barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,866
Serikali ya Mkoa wa Manyara imelifunga bwawa la Nyumba ya Mungu na kuzuia shughuli zozote za uvuvi na kiuchumi ndani ya bwawa hilo kuanzia Julai 01 2016.Hatua hiyo imetolewa tamko na Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara Ndugu Eliakimu Maswi.
Hatua hiyo imefikiwa kwa kukutanisha wadau wa Mkoa wa Manyara na Mkoa wa Kilimanjaro.Wavuvi zaidi ya 20,000 wanaofanya kazi za uvuvi katika eneo hilo wataathirika na uamuzi huo,huku wafanyabiashara wengine wanaofanya biashara kutegemea wavuvi wa bwawa hilo nao wakiingia katika kizungumkuti cha mdororo wa kiuchumi sababu walitegemea shughuli ya uvuvi na wavuvi kuendesha maisha yao
Katibu Tawala Maswi anasema Serikali imefikia hatua hiyo baada ya wavuvi wa eneo hilo kuendekeza uvuvi haramu wa kutumia nyavu zilizopigwa marufuku na utumiaji wa sumu katika kuvua,Maswi anasema mwaka 1970 Bwawa la Nyumba ya Mungu lilikuwa lizalisha tani 25,000 za samaki lkn kufikia mwaka huu 2016 bwawa hilo linazalisha tani 11 tu.
Maswi ametoa onyo kwa wavuvi hao kuondoka kandokando ya bwawa hilo na kukoma kuvua kuanzia Julai Mosi,huku akiwasisitiza wenyeviti wa Kijiji na Watendaji wao kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama katika kuwabaini watu wote wanaoendesha uvuvi haramu katika bwawa hilo.
Wavuvi wanaofanya shughuli zao katika eneo hilo,wameiambia serikali kuwa uamuzi huo utawaacha katika hali ngumu ya maisha sababu wamekuwa wakitegemea uvuvi kuendesha maisha yao