Serikali yasaini makubaliano ya ujenzi wa Barabara ya Arusha-Holili

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
attachment.php


Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imesaini mkataba wa makubaliano ya awali ya ujenzi wa barabara kutoka Arusha mpaka Holili.

Makubaliano hayo yamesainiwa na Mkurugenzi wa Barabara kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Ven Ndyamukama kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Naibu Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano (JICA) Bw Hideyuki Manioka kwa niaba ya Serikali ya Japan.

Mhandisi Ven Ndyamukama amesema kuwa Tanzania imesaini mkataba huu wa awali ambao baada ya majadiliano ya awali kati ya Tanzania na Japan, serikali ya Japan itatoa mkopo wa riba nafuu kwa serikali ya Tanzania ili kuwezesha kuanza kwa utekelezaji wa mradi huu mapema Machi mwakani.

Wamekuja kufanya utafiti na kufatilia taarifa tulizo nazo kuhusu mradi huu na kupeleka taarifa serikali ya Japan na tunategemea June mwakani kusaini hati ya kupata mkopo ambao utawezesha ujenzi wa barabara hii, alisema Mhandisi Ndyamukama.

Pia ameongeza kuwa baada ya mkopo huo kutolewa wao kwa upande wao wamejipanga katika kufanya mradi huo ukamilike kwa wakati ikiwemo upatikanaji wa wakandarasi kwa ajili ya mradi huo.

Aidha Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano (JICA) Bw Hideyuki Manioka amesema kuwa wataendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kusaidia miradi mbalimbali ya maendeleo.

Mradi huu wa barabara toka Arusha mpaka Holili yenye urefu wa kilometa 105 umefadhiliwa na Serikali ya Japan kupitia Wakala wa mambo ya Ujenzi(JICA) na unatarajiwa kuanza mapema mwakani, hii ikiwa ni juhudi za Serikali katika kuboresha miundombinu hasa ya barabara kwa kuzifanya barabara nyingi nchini kuwa katika kiwango cha lami.

Chanzo:
Michuzi
 

Attachments

  • uj1.jpg
    uj1.jpg
    26.4 KB · Views: 1,740
Hio mikopo iwe ya kujenga Njia sita Kutoka Arusha mpaka Holili sio kujenga uchochoro kama wa Arusha - Mnjingu, kama mkopo hautoshi kujenga njia sita acheni ni kututia kwenye madeni bure, msongamano wa magari kwa sasa unaanzia Arusha mpaka njia panda Moshi. Toeni ufafanuzi kwanza kabla ya kuchukua mikopo, na mpaka wananchi wakubali ndio mchukue kwani wao ndio wanaolipa.
 
Hio mikopo iwe ya kujenga Njia sita Kutoka Arusha mpaka Holili sio kujenga uchochoro kama wa Arusha - Mnjingu, kama mkopo hautoshi kujenga njia sita acheni ni kututia kwenye madeni bure, msongamano wa magari kwa sasa unaanzia Arusha mpaka njia panda Moshi. Toeni ufafanuzi kwanza kabla ya kuchukua mikopo, na mpaka wananchi wakubali ndio mchukue kwani wao ndio wanaolipa.

Tuko pamoja Mkuu sio sita tu,
Inatakiw aiwe Super Highway, na maeneo yenye msongamano kama kuanzia Aruemru mapaka arusha, kiboororni mpaka moshi mjini kuwe njia Nane na kwingine kuwe ndio nia Sita. na bila kusahau njia za wapita kwa miguu, baiskeli na vyombo vingine.
 
Back
Top Bottom