Serikali yaleta wataalamu kutoka China kudhibiti mitandao ya kijamii kama YouTube, Facebook

Neno "udikteta" nililitaja kwa mara ya kwanza disemba 2015 wakati napinga ada elekezi. Nilionya juu ya nchi kurejeshwa kwenye mfumo wa ujamaa. Mfumo huu ni kandamizi na wa kijinga sana. Wanaoufuata huwa ni asili wawe madikteta na pia wenye mawazo mgando na wanaoongoza bila hekima na upendo kwa watu wao. Hiki ndicho kinachoendelea. ACHA WAISOME NAMBA.
 
Naona hii serikali inazidi kumdhibitishia Nyerere huko aliko kua alifanya makosa kuwafurusha watu weupe,na anaoneshwa kivitendo,serikali ya JPM inawafuata wachina waje huku kwetu watusaidie kudhibiti mitandao ya mawasiliano.Namsihi Magu aipe maelekezo tume ya kuhakiki ubora wa vyuo vikuu kuzuia udahili wa wanachuo katika vyuo vyote vinavyotoa kozi za IT maana hamna namna kuendelea kutoa hizo kozi halafu watu wanadharauliwa na serikali yenyewe,tena waziwazi.
 
Kipindi kile wakati wanazuia watu kuposti picha za uchi Mitandaoni tuliongea sana na kupiga kerere lakini Leo hii watu wanaona mafanikio yake. Kwa iyo ni upepo. Kama ulivyo upepo mwingine ivi. Wazuie Mitandao na waweke sheria ngumu ukihudhi watu unafunguliwa mashtaka tuu, hakuna jinsi kumbukeni hii Mitandao imekuja kwetu imekutana na watu wa kila aina wenye elimu na wasio na elimu. Kwa iyo kwa sheria itasaidia sana
 
Serikali ya Tanzania imelata wataalamu kutoka China kuisaidia kudhibiti mitandao ya kijamii kama Facebook, Instagram, Youtube, WhatsApp na nyingine kama ambavyo China imeweza kuidhibiti mitandao hii nchini mwao, ambapo haipatikani nchini China bali mitandao ya kijamii ya kichina.

Hayo yamesemwa na Naibu waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Edwin Ngonyani alivyokuwa akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari, wadau wa mitandao na wataalamu kutoka China.

Amesema japo sisi hatuwezi kuwa na mitandao yetu ya kijamii na tunatumia mitandao ya kijamii ya Marekani ila wataangalia namna ya kufanya ili mtu anayeandika kwenye mtandao awajibike na anachokiandika maana mitando hii imekuwa ikitumika kuharibu nchi kama ilivyotokea kwenye nchi za Kiarabu

Je, mitandao hii wataidhibitije?



Ila kumfanya mtu asiseme ya moyoni ni kazi. Na coded language je?
 
Kadri siku zinavyosonga mbele, n pamoja na mabadiliko ya teknolojia ndivyo inazidi kuwa vigumu kutawala Africa
 
China kwenyewe watu wanatumia Fb & whatsapp...hawa wazee wanadhani tupo 18's century....labda VPN zisiwepo
 
Back
Top Bottom