Serikali yapiga marufuku wapiga ramli nchini!

Serikali yapiga marufuku wapiga ramli nchini!

Vigogo wamepata hofu baada ya utabiri kuwa kuna mgombea urais atafia jukwaan wakat wa kampeni.

Wala hawana uchungu wowote na albino.

Lakini kupga marufuku hawa waganga itasaidia kupunguza mikosi kwenye nchi yetu.
 
Hivi professa Maji Marefu sio mpiga ramli mkuu?@Nyani Ngabu na EMT tuelimishane hapa.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Sana MziziMkavu usimlaumu Sana hapo ndo kimo cha ufahamu na uelewa wake kilipoishia .....

Anaamini kuisha kwa ramli ndio mwisho Wa mauwaji hajishughulishi kuwaza vipi wanaouliwa kwa chuki tu au imani za kipuuzi (wengine huchukulia maalbino Kama laana na mikosi ktk koo zao) hawa je?

Hizi ndo think tank zetu miaka 53 ya Uhuru tupo Kama watumwa.....
Huyu Hapa Waziri wa Mambo ya ndani anapiga Marufuku Eti kupiga Ramli ndio kutasaidia walemavu wa ngozi Albino kuto kuuliwa msome hapo chini.

Tanzania kupambana na ukatili wa Albino

Mshirikishe mwenzako
150113151928_albino_640x360_bbc_nocredit.jpg


Wafanyakazi wa BBC wakiwa kazini,Tulanana Bohela wa Focus on Africa na Halima Nyanza wa BBC Swahili wakimhoji waziri wa mambo ya ndani Mathias Chikawe.
Serikali ya Tanzania imeunda kikosi maalumu kwa ajili ya kupambana na vitendo vya ukatili wanaofanyiwa watu wenye ulemavu wa ngozi –Albino- na huku ikitangaza pia kupiga marufuku kuanzia leo wapiga ramli wote ambao wanaelezwa kuchangia mauaji ya watu hao.

Waziri wa Mambo ya Ndani Mathias Chikawe Ameitaja mikoa inayotarajiwa kuanza kwa operesheni maalum ya kupambana na vitendo vya ukatili dhidi ya walemavu katika juhudi za kukomesha kabisa matukio hayo, ambayo yameelezwa kuanza kuibuka tena.


Mikoa hiyo ni Mwanza, Simiyu, Geita, Tabora na Shinyanga.Operesheni hiyo pia inatarajiwa kuendelea katika mikoa mingine.Aidha amesema operesheni hiyo itaanza baada ya wiki mbili kwa ushirikiano wa polisi na wawakilishi kutopka chama cha watu wenye ulemavu Tanzania.


Kazi ya kikosi hicho ni pamoja na kupitia pia kesi zote zilizowahi kufikishwa mahakamani kuhusiana na vitendo hivyo.kizungumzia kuhusiana na kupigwa marufuku kwa wapiga ramli nchi nzima, Waziri Chikawe amesema jeshi la polisi litaandaa operesheni maalum kuwatafuta na kuwashtaki.


Amesema wapiga ramli hao wanajulikana na wananchi wanaomba kusaidia kuwatambua.

Aidha amewataka wananchi kutoa ushirikiano katika kufanikisha zoezi hilo zima, ikiwemo pia kuyataka madhehebu ya dini mbalimbali na mashirika ya kijamii kutoa elimu juu ya jambo hilo.Sababu kubwa iliyotajwa inayosababisha watu kutafuta viungo hivyo vya binadamu inaelezwa kuwa ni kupata utajiri.Chanzo.
http://www.bbc.co.uk/…/2…/01/150113_albino_tanzaniataskforce
 
Wizara ya mambo ya ndani imepiga marufuku upigaji ramli ili kukabiliana na mauaji ya albino nchini.

Source:TBC Taifa

cc: MziziMkavu

Ramli hazipigwi kama maandamano ya Chadema. Kama wameshindwa kuwadhibiti panya road wanaoonekana na wapo Dar pekee,ni vigumu kuwadhibiti wapiga Ramli ambao hawaigi hadharani na wameenea nchi nzima.
 
Last edited by a moderator:
Mikoa inayoongoza kwa upigaji ramli:

Tanga

Pwani

Mwanza

Simiyu

Shinyanga

Rukwa

Nadhani makamanda wa polisi wa mikoa hii wangeanza operesheni kabambe ya kuvunja vibanda vya ramli.
 
Ramli hazipigwi kama maandamano ya Chadema. Kama wameshindwa kuwadhibiti panya road wanaoonekana na wapo Dar pekee,ni vigumu kuwadhibiti wapiga Ramli ambao hawaigi hadharani na wameenea nchi nzima.

Wakiwa na dhamira na weledi watafanikiwa.
kwa mfano ukienda kwa msisi Tanga huwezi kuwakosa wapiga ramli chini ya 50 hivi.
 
Hata waganga na watu wote wanaotabiri wapigwe marufuku

kwahyo wakipigwa marufuku waganga ndo mauaji ya albino yataisha? mbona hata madawa ya kulevya yamepigwa marufuku ila ma-drug dealer wanatinga hadi ikulu na rais anayo majina, sasa sijui atamkabidhi majina rais ajaye!
 
Back
Top Bottom