ntwara oyeee
Terms zitakuwa mbovu tu. Je, gesi na mafuta hayo ni kwa ajili ya ku-export au kwa matumizi ya mtanzania?
Terms zitakuwa mbovu tu. Je, gesi na mafuta hayo ni kwa ajili ya ku-export au kwa matumizi ya mtanzania?
Wadanganyika mnasheherekea hata mkataba hamjauona!! Huko nyuma serikali ilisema hivyo hivyo walipotiliana saini na kampuni ya SONGAS, lakini toka kampuni hii ianze kuchimba gas huko kusini bei ya umeme haijapungua kama tulivyoahidiwa wala ile ya cement; ingawa kiwanda cha twiga cement kinatumia gas katika uzalishshaji. Katika mikataba hii mara nyingi tunaliwa kwasababu hao wanaotia saini hawasomo zile fine prints ambazo huwa zinakuwa na vipengele muhimu na hatari katika mikataba; kama mnavyojua viongozi wetu ni wavivu kusoma na ndio maana huwa wanapokea hata cheki zenye tarakimu tofauti na maandishi!! Hawataki kutuonyesha mikataba kwasababu wataumbuka na ufisadi wao kama si hivyo kwanini wafiche?.
Nimeona hii na maoni yangu hapa ni kuwa kuna utata kwenye hii figure siamini kama hii kampuni ina ubavu wa kupata dola bilioni saba, na vilevile sijawahi kusikia kampuni yeyote ikitumia kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya exploration (utafutaji) tofauti na development(kuendeleza). Ukweli ni kuwa kazi ya exploration ni kama kamari unaweza kupata au kukosa.
Sasa mi siamini hii figure kwa pointi zifuatazo;
Ophir wenyewe kama alivosema mdau mmoja hapo juu wana cash USD135m sasa vipi watumie dola bilioni 7 (zaidi ya mara 50!) kwa kamari, haiingii akilini.
- Hii kampuni Ophir haina ubavu wa ku raise 7 billion for exploration.
- Hakuna kampuni yeyote ya mafuta (including majors yaani BP, Exxonmobil etc) ambayo inatumia kiasi hicho cha pesa kwa ajili ya utafutaji wa mafuta, kama ni development sawa hiyo ni issue nyingine.
- Kwa vile East Africa ni new frontier, yaani ni eneo jipya la exploration kawaida ni kampuni ndogondogo ndio hufanya exploration kwa kati ya USD 10mil to Usd 60mil na sio hiyo figure.
Watanzania hesabu zinasumbua sana.
Ila ni muhimu kwa hizi kampuni kuendelea kufanya exploration kwa sababu sisi hatuna hizo hela na pili si vema tutumie hela za walipa kodi kuchezea kamari.
mmmh.. hivi ule mkataba wa IPTL haufanani na huu... ? Mbona tayari kuna makampuni mengine mengi tu ambayo yanatafuta gas na mafuta nchini? Kama serikali inaubia inaubia kupitia chombo gani, taasisi gani au kampuni gani? Maana nakumbuka hata kwenye Meremeta serikali ilikuwa na ubia kupitia Tangold ambayo warithi wake walikuwa ni familia za kina Chenge!