Serikali Yaridhia Uraia wa Nchi Mbili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali Yaridhia Uraia wa Nchi Mbili

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Buchanan, Jul 6, 2010.

 1. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #1
  Jul 6, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  na Rahel Chizoza, Dodoma

  SERIKALI imekubali kuwepo kwa uraia wa nchi mbili kwa Watanzania walioko nje ya nchi na kwamba wasichukuliwe kama wasaliti.
  Kutokana na hatua hiyo, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa iko kwenye mchakato wa kuwasilisha muswada kuhusu uraia wa nchi mbili kwenye kikao cha Baraza la Mawaziri.

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe, alisema juzi bungeni mjini hapa, kuwa anafanya mawasiliano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) ili kupata baraka zao kutokana na suala hilo kuwa la Muungano.

  Akihitimisha hoja ya bajeti ya wizara hiyo, kwa mwaka wa fedha 2010/2011, Waziri Membe alisema siyo dhambi, Watanzania kutafuta riziki nje ya nchi na ni haki yao kubaki na uraia wa Tanzania.

  Alisema wakati umefika kwa Watanzania, kupatiwa haki yao ya msingi kwani licha ya kuwa ni manufaa kwao pia ni manufaa kwa nchi kutokana na fursa ya kuongeza pato la taifa.

  “Tusiwaangalie Watanzania walioko nje ya nchi kama wasaliti, watu hawa ni raia wema lakini walikwenda kutafuta riziki tu ili wachumie juani na kulia kivulini, hivyo tunapowafutia uraia wa ndani hatuwatendei haki,” alisema Waziri Membe.

  Alisema kwa kawaida watu wanaoweza kufutiwa uraia wa nchi zao ni wale wanaoondoka nchini kwa sababu mbalimbali kama vile uhaini au wakimbizi kutokana na vita.

  Alisema kama Tanzania imeweza kutoa uraia kwa wakimbizi 169,000 kutoka Rwanda na Burundi, haiwezi kushindwa kuwabakishia uraia wao wananchi wake wanaokwenda kutafuta nje ya nchi.

  Kuhusiana na suala la wakimbizi kutoka nchi jirani na kuingia nchini, Waziri Membe alisema Tanzania imechoka kupokea wakimbizi na kuonya kuwa wakimbizi wowote watakaoingia nchini hivi sasa kutoka Burundi, watakamatwa na kurejeshwa kwenye nchi zao.

  Alisema hivi karibuni nchi ya Burundi, ilifanya uchaguzi ambapo vyama 12 vilivyosusia uchaguzi na kupatikana kwa taarifa kuwa baadhi ya viongozi wa nchi hizo wameingia msituni.

  “Tanzania siyo kichaka cha kuficha watu wahalifu, kiongozi yeyote wa chama kilichosusia uchaguzi atakayekimbilia nchini, atakamatwa na kurejeshwa kwao,” alisema Waziri Membe.


  Source: Tanzania Daima.
   
 2. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #2
  Jul 6, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160


  Hivyo suala la Uraia si lipo chini ya mambo ya ndani sasa foreign wanakujaje hapa? Isijekuwa changa la macho hili. Buchanan tusaidiane kwenye hili
   
 3. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #3
  Jul 6, 2010
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,749
  Likes Received: 545
  Trophy Points: 280

  ni uraia wa nchi mbili kwa watu walioko nje ya nchi tu.Hivyo wizara ya mambo ya nje lazima ihusike.
   
 4. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #4
  Jul 6, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  wow, basi na mimi ngoja nichukua uraia wa canada na Ireland....hapo vipi! na katu sitaukana utz, sitakubali kuwa mkimbizi wala mgeni kwenye ardhi Mungu aliyonileta.
   
 5. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #5
  Jul 6, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  I cannot understand the minister sheria ya immigration iko chini ya Home affairs na sheria ya Uraia citizenship Act nayo iko chini ya Home Affairs sasa kusema watatunga sheria mpya itakayotungwa na foreign affairs haileti sense. Mimi naona kifungu cha saba cha sheria ya Uraia kikibadilishwa itaserve purpose kuliko kufanya mabadiliko.

  Hebu tuangalie hili katika mtazamo huu,
   
 6. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #6
  Jul 6, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Immigration act ina deal na watu wa nje wanaokuja Tanzania na watanzania wanaoenda nje Citizenship inaeleza nani ni raia na haki zao. Hizi zote ziko home affairs, Kwa nini dual citizenship yenyewe iwe chini ya Foreign Affairs, liangalie mara mbili halafu angalia kazi za mawaziri katika instrument za uteuzi. Hili ni suala la uraia per se sio la mambo ya nje, aidha kuna kumislead watu au cheap popularity
   
Loading...