Serikali yalifunga daraja la Mwanza - Musoma kwa siku 10

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
1,801
2,000
Daraja la Mto Simuyu lililoko wilayani Magu katika barabara kuu ya Mwanza-Musoma limeharibika, hivyo serikali kulifunga kwa siku 10 ili kupisha matengenezo makubwa.

Daraja hilo limeharibika kutokana na uchakavu uliosababisha vyuma kukatika.

Akiwasilisha taarifa ya ufungwaji wa daraja hilo Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Marwa Rubirya, alisema ameifunga barabara hiyo kuanzia jana hadi Machi 18, mwaka huu ili kupisha matengenezo makubwa ya daraja.

Mhandisi Rubirya aliongeza kuwa wameamua kufanya matengenezo ya haraka ili kujiepusha na athari zitakazoweza kujitokeza kwa sababu kuchelewa kwa ujenzi huo unaweza kuwasababishia athari watumiaji wa barabara hiyo.

Alisema kuwa barabara hiyo imefungwa ili kupisha matengenezo kuanzia saa tatu usiku hadi saa 11 asubuhi, huku akiomba ushirikiano wa Jeshi la Polisi katika kutekeleza kazi hiyo.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa daraja hilo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, alisema kutokana na changamoto hiyo njia zitafungwa kwa muda uliopangwa kwa siku kumi ili kupisha matengenezo hayo.

Alisema serikali ina mpango wa kujenga daraja jipya, hivyo hatua zinazofanyika sasa ni za muda mfupi, na kuwataka wananchi kuwa wavumilivu ili waboreshewe njia itakayowanufaisha na kuendeleza ujenzi wa taifa.

“Hali halisi ilivyo na nyie mmeiona… ninachowaomba muwe wavumilivu, ujenzi ufanyike ili kuepusha madhara makubwa ya baadaye," alisema Mongella.

Lusia Isack, mkazi wa Magu akizungumzia adha hiyo, alisema wanakuwa wa hofu kila wanapopita kwenye daraja hilo hasa wanapofika katikati, hivyo wanaishukuru serikali kwa kuliona hilo na kutatua changamoto hiyo kabla haijaleta maafa.

Aliongeza kuwa uchakavu wa miundombinu pamoja na ufinyu wa daraja hilo umekua ukisababisha msongamano mkubwa wa magari, ambao umekuwa ukiwapotezea muda wa kufanya shughuli za uzalishaji mali, hivyo aliiomba serikali kuharakisha marekebisho ya daraja hilo.

"Hili daraja ni bovu sana, hata ukiwa umebebwa kwenye baiskeli ukifika katikati daraja linaanza kucheza… sasa ukiwa kwenye gari unawaza sijui nitapita salama kwa sababu likidondoka tu sidhani kama kuna mtu atakayepona,” alisema na kuongeza:

“Kinachobaki ni kuomba Mungu wakitutengenezea, watakuwa wametusaidia sana."

Daraja hili lililojengwa mwaka 1962 katika eneo la Kisaba Kata ya Lubugu linakabiliwa na uchakavu wa miundombinu ambapo kwa kuonyesha nyufa baada ya vyuma vilivyokuwa vinalishikilia kukatika.

IPP MEDIA
 
Bill

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
5,729
2,000
Kwahiyo kuanzia saa 12 asubuhi mpaka saa 2.59 usiku magari yataruhusiwa kupita
 
lukwila

Member
Dec 3, 2017
45
125

Kisaba=kisamba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Elungata

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
34,867
2,000
Hili daraja,hivi liliachwa na mjerumani au mreno?.
Maana limekongoroka Hadi Basi...
 
Shoctopus

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
2,539

Daraja kujengwa muda wa siku kumi kwa hawa engineers wa bongoland!
Wamefanya lini hydrology surveys na engineering designs? And by whom?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Top Bottom