Tanzania Yasitisha Matumizi ya Dawa ya Kikohozi kwa Watoto

Wild Flower

Member
Jul 20, 2023
88
105
Mamlaka za kudhibiti dawa za Tanzania, Rwanda na Zimbabwe zimesitisha toleo la dawa za kikohozi za watoto za kampuni ya Johnson & Johnson, kama hatua ya tahadhari baada ya mamlaka za Nigeria kusema vipimo vilionesha kuwepo na kiwango kikubwa cha sumu.

Nchi hizo zinaungana na Nigeria, Kenya na Afrika Kusini kuondoa dawa hizo madukani, ambazo hutumika kutibu kikohozi kwa watoto. Afrika Kusini imesitisha matokeo zaidi limesema shirika la habari la Reuters.

Vipimo vya maabara kwenye dawa hizo vilivyofanywa na mamalaka ya udhibiti wa dawa ya Nigeria ilionesha kuwepo kwa kiwango kikubwa cha kemikali ya diethylene glycol, ambayo imehusishwa na vifo vya watoto kadhaa nchini Gambia, Uzbekistan na Cameroon tangu mwaka 2022.

Toleo hilo la Benylin lililoondolewa madukani lilitengenezwa na kampuni ya J&J ya Afrika Kusini Mei 2021, ingawa kampuni ya Kenya ya Kenvue sasa inamiliki aina yake.

Mamlaka ya udhibiti wa dawa ya Tanzania -TMDA- ilisema ilianza kusitisha matumizi ya dawa hizo Aprili 12 baada ya kusikia kuhusu matokeo ya vipimo vya Nigeria.

"Zoezi hili halihusishi uchunguzi bali kufuatilia mwenendo na kuhakikisha dawa zenye hitilafu zinaondolewa madukani," msemaji wa TMDA Gaudensia Simwanza aliiambia Reuters siku ya Jumatatu.

Msemaji wa mamlaka ya Kenya alisema matokeo ya vipimo kwenye dawa hiyo huenda yakatolewa siku ya Jumatano
================================
Drug regulators in Tanzania, Rwanda and Zimbabwe have recalled a batch of Johnson & Johnson (JNJ.N), children's cough syrup as a precautionary measure after their Nigerian counterpart said laboratory tests found high levels of toxicity.

The countries join Nigeria, Kenya and South Africa in recalling the same batch of the syrup, which is used to treat coughs, hay fever and other allergic reactions in children. South Africa has also recalled an additional batch.

Laboratory tests on the syrup by Nigeria's health regulator showed a high level of diethylene glycol, which has been linked to the deaths of dozens of children in Gambia, Uzbekistan and Cameroon since 2022 in one of the world's worst waves of poisoning from oral medication.

Diethylene glycol is toxic to humans when consumed and can result in acute kidney failure.
The batch of Benylin Paediatric syrup recalled was made by J&J in South Africa in May 2021, although Kenvue (KVUE.N), opens new tab now owns the brand after a spin-off from J&J last year.

Tanzania Medicines and Medical Devices Authority (TMDA) said it had begun the recall on April 12 after hearing about the Nigerian test results.

"This is an exercise that does not involve investigation but rather monitoring to ensure that those affected drugs are removed from the market," TMDA spokesperson Gaudensia Simwanza told Reuters on Monday.
A spokesperson for Kenya's drug regulator said its test results on the syrup would likely be ready on Wednesday.

"A review of our safety database doesn't reveal any adverse events reported," the Rwanda Food and Drugs Authority said in a statement dated April 12. "However, Rwanda FDA issues the present recall for precautionary measures."

Zimbabwe's Medicines Control Agency said that it did not have a record of the product's importation into Zimbabwe, but that it was concerned the syrup could enter the local market illegally. It said it would step up inspections in case.
SOURCE: REUTERS
 
Hata poda zao zilikuwa reported zina madhara makubwa.

Hii kampuni kwa nini haichukuliwi hatua
 
hawa jamaa siamin kama ni bahat mbaya naamin kabisa wanampango mkakati na human population walikua powder zao zilizua taharuk kipind flan na bado kuna majasiri walidungwa chanjo zao
 
Kwa hiyo hadi MAMLAKA za NCHI zingine zigundue ndo TMDA nanyi mchukue maamuzi....!!!!!!!!????
WTF wasingesema? Nyie bnafsi hamuwezi kufanya kazi kwa kujjiamini? Na kwa nini ninyi msiwe wa kwanza kugundua hilo!!?? I do remember, Hayati Magufuli aliwahi challenge vipimio vya COVID na tukagundua jambo..... ila mmelala sana TAASISI NYINGI za BONGO
 
Kiukweli huwa hamna dawa ya kikohozi
Ni ujanja ujanja tu na hii hata mtu aliyesomea udaktari anajua
 
Kiukweli huwa hamna dawa ya kikohozi
Ni ujanja ujanja tu na hii hata mtu aliyesomea udaktari anajua
Madawa ni biashara.

Natamani ningekuwa nina HISA kwenye pharmaceutical companies, haki ya Mungu ningekuwa TRILLIONAIRE.

Manyumbu ni mengi mno, unavuna tu utajiri kiulaini.

I wish i could be 😭😭 Magufuli uko wapi 😭😭😭
 
Kuna Mahali Tanzania tunakwama pakubwa.
TMDA hao hao wanatakiwa wafanye QA(QC) na majukumu mengi kama yote waliyo nayo hiyo QC huwa wanafanya saa ngapi? au ndo hufanya kwa kujiskia?
Na sina uhakika na maabara zetu za dawa za +255 kama zinaweza perform QC za dawa nyingi juu ya PAIs na non PAIs zinazopatikana ktk kila dawa inayoingia sokoni. Sasa mpaka nchi zingine zigundue Na Sisi ndo tucopy?
 
Naombeni picha hata moja ya mfano wa dawa hiyo maana kuna mtoto anatumia dawa ya kikohoji na tumeinunua juzi tu
 
hawa jamaa siamin kama ni bahat mbaya naamin kabisa wanampango mkakati na human population walikua powder zao zilizua taharuk kipind flan na bado kuna majasiri walidungwa chanjo zao
Hizo powder, mafuta mpaka sabuni za kuongea kwa watoto mbona bado zipo madukan?
 
Back
Top Bottom