Serikali yasalimu amri: yaagiza kuondolewa kwa vifaa vibovu vya kupima HIV | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yasalimu amri: yaagiza kuondolewa kwa vifaa vibovu vya kupima HIV

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jan 6, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jan 6, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Wiki iliyopita tuliandika kuhusu kile ambacho tuliamini kuwa ni uzembe mkubwa katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ambapo iliachia kwa muda wa karibu miezi miwili kutoa tamko la kuagiza vifaa vibovu vya kupimia HIV vya SD Bioline ambavyo vilitangazwa na WHO kuwa ni vibovu na vinatakiwa kuondolewa kwa matumizi.

  Serikali hatimaye imeamua kuondoa vifaa hivyo lakini haijatoa maelezo ya wazi ya nini kifanyike na nani afanye na vipi ifanyike katika kuviondoa vifaa hivyo. Hatujaelewa ni kwanini serikali imechelewa kutoa agizo hilo na ni kwanini Mganga Mkuu hajawajibishwa kutokana na hili.

  Kuna vitu vya kuchezea lakini wanapochezea hadi maisha ya Watanzania wanakuwa wanazidi kuthibitisha kuwa wamepoteza uhalali wa kuitwa "viongozi"! This is just shameful! Natumaini wabunge wenye ujasiri watataka maelezo yatolewe kwenye kikao kijacho cha Bunge:

  [h=1]TANZANIA: Government recalls faulty HIV test kits[/h]
  [​IMG]
  The UN World Health Organization has issued an alert on the test kit, which failed quality assurance tests (file photo)
  DAR ES SALAAM, 6 January 2012 (PlusNews) - Tanzanian health authorities have announced the withdrawal of a South Korean HIV test kit from circulation following warnings about its poor quality.

  In November, the UN World Health Organization removed the Standard Diagnostics BiolineĀ® HIV 1/2 3.0 Rapid HIV Test Kit from its list of approved rapid test kits with immediate effect; the alert was issued after Bioline failed quality assurance tests.

  The Tanzanian government has followed neighbouring Kenya [ PlusNews Global | KENYA: New guidelines follow recall of faulty HIV test | Kenya | Education | Governance | HIV/AIDS (PlusNews) | Prevention - PlusNews ] in issuing an immediate recall of all Bioline testing kits in the country.

  "What we know so far is that 1,178 test kits have been used in the field, but we have yet to substantiate exactly how many of them were defective," Hadji Mponda, Tanzania's Health Minister, said at a news conference on 5 January.
   
 2. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #2
  Jan 6, 2012
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Serikali inakusikiliza.Ungekua mogul sasa hivi kama ungekua na hatimiliki ya ushauri wote walioiba kwako, ingawa wabishi kukubali.
  Yale mapambano yako ya kifikra yanaanza kuzaa matunda.
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Jan 6, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280

  Lakini kwanini hadi tuandike kama kwa kuwashtumu? Sasa hivi kuna kashfa ya Omar Nundu; nayo naogopa hata pa kuanzia kwa sababu unajiuliza why? Hivi ni kweli serikali haiwezi kufanya kazi bila kusukumwa na kuibuliwa kwa kashfa?Kwanini tusubiri hadi kashfa?
   
 4. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #4
  Jan 7, 2012
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Eng. Nundu ana kashfa gani tena? Huyu si aliletwa kusafisha madudu ya wizara hii? Du..kweli tumeshindikana.
   
 5. myhem

  myhem JF-Expert Member

  #5
  Jan 7, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Yaani hii nchi sasa hivi nadhani kinachotokea ni kama fungulia mbwa ambapo JK ameamua kuacha kila aliyepewa dhamana afanye anavyotaka na hatamfanya lolote.Hii ni kashfa ambayo tulitegemea kusikia watu wanaachia ngazi lkn itakuwa business as usual! Kama kina Dr.Hosea,Utuoh,Luhanjo wanaendelea kupeta na wengine mpaka wanafikia ukomo wa utumishi wao unategemea nini?

  Kibaya zaidi hata bunge letu limekuwa TOOTHLESS kwani maazimio yake yanadharauliwa na ikulu.
   
 6. myhem

  myhem JF-Expert Member

  #6
  Jan 7, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Just imagine watu ambao wamepima kwa hivyo vifaa halafu majibu yake yakawa si sahihi! Yaani asiye na ngoma kaambiwa kuwa anayo na mwenye nayo kaambiwa kuwa hana!
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Jan 7, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, kupiitia Bohari ya Dawa (MSD) imesitisha uagizaji wa vifaa vya kupimia Ukimwi ambavyo havikuwa na ubora wa kutosha.
  Vifaa hivyo aina ya SD Bioline vilivyokuwa vikitengenezwa na kampuni ya moja ya Korea vilikuwa na hitilafu ya kushindwa kutoa matokeo ya upimaji kwa asilimia 20-50.

  Hayo yalisemwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Haji Mponda jijini Dar es Salaam jana wakati akiongea na waandishi wa habari.

  "Hivi sasa vipimo hivi vitakaguliwa baada ya kuwasili nchini kabla ya kusambazwa katika vituo mbalimbali vya afya nchini," alisema.

  Alisema vipimo hivyo kabla ya kutumika ni lazima vidhibitishwe na Shirika la Afya Duniani (WHO) au mashirika mengine ya kimataifa na hatimaye kusajiliwa na mamlaka husika ikwemo Bodi ya Maabara Binafsi za Afya na Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA).

  Pia, kutafanyika tathmini ya upya ya Mfumo wa Taifa wa vipimo vya haraka vya maambukizi ya ukimwi (Evakuation of Nataonal HIV Rapid Testing Algorithim) ambayo itajumuisha vipimo vyote ambavyo vimethibitishwa na WHO na kusajiliwa.
  CHANZO: NIPASHE
   
 8. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #8
  Jan 7, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Mwanakijiji, uliwahi kuisikia hii:

  X: I hate being pushed around and please stop talking behind my back , dude !
  Y: What else did you expect me to do, you are on a wheelchair, stupid !

  Our government is on a wheelchair !
   
Loading...