wanaiba mabilioni ya hela kila mwaka je hizo hela zinatoka wapi kama serikali haina hela
 
JKT iendelee angalia hapa vijana walivyowakakamavu safi sana hapa ni parade ya kumaliza mafuzo.
 
Last edited by a moderator:
Serikali imesitisha mafunzo ya JKT kwa mwaka huu. Kwa hiyo wale vijana waliokua wanategemea kuanza mafunzo hayo mwezi wa pili mwaka,mafunzo hayo hayatakuwepo tena.

Sababu ya kusitisha mafunzo hayo ni ukata unaoikabili serikali,serikali haina hela.

MAONI YANGU. Mafunzo haya ya JKT yapigwe marufuku kabisa na yafutwe maana hayana faida yoyote wala tija katikaTaifa hili. Binafsi natamani serikali ifilisike kabisa ili isiweze kufadhili mafunzo hata tena.

Chanzo: Gazeti la Jamhuri.

Wamesitisha mafunzo ya mujibu wa sheria au wamesitisha wa kujitolea hapo hujaeleweka mkuu umecreat uncertainity kwa raia
 
kwa kweli mimi naona haya mafunzo ya JKT walipaswa kushirikiana na VETA wawafundishe vijana vitu vya maana. UKAKAMAVU bila ajira ni sawa na UPROFESA bila HELA.
 
Back
Top Bottom