Chrismoris
JF-Expert Member
- Oct 27, 2017
- 14,544
- 18,432
Baba Jesca amebanwa hadi kasalimu amri.
Wazungu wanasema
Who pays the piper chooses the tune.
Wazungu wanasema
Who pays the piper chooses the tune.
'PRAISE TEAM' MKO WAPIIIIIII?????...
MKUJE HUKUUUUUI....
Yaleyale yakudharau wakunga wakati uzazi bado upo, au kumtukana mamba wakati haya mto hujauvuka!
Huu ni ushindi kwa mabeberu waliokatalia baadhi ya misaada, wakishinikiza sheria ibadilishwe.
Hahaha mtaani kuna msemo " masikini hana tabia, mpe pesa utamjua tabia yake halisi",Masikini hana jeuri Kwa tajiri,baki Na jeuri yako nibaki Na Pesa zangu.
Hahaha ngoja wazipate mtasikia, kwanza tutaambiwa ni za ndani, pili tutasikia hatupangiwi. Hao ccm akili zao wanazijua wenyewe.Hawawezi, fedha hizo zina masharti, zinaweza kuwatokea puani
Hahaha walisema tunatumia pesa zetu, hiyo 40% umeitoa wapi?! Usiwachonganishe na wapiga kura wao.Hapumbaziki mtu hapa. Ni mapoyoyo wenyewe ndo wanaojipumbaza......!!
Hiyo jeuri ya Magufuli na CCM wanayo? Mtu anayekupa misaada kwa zaidi ya 40% ya Bajeti yako kwa mwaka siyo mtu wa kumpuuza na kumdharau hata kidogo...!!
Mabeberuu sio wajinga kiasi hichooHahaha usiwaamini ccm, wakiishapata pesa za world bank wanaweza kuirudisha kwa hati ya dharula hiyo sheria waliyoitoa. Kwa sasa wanataka kuwapumbaza mabeberu.
Wakina polepole Katika hili hutawasikiaMpaka wabanwe ndio huamka.haya ile timu ya kuunga mkono pingeni sasa. maana tulipopinga mkasema sisi sio wazalendo sasa sijui na serikali yenu sio wazalendo ama vipi??
Haya marekebisho yamekaa vizuri sababu yanatoa haki kwa mwongo wa takwimu kuchukuliwa hatua na aliyeumizwa na uongo wa kitakwimu.Haki hiyo kwenye Sheria iliyopita haikuwemo.Mfano Mimi nimezuliwa kitakwimu kuwa nimezaa watoto 40 nje ya ndoa.Sheria imenipa mwanya wa kulishughulikia Hilo kikamilifu.Hii Sheria hairuhusu uzushi inatoa Uhuru wa kutoa takwimu zozote ila mtoa takwimu a beware kuwa hizo takwimu Kama zitakuwa na tatizo zikaumiza mtu huyo mtu ana Uhuru wa kupambana na huyo mtoa takwimu Koko.Iwe mahakamani au popote.Haijatoa Uhuru holela usio na mipaka wa kujipikia takwimu zozote za kujitungia au kuokota majalalani.Sasa hivi Ni kuwa kila mtoa takwimu anatakiwa kujua kuwa Kuna Risk factor kwenye takwimu zake.
Kiongozi pole wape hip time ya ccm na wanaccm wenyewe sio watanzania wote, hasa mwenyekiti wao, makonda and co.Huu ni ushindi kwa mabeberu waliokatalia baadhi ya misaada,
wakishinikiza sheria ibadilishwe.
View attachment 1140658
View attachment 1140668
BUNGE limefuta kifungu cha 37(4) cha Sheria ya Takwimu kinachotoa adhabu kwa mtu anayetoa taarifa za takwimu bila kupata kibali cha Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).
Katika kifungu hicho cha 37 (4) kabla ya kupendekezwa kufutwa katika marekebisho yaliyopelekwa bungeni na kisha kupitishwa, adhabu kwa makosa ya jinai katika Sheria ya Takwimu ilikuwa ni miezi sita jela au kulipa faini isiyopungua Sh. milioni mbili au vyote viwili.
Makosa kwa mtu yeyote kutoa taarifa zilizopatikana isivyo halali, adhabu yake ni kifungo kisichopungua miezi 12 au faini isiyopungua Sh. milioni tano au vyote viwili.
Katika marekebisho ya Sheria ya Takwimu (Sura ya 351) iliyosomwa Bungeni na Prof. Kilangi, yanaeleza kuwa marekebisho ya jumla yanayopendekezwa katika sheria hiyo yanalenga kubainisha dhahiri haki ya kuchapisha au kutoa taarifa za takwimu kwa umma.
Kwa maelezo ya Mwanasheria Mkuu huyo wa serikali, mapendekezo hayo yanakusudia kuanzisha Kamati ya Kitaalamu (Technical Committee) ambayo jukumu lake litakuwa kupokea kujadili malalamiko yanayotokana na wadau kuhusu usahihi wa takwimu zilizotolewa kwa umma.
"Katika jedwali la marekebisho, inapendekezwa kufuta vifungu vya 24A na 24B na kuviandika upya, pia kuongeza vifungu vipya vya 24C, 24D, 24E na 24F kwa lengo la kuweka utaratibu wa kutoa matokeo ya takwimu zinazotofautiana na takwimu rasmi zilizotolewa na serikali," alisema Kilangi.
Kwa mujibu wa Mwanasheria Mkuu, marekebisho hayo yanatoa fursa kwa mtu yeyote kutoa takwimu zinazotofautiana na zilizotolewa na serikali, iwapo atakuwa amezingatia misingi ya kitakwimu iliyowekwa katika miongozo mbalimbali ya kitaifa na kimataifa inayosimamia utoaji wa takwimu.
Lakini, sambamba na marekebisho hayo sheria hiyo inapendekeza kufutwa kwa kifungu cha 37 (4) kinachotoa adhabu kwa mtu anayetoa taarifa za takwimu bila kupata kibali cha Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).
Rejea https://www.ippmedia.com/sw/habari/bunge-lafuta-adhabu-sheria-ya-takwimu
---------
"Don't start what you can't finish!"
anyway, poleni Taifa Stars, pole mh. Makonda na poleni Watanzania wote.