Serikali yapiga marufuku Walimu kuwarekodi wanafunzi na kusambaza video kwenye Mitandao ya Kijamii

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
Waziri wa Elimu, Profesa Mkenda akizungumza na Walimu na Wadau wa elimu amesema kuwa ''Tunakemea walimu wote wanaowarekodi wanafunzi wanaokosea na kusambaza clips kwenye mitandao ya kijamii, wanafunzi wana faragha zao wanapokosea hawapaswi kurekodiwa na kusambazwa''

Elimu.jpg

Picha: Waziri wa Elimu Profesa Mkenda (Aliyesimama)

 
Last edited:
Nasubiri siku mwalimu amrekodi mwanangu tugawane majengo ya serikali.
 
Lakini mengine yamesaidia kufunua uovu mwingi na mengine yamesaidia kuonesha dunia madhila wanayopitia baadhi ya watoto
 
Lakini mengine yamesaidia kufunua uovu mwingi na mengine yamesaidia kuonesha dunia madhila wanayopitia baadhi ya watoto
Ni kweli kabisa, lakini mengi yanasambazwa ni ya kudhalilisha na kutweza utu wa mtoto. Mfano kuna ile moja kati ya nyingi ambayo Mwalimu alirekodi wanafunzi aliokuwa/waliokuwa wanawahoji kuhusu kuingiliana kinyume na maumbile. Watoto wenyewe shule ya msingi, ile clip inaumiza sana.
 
kuishi nje ya nchi tunapitwa sana saa hii ndalichako kapumzika kumbe
 
Back
Top Bottom