Serikali yapokea maombi 594,300 ya waombaji wa kazi katika utumishi wa umma kuanzia Desemba 2015-Desemba 2018.

Trust None

JF-Expert Member
Feb 12, 2018
1,260
4,415
Hii ni habari ya Desemba 2018. Lengo ni kulinganisha na taarifa ya nafasi 4,500 za ualimu zinazogombewa na jumla ya wahitimu 91,000.

Tatizo la ajira katika awamu hii ni kubwa mno. kwa kipindi hicho, walioajiriwa ni Chini ya 71,000 sawa na asilimia 11 (11%) ya waombaji wote 594,300. Je, ni wangapi wapo mtaani mpaka leo?

Soma zaidi

Turudi kwenye nafasi 4,500 za ualimu zilizotangazwa hivi karibuni ambazo zinagombewa na waombaji takribani 91,000. Wakiajiriwa hao 4,500 itakuwa sawa na asilimia 5 (5%) ya waombaji wote. Kwa hali hii hali ikoje huko mtaani. Ni wangapi hawakuomba? Huenda wengine waliacha kutokana na nafasi kuwa kiduchu.

Ajira za mkupuo zilikoma tarehe 1 mei, 2015 na baada ya hapo zimekuwa za kuomba. Kwa hali hii tunaelekea wapi?
...MTANIKUMBUKA (ni kauli ya kiongozi mmoja wakati anaaga)

Kujiajiri ni wazo zuri, lakini tujiulize kwanza ni kozi gani ulisoma ili ujiajiri? Kozi za kucheza na madesa, slides na vitini ni ndoto kujiajiri.

Watawala mliangalie hili, japokuwa tatizo la ajira haliwezi kuisha ila litapungua na kupunguza makali ya maisha kwa wananchi.
 
Unajua ,ukiwa ni mzee wa kulimbikiza madeni.,, akili haitojiongeza namna gan uongeze mapato ili ulipie maden yako.

Mwisho hautakaa kamwe ulipe maden hayo.


'A bad peace is better than a good quarrel '
 
Serikali ianzishe "Willing Retirement" - kwamba hata ukifanya kazi miaka 10 kisha ukajisikia kustaafu basi ustaafu.
Mnaoshadidia vijana kuajiriwa Serikalini mnawachonganisha na Serikali yao - duniani kote ni nchi gani imetoa ajira kwa vijana asilimia 100?

Jitambuweni!
 
Serikali ianzishe "Willing Retirement" - kwamba hata ukifanya kazi miaka 10 kisha ukajisikia kustaafu basi ustaafu.
Mnaoshadidia vijana kuajiriwa Serikalini mnawachonganisha na Serikali yao - duniani kote ni nchi gani imetoa ajira kwa vijana asilimia 100?

Jitambuweni!

..kwenye nchi za wenzetu sekta binafsi ndiyo muajiri mkuu.

..serekali inatakiwa kuweka mazingira ambayo yatawezesha SEKTA BINAFSI ku create ajira.

..rate of un-employment hapa Tanzania ni kubwa mno. It is unsustainable na ni hatari kwa usalama wa taifa letu.

..pia hakuna nchi ambayo imeendelea huku wananchi walio wengi wakiwa " wamejiajiri " au wanafanya kazi ktk sekta zisizo rasmi.

..kwa hiyo serekali na CCM wakiri kwamba wameshindwa na siyo kuwasakama vijana wasio na kazi wajiajiri wenyewe.

Cc chige, Nguruvi3
 
Back
Top Bottom