Jeuri, dharau, unafiki na uroho wa viongozi wa Tanzania ndiyo itakayoliangamiza Taifa letu. Haiingii akilini watu wanadai kuboreshwa kwa mazingira ya utoaji wa huduma muhimu kama afya na elimu; wanatokea viongozi wachache tena kwa kiburi na jeuri wanasema hakuna fedha ama liwalo na liwe lakini wanakuwa na jeuri ya kusema wanaodai waondoke kwani wana fedha za kutosha kuagiza madaktari wa nje ama kuingia ubia na hospitali binafsi. Hivi kwa uelewa wao finyu wanafikiri hospitali binafsi wanapata wapi madaktari kwa ajili ya shughuli zao.
Nafikiri imefika wakati Watanzania tuoneshe umoja wa hali ya juu kwani kiburi cha hawa viongozi ni matokeo ya kugawanyika kwetu na uhuru walioachiwa katika kukomba rasilimali za Taifa letu. Leo hii tunaambiwa kuwa kuna viongozi wanamiliki mabilioni na matrilioni ya shilingi kwenye akaunti za nje lakini watanzania wanakufa kwa kukosa madawa ama huduma nyingine za msingi kama elimu na maji.
Rais wa nchi anasafiri kiholela na msafara wa watu zaidi ya hamsini pasipo kufikiri hali ya wananchi wake; rais kama huyo atakuwa na huruma kwa wananchi wake kweli?? Gharama kwa safari moja ya rais ingeweza kuboresha huduma ya zahanati ngapi hapa Tanzania.
Hata pale wanapougua wao huwahishwa India na kwingineko kwa ajili ya kupata huduma ya daraja la kwa tena kwa gharama ya fedha za walipa kodi, mtanzania mnyonge atapata wapi huduma kama hiyo kama sio kuishia kwenye miti shamba na kwenye vikombe kama ilivyotokea Samunge huko Loliondo.