Serikali yasalimu amri sheria ya takwimu

Serikali yasalimu amri sheria ya takwimu

Trust None

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2018
Posts
1,260
Reaction score
4,421
Huu ni ushindi kwa mabeberu waliokatalia baadhi ya misaada,
wakishinikiza sheria ibadilishwe.


Screenshot_20190628-073038.png

Screenshot_20190628-074140.png


BUNGE limefuta kifungu cha 37(4) cha Sheria ya Takwimu kinachotoa adhabu kwa mtu anayetoa taarifa za takwimu bila kupata kibali cha Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).

Katika kifungu hicho cha 37 (4) kabla ya kupendekezwa kufutwa katika marekebisho yaliyopelekwa bungeni na kisha kupitishwa, adhabu kwa makosa ya jinai katika Sheria ya Takwimu ilikuwa ni miezi sita jela au kulipa faini isiyopungua Sh. milioni mbili au vyote viwili.

Makosa kwa mtu yeyote kutoa taarifa zilizopatikana isivyo halali, adhabu yake ni kifungo kisichopungua miezi 12 au faini isiyopungua Sh. milioni tano au vyote viwili.

Katika marekebisho ya Sheria ya Takwimu (Sura ya 351) iliyosomwa Bungeni na Prof. Kilangi, yanaeleza kuwa marekebisho ya jumla yanayopendekezwa katika sheria hiyo yanalenga kubainisha dhahiri haki ya kuchapisha au kutoa taarifa za takwimu kwa umma.

Kwa maelezo ya Mwanasheria Mkuu huyo wa serikali, mapendekezo hayo yanakusudia kuanzisha Kamati ya Kitaalamu (Technical Committee) ambayo jukumu lake litakuwa kupokea kujadili malalamiko yanayotokana na wadau kuhusu usahihi wa takwimu zilizotolewa kwa umma.

"Katika jedwali la marekebisho, inapendekezwa kufuta vifungu vya 24A na 24B na kuviandika upya, pia kuongeza vifungu vipya vya 24C, 24D, 24E na 24F kwa lengo la kuweka utaratibu wa kutoa matokeo ya takwimu zinazotofautiana na takwimu rasmi zilizotolewa na serikali," alisema Kilangi.

Kwa mujibu wa Mwanasheria Mkuu, marekebisho hayo yanatoa fursa kwa mtu yeyote kutoa takwimu zinazotofautiana na zilizotolewa na serikali, iwapo atakuwa amezingatia misingi ya kitakwimu iliyowekwa katika miongozo mbalimbali ya kitaifa na kimataifa inayosimamia utoaji wa takwimu.

Lakini, sambamba na marekebisho hayo sheria hiyo inapendekeza kufutwa kwa kifungu cha 37 (4) kinachotoa adhabu kwa mtu anayetoa taarifa za takwimu bila kupata kibali cha Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).

Rejea https://www.ippmedia.com/sw/habari/bunge-lafuta-adhabu-sheria-ya-takwimu

---------
"Don't start what you can't finish!"

anyway, poleni Taifa Stars, pole mh. Makonda na poleni Watanzania wote.
 
Kujifanya jeuri na kuwaita mabeberu wakati tunahitaji msaada wao tunaenda kuomba. Wametunyima hela, miradi kuendelea isingewezekana hatimaye tumesalimu amri na huo ni mkopo tu.
 
Njaa haina baunsa....
Magufuli alijifanya yeye ni kidume kumbe Hana lolote sikuzote hapa duniani huwezi kuwanyamazisha watu Kwa Sheria za hovyo mwisho wa siku utashindwa Tu.

Safi Sana mabeberu na pia tunawaomba huyu mtu asipewe pesa Hadi Sheria zingine za kishamba aziondoe
 
Hahaha usiwaamini ccm, wakiishapata pesa za world bank wanaweza kuirudisha kwa hati ya dharula hiyo sheria waliyoitoa. Kwa sasa wanataka kuwapumbaza mabeberu.
Masikini hana jeuri Kwa tajiri,baki Na jeuri yako nibaki Na Pesa zangu.
 
Mabeberu kiboko ya jiwe,Nyerere aliwavimbia mabeberu kulinda heshima akaona ang'atuke.Njaa haina baunsa.
 
Pamoja na yote tunayowalaumu Wazungu, hawa Wazungu wana huruma zaidi na waafrika kuliko Watawala wengi wa nchi za kiafrika.

Kama laiti hawa wazungu wasingekuwepo, sijui dunia ingekuwaje.

Kuna mijitu ina roho za ajabu, na nimiafrika, lakini kila siku inaota na kufikiri ni jinsi gani itaweza kuwatesa, kuwafunga, kuwateka na kuwaua binadamu wenzao. Mijitu ya namna hiyo kamwe haitapata baraka Duniani wala mbinguni maana imeishi Duniani ikimwakilisha shetani aliye chanzo cha hadaa na mateso ya wanadamu.

Sala zetu kwa Mungu wa kweli, hawa walio mawakala wa shetani, wazidi kuanikwa na uovu wao ukakae hadharani ili kila aliye na roho ya Mungu apate kuuona.
 
Watutafutie pia nani alimshambulia rais wetu mpendwa ajaye wao walijifanya kumpuuza eti hawajulikani sasa wanaanza kukiona cha moto. Hakuna jiwe juu ya jiwe litakalo salia halita fikishwa mahakama ya uhalifu ya kimataifa.
 
Pamoja na yote tunayowalaumu Wazungu, hawa Wazungu wana huruma zaidi na waafrika kuliko Watawala wengi wa nchi za kiafrika.

Kama laiti hawa wazungu wasingekuwepo, sijui dunia ingekuwaje.

Kuna mijitu ina roho za ajabu, na nimiafrika, lakini kila siku inaota na kufikiri ni jinsi gani itaweza kuwatesa, kuwafunga, kuwateka na kuwaua binadamu wenzao. Mijitu ya namna hiyo kamwe haitapata baraka Duniani wala mbinguni maana imeishi Duniani ikimwakilisha shetani aliye chanzo cha hadaa na mateso ya wanadamu.

Sala zetu kwa Mungu wa kweli, hawa walio mawakala wa shetani, wazidi kuanikwa na uovu wao ukakae hadharani ili kila aliye na roho ya Mungu apate kuuona.




Aiseeeeee
 
Back
Top Bottom