Serikali yanywea | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yanywea

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mpita Njia, Jun 17, 2009.

 1. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #1
  Jun 17, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,014
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Pinda katangaza hivi punde mjini Dodoma kuwa baada ya kelele nyingi za wananchi, viongozi wa dini na wabunge, serikali imeamua kugeuza uamuzi wake wa kufuta misamaha ya kodi kwa taasisi za dini. Amesema Mkulo atatangaza kesho jinsi serikali itakavyopfidia pengo la fedha linalotokana na uamuzi huo
   
 2. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #2
  Jun 17, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,623
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hiyo ni weakness kubwa sana, mpaka sasa sijaona sababu kwa nini wasitozwe kodi kwenye non-spiritial services.

  Nitawaunga mkono tu kama watapunguza matumizi ya serikali, kutangaza kuuza VX zote... na waziri apewe SUV [RAV 4, Honda, Suzuki Vitara]!!!
   
 3. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #3
  Jun 17, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,160
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  MN,

  Huu ni ubabaishaji wa hali ya juu kwa serikali yetu.....inamaana hawakufanya utafiti wa kutosha kabla ya kufanya maamuzi ya awali ndugu zangu?

  To me it was very right decision ya kuondoa ile misamaha ya kodi hasa ukizingatia these days the so called churches and other religious organs are mushrooming only to claim the benefits of tax exemptions granted to them for their personal benefits!

  Kwa hiyo hiyo misamaha ilikuwa sahihi kabisa kuiondoa though kuna ukweli kwamba kuna baadhi ya taasisi ambazo zinaitumia misamaha hiyo kwa malengo yaliyokusudiwa!
   
 4. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #4
  Jun 17, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,160
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Tupo pamoja on this kasheshe......sio hilo tu zile 34.6bil zilizotengwa kwaajili ya Travel ya government officials wazipunguze ndizo zifidie hiyo kodi iliyopungua kwa maamuzi yao ya kukurupuka!
   
 5. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #5
  Jun 17, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Ndiyo maana hatuendelei. Viongozi wetu hawana msimamo. Kama jambo walikaa na kulijadili kwa kina sioni wana shindwaje kutetea hoja zao. Hii inaonyesha kuwa serikali yetu siyo secular kama tunavyo dhani na taasisi za dini zina nguvu kuliko tunavyo dhani au serikali yetu ina kupuruka kuamua mambo ndiyo maana waki banwa wana shindwa tetea maamuzi yao.
   
 6. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #6
  Jun 17, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,623
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Next Level,

  Hata ikiwa wanatumia vizuri, lakini wajameni taasisi za dini kazi yao ni kueneza neno la Mungu!

  Kazi zao sio ku-run government parallel to government ya kaisari, haya mambo ya shule na hospital za taasisi za dini in reality ni services za kutolewa na serikali ikiruhusiwa kupokea kodi.
   
 7. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #7
  Jun 17, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,096
  Likes Received: 247
  Trophy Points: 160
  Uamuzi mzuri sana huu maana mantiki ya misamaha hii ililenga zaidi kuudidimiza ukristo. Angalia mifano aliyoitoa Mkulo inahusu Makanisa tu. Pia hakukuwa na mantiki kuwaadhibu Wakristo wote kwa makosa ya wachache. Sheria ziko wazi. Atakayekiuka ndiye aadhibiwe. Kwa mfano dhehebu au shirika la dini lilitakiwa liagize magari kwa ajili ya shughuli za kiroho halafu lenyewe likayaingiza kwa ajili ya biashara. Kinachofuata ni kulichukulia hatua shirika au dhehebu husika. Sio kuyachukulia na madhehebu mengine ambayo hayajakiuka taratibu na kuyafutia misamaha kwa kosa la wachache! Ile kauli ya Mkulo kwamba "uamuzi huu wa kufuta baadhi ya misamaha haukufanywa kwa sababu yeye na Rais Kikwete ni waislamu bali uamuzi ulifanywa wakati wakristo ni wengi waliohusika na uamuzi huo". Hivi hapa anataka kueleza nini? Wakristo walio wengi wanaangalia kwa makini mwenendo wa Serikali hii ya Awamu ya Nne!
   
 8. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #8
  Jun 17, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,160
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Kasheshe,

  Nikisemacho mimi ni kuwa laiti misamaha ile ingetumika whole and exclusively kwa manufaa ya waumini wa dini.....hili halingeleta shida sana! Tatizo linakuja pale tu ambapo misamaha inatumika na wajanja kukwepa kodi....this is very bad!

  Kama unazungumzia huduma kama shule, afya etc.....hii mbona hata ukianzisaha ya kwako zipo exempted? hakuna shule yoyote au hospital yoyote ambayo vifaa vyake vinapigwa VAT mkuu.....so kinachozungumzwa hapa ni other supplies!
   
 9. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #9
  Jun 17, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,623
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kaka kama unafikiria hivyo then una tatizo! Ila in any case huu ni uamuzi uliofanyika kwa sababu mwaka unakuja ni uchaguzi, imesogezwa mbele tu... serikali yoyote huko mbele especially angalia budget ya 2011/12... hiyo misamaha itakuwa imeondolewa.
   
 10. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #10
  Jun 17, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,160
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Naungana na Kasheshe....na for your information mimi binafsi ni Mkristo tena ex Seminarian...lakini sikubaliani kabisa na hoja yako!

  Hoja za namna hii haziwezi kutupeleka mbali kabisa!
   
 11. MwanaHaki

  MwanaHaki JF-Expert Member

  #11
  Jun 17, 2009
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,348
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  \

  NextLevel

  Ulisikiliza alichokisema leo Bungeni Mheshimiwa Lucy Mayenga, Viti Maalum (CCM)? Amesema watendaji wengi serikalini ni wazembe, wasio na ubunifu, wasiojua kazi na wenye kujawa na ubinafsi kiasi kwamba utendaji wao umekuwa kero. Amesema Serikali haipaswi kuwavumilia watu kama hawa ambao kila mwaka "wanashughulikia" kupata ufumbuzi wa matatizo yale yale! Amesema sasa umefika wakati wa kuwaondoa watu hao, wasivumiliwe kwa kuwa wamekuwa na utendaji wa muda mrefu serikalini! They have to go! Yaani, sasa, Serikali inapaswa kuendeshwa kama PRIVATE SECTOR, kwani, hata mimi ninamuunga mkono Mhe. Mayenga! Nani aliyesema kwamba Serikalini ndio kimbilio la wazembe wote waliofukuzwa kazi kwenye PRIVATE SECTOR?

  Kukujibu swali lako hapo juu, NDIO, hakuna utafiti wa kina uliofanywa kabla ya Serikali kufikia uamuzi wa kufuta misamaha ya kodi kwa NGOs na Taasisi za Kidini! Hakuna!

  Wamesema kwamba wamegundua matukio ya wizi, yaani, watu walioingiza vitu kadhaa kwa "gia" ya NGO na Taasisi za Kidini, lakini vitu hivyo vikaishia mitaani, kwenye maduka, kama bidhaa za kawaida. Sukari, nguo, mabati, na kadhalika!

  Sasa, kama alivyosema Dr. Slaa (nadhani leo Bungeni), kwa nini basi Serikali isiwakamate na kuwashughulikia hao Makasisi, Mapadre, Maimamu na Masheikh waliolihujumu taifa letu? Si kuna ushahidi? Huo ni uhalifu tu kama ulivyo uhalifu mwingine.

  Serikali "haikunywea", kumekuwa na UZEMBE ulioanzia kwa Mshauri Mkuu wa Waziri wa Uchumi katika suala hili, yaani, Mama Mary Nagu, ambako muswada huo wa kuondoa misamaha ya kodi ulikotokea, Mkullo yeye akaingia KICHWA KICHWA, fumba na kufumbua, bila hata a DUE DILLIGENCE (hivi hiki kitu kitazungumziwa mpaka lini?), wameleta muswada bungeni usio na kichwa, utumbo wala miguu! Kha!

  ./Mwana wa Haki
   
 12. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #12
  Jun 17, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,160
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Mwanahaki you said it all nimeandika kuonyesha msisitizo tu....but I conquer with you comments 100%

  Cheers
   
 13. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #13
  Jun 17, 2009
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,049
  Likes Received: 1,212
  Trophy Points: 280
  Pengo amewatisha nini??
  Baada ya kusimama yeye live nakusema lazima afe na mtu ngoma imekuwa hachezeki tena nini? kwi kwi kwi kwi
   
 14. K

  KipimaPembe JF-Expert Member

  #14
  Jun 17, 2009
  Joined: Aug 5, 2007
  Messages: 1,287
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Kusema kweli mimi bado naunga mkono kuwa dini lazima zitozwe kodi kwa kila kitu. Mi sielewi kwa nini hata vifaa vya ibada visitozwe kodi. Wenye dini zao wanaoviingiza vitu hivyo kwa nini wasilipie kodi?

  Kusema kweli suala hili ni kweli lilishachukua dimension ya kidini. Nchi yetu watu wengi we are still very low. Ilikuwa rahisi sana kusema kodi hii imeyalenga madhehebu ya Kikristo, hasa yale makubwa kama wakatoliki ambao ni kama ki-sub government ndani ya serikali. Suala ni kuwa makanisa makanisa sasa hivi yame jiimarisha au kujijenga zaidi kwa kutoa social services na hii ni failure kubwa ya serikali. Ni kweli kuwa haya makanisa yakiondoa social service zao maeneo mengi yataumia.

  Tatizo kubwa ndo hilo la kufanya mambo kwa kukurupuka. Decision kubwa kama hiyo ilitakiwa iwe backed na data za kutosha. Hata hivyo nilianza hata mimi kutilia shaka uamzi huo baada ya kugundua kuwa kodi ambayo inasamehewa kupitia sehemu hii ya dini ni percentage ndogo mno ya misamaha yote ya kodi.

  Sehemu kubwa au lion's share ya misamaha ya kodi inakwenda kwa makampuni ya madini ambao ni huge profit makers ambao logic kwa kweli ya kuwapa misamaha mikubwa kiwango hicho haipo. Baada ya kuona hilo nikapunguza hata mimi munkari kuhusu taasisi za kidini kutosamehewa. Yaani unamsamehe Barrick Gold anayetoa divident kibao kwa share holders wake kule Canada halafu unamtoza kodi Method kilaini anayeendesha msimbazi center na Bugando referal hospital!! Hii haiingii akilini.

  Ni rahisi kufikiria kuwa serikali ilizitarget hizi taasisi za kidini ili kuzidhoofisha tu na wala si kuongeza pato la serikali kama tunavyoambiwa. Yaani badala ya kugusa asilimia 70 ya misamaha ya kodi, wanakimbilia asilimia kama 5 tu ya misamaha yote. Impact yake kwenye leakage ya government revenue ni ndogo mno. Lakini vile vile impact yake kwa walala hoi wa kawaida ingekuwa kubwa.

  Nadhani kufanya mambo kwa kukurupuka ni kawaida ya serikali yetu. Hapa unaweza sema ushauri ulitolewa kwenye vijiwe vya kahawa tuuu.
   
 15. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #15
  Jun 17, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,014
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Inavyoelekea serikali haikupima upepa maana hii ni kigeugeu kweli. lakini nadhani pia wameangfalia na Oktoba 2010 na hii elimu ya uraia inayotolewa na wakatoliki, iwapo wataamua kuunganisha na kampeni zao, hali inaweza kuwa mbaya kwa muungwana mwakani
   
 16. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #16
  Jun 17, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,650
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Labda serikali imeogopa lile tamko la kanisa la kuwafundisha waumini wake jinsi ya kupiga kura, na imeonekana dhairi kuwa may be sisiem ingekosa kula kwa kunyimwa kura, labda wangepewa Chadema au CUF.
   
 17. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #17
  Jun 17, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,096
  Likes Received: 247
  Trophy Points: 160
  Kama kuna wenye matatizo ni wenye kuadhibu na wasiokuwemo! Mkulo alitoa na mifano kabisa kuhusu wanaotumia misamaha vibaya. Otherwise hiyo mifano aliyoitoa ina maana gani? Mkulo hajaeleweka kabisa kuhusu hili. Afadhali tu ameshtukia mapema.
   
 18. K

  KipimaPembe JF-Expert Member

  #18
  Jun 17, 2009
  Joined: Aug 5, 2007
  Messages: 1,287
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Kwa kweli msimamo wangu unabaki kuwa dini ni kitu personal ambacho hakiwahusu watu wengine ambao si members wa dini hiyo. Kuendelea kutoa misamaha ya kodi kwa dini ni kutoa preference kwa wenye dini. Wasio na dini nao wanavyo vitu personal wanavyovipenda lakini havisamehewi kodi. Dini ni personal sawa na unywaji wa pombe au uvutaji wa sigara. Wenye dini wanastahili kulipia vifaa vyao vya ibada kama wanavyolipa sadaka na zaka makanisani bila kuhoji matumizi yake.

  Hata hivyo, logic ya kumsamehe kodi Barick gold na kumtoza kodi mwenye kanisa ndo inayofanya ni withdral support yangu kwa suala hilo.

  Mikataba ya madini iliyosainiwa iko juu ya sheria zote zitakazotungwa mpaka muda wa mikataba ile utakapoisha. Nilishangaa nilipogundua kuwa misamaha iliyofutwa kwenye madini ni kwa makampuni ambayo hayajaingia nchini yaani makampuni ambayo hayapo. Yale yaliyopo misamaha kama kawaida.

  Sasa ikiwa hawa wanaozalisha faida kubwa huko kwao wanaachiwa halafu tunatozana sisi hata kwenye vifaa vya ibada, huu ungekuwa utaahira. Kwanza kodi yenyewe ingekuwa only symbolic.

  Kwa hiyo aliyeileta kodi hiyo aliazimia kuzikomoa taasisi za kidini ambazo anadhani hazimhusu.
   
 19. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #19
  Jun 17, 2009
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,049
  Likes Received: 1,212
  Trophy Points: 280
  Naona hoja yako dhaifu kwani watu wanaohudumiwa mfano pale bugando ni wamission tu ??
  Kweli wanadini wanahitaji kulipa kodi lakini kwa hoja hii bado dhaifu.
   
 20. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #20
  Jun 17, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,096
  Likes Received: 247
  Trophy Points: 160
  Unajua kinachogomba hapa ni sababu ya kufuta hiyo misamaha. Ni kwa sababu kuna baadhi wanaitumia vibaya na wanaoitumia vibaya wanawafahamu! Hivi wasio na misamaha ya kodi huwa hawakwepi kodi? Mkulo Dont victimize people in vain.
   
Loading...