Serikali Yanunua Magari 727 ya Kubeba Wagonjwa

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Wizara ya Afya imenunua magari 727 ya kubeba wagonjwa yatakayotolew a kwa kila halmashauri na hospitali za mikoa. Naibu Waziri, Dk Godwin Mollel amesema kila halmashauri inatarajiwa kupata magari mawili na hospitali ya mkoa itapata moja.

Dk Mollel alisema hayo alipofanya ziara kukagua utoaji huduma na mandeleo ya ujenzi wa miundombinu na upatikanaji wa vifaa tiba katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma.

"Tumenunua ambulance (magari ya kubeba wagon-jwa) 727 na tayari zimeanza kuingia na tumekubaliana angalau zifike ambulance 200, kuna uwezekano wa kila halmashauri kupata mbili na kila hospitali ya mkoa kupata, hivyo kuna uwezekano wa mkoa wako (Kigoma) kupata ambulance 17 zitakazosaidia kupiga hatua katika huduma za afya," alisema.
 
Wameyanunua kwa bei gani ili nasi Wananchi tujiridhishe kuwa kodi yetu haijapigwa?

Toyota Landcruiser 70 2021 Prices
Prices for the Toyota Landcruiser 70 2021 start from $35,000 for the hardtop STD AL-wheel 3DR 4x4 to $47,150 for the top of the lineup hardtop DLX DSL 5DR 4x4.

Samia ameturuhisu tuhoji bila kuwindwa kama Digidigi.
 
Shubaa miti !! huo ni upotevu na ubadhirifu wa pesa na rasilimali za walipa Kodi, badala ya kuboresha huduma za afya unakwenda kununua magari wakati vituo vya huko pembezoni hata dawa za msingi hakuna.
 
Wameyanunua kwa bei gani ili nasi Wananchi tujiridhishe kiwa kodi yetu haijapigwa?

Toyota Landcruiser 70 2021 Prices
Prices for the Toyota Landcruiser 70 2021 start from $35,000 for the hardtop STD AL-wheel 3DR 4x4 to $47,150 for the top of the lineup hardtop DLX DSL 5DR 4x4.

Samia ameturuhisu tuhoji bila kuwindwa kama Digidigi.
Hapo kuna ufisadi pesa zimepigwa haswa
 
Wizara ya Afya imenunua magari 727 ya kubeba wagonjwa yatakayotolew a kwa kila halmashauri na hospitali za mikoa. Naibu Waziri, Dk Godwin Mollel amesema kila halmashauri inatarajiwa kupata magari mawili na hospitali ya mkoa itapata moja...
Haya yataenda kuwabeba " Maafisa Hospitali" badala ya kubeba wagonjwa. Tumekuwa tukiona haya yakitendeka miaka yote.
 
Changamoto kubwa manunuzi yetu yamegubikwa na 10%,

Hapo watu wamepiga pesa balaa
 
Wizara ya Afya imenunua magari 727 ya kubeba wagonjwa yatakayotolew a kwa kila halmashauri na hospitali za mikoa. Naibu Waziri, Dk Godwin Mollel amesema kila halmashauri inatarajiwa kupata magari mawili na hospitali ya mkoa itapata moja.

Dk Mollel alisema hayo alipofanya ziara kukagua utoaji huduma na mandeleo ya ujenzi wa miundombinu na upatikanaji wa vifaa tiba katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma.

"Tumenunua ambulance (magari ya kubeba wagon-jwa) 727 na tayari zimeanza kuingia na tumekubaliana angalau zifike ambulance 200, kuna uwezekano wa kila halmashauri kupata mbili na kila hospitali ya mkoa kupata, hivyo kuna uwezekano wa mkoa wako (Kigoma) kupata ambulance 17 zitakazosaidia kupiga hatua katika huduma za afya," alisema.
Wagalatia watachukia Basi
 
Back
Top Bottom