Hapo zamani za kale uchawi ulihusishwa zaidi na watu wanaishi vijijini. Lakini siku hizi kama alivyoandika mwandishi mmoja
Uchawi kuchangamkiwa na wa mjini ni hatari zaidi, pamoja na kuwa tayari ulikuwa hatari hata huko vijijini.
Anaendelea kusema kuwa "Uchaguzi uliopita, tulisoma kwenye gazeti moja na kuonyeshwa picha ya mtu aliyekwenda kujiweka sawa kwa mganga wa kienyeji; huyu ni moja kati ya wasomi wengi ambao hatuonyeshwi. Nasema msomi kwa sababu naamini watu wanaogombea nafasi za uongozi katika nchi hii wamepita shule, [though siyo wote]
Kila siku tunasikia mijini habari za uchawi. Uchawi umeongezeka mijini kiasi kwamba hata waganga wa kienyeji wenye kujishirikisha na mambo ya ushirikina nao wamehamia mjini kuwasaidia hao wanaotarajia kutajirika na kupata vyeo kwa ushirikina.
Hapa siwazungumzii wale wenye dawa za kutibu ugonjwa huu na ule; sina ugonvi na hao. Inashangaza sana kwani tuko karne ya 21; karne ya sayansi na teknolojia ambayo binadamu wameweza kuvumbua mengi ambayo huko nyuma yalikosa maelezo na yakahusishwa na nguvu za giza......
Kimbilio la kuondoa imani hii potofu wangekuwa ni watumishi wa Mungu. Lakini baadhi yao nao wamepata ugonjwa huo huo kama wa waganga wa kienyeji wa kuwatia watu hofu kuhusu mambo ya uchawi. Wakati waganga wa kienyeji wanatoa picha ya uchawi kuwaletea maendeleo wale wanaouamini, baadhi ya watumishi wa sasa wanatoa picha ya kama vile ulimwengu huu sasa unamilikiwa na wachawi na kila kinachoendelea kinaendeshwa na wachawi.
Ukitaka kielelezo sikiliza mahubiri yao au njoo nikuoneshe kanisa ambalo limeandikwa kwa maandishi makubwa kabisa "
KIBOKO CHA WACHAWI" (cc
Kaunga).
Uchawi kuchangamkiwa na wa mjini ni hatari zaidi - Kolamu - mwananchi.co.tz