Serikali yakata rufaa kupinga hukumu ya Jamal Malinzi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,480
9,241
Serikali imewasilisha nia ya kukata rufaa Mahakama Kuu, kupinga hukumu na adhabu iliyotolewa na Mahakama ya Kisutu, dhidi ya aliyekuwa rais wa zamani wa TFF, Jamal Malinzi na katibu wake, Celestine Mwesigwa

====
UPANDE wa Mashtaka umewasilisha nia ya kukata rufaa Mahakama Kuu, kupinga hukumu na adhabu iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu dhidi ya aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Jamal Malinzi na Katibu wake, Celestine Mwesigwa.

Katika hukumu hiyo, iliyotolewa Desemba 11, 2019, Malinzi alitakiwa kulipa faini ya Sh 500,000 au kwenda jela mwaka mmoja, huku Mwesigwa, akitakiwa kulipa faini ya Sh 1milioni au kwenda jela miaka miwili baada ya Mahakama ya Kisutu kumtia hatiani katika mashtaka mawili, kati ya 20 yaliyokuwa yanamkabili.

Vigogo hao wa TFF walihukumiwa kifungo hicho baada ya kutiwa hatiani kwa mashtaka ya kughushi muhtasari wa kikao cha Kamati Utendaji ya Shirikisho hilo.

Uamuzi wa kukata rufaa umetolewa leo Jumatatu na Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Wankyo Simon, ambapo alisema upande wa mashtaka umewasilisha nia hiyo ya kukata rufaa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Simon alisema maombi hayo ya rufaa yaliwasilishwa Mahakama Kuu, Desemba 13, 2019.

Alidai kuwa wamewasilisha nia hiyo baada ya kutoridhishwa na adhabu ya hukumu hiyo iliyotolewa na Hakimu Mkazi Mwandamizi Maira Kasonde, aliyekuwa akisikiliza shauri hilo katika makosa waliyotiwa hatiani washtakiwa hao.
 
Tatizo sio Malinzi tatizo ni sheria zetu mbovu.

Yaani makosa ya uhujumu uchumi wa mamilioni faini yake laki 5? are we serius kweli?

Mwanasheria mkuu yupo ofisi, jaji mkuu offisini, waziri wa katiba na sheria yupo ofisini.

Yaani fine haitoshi hata garama ya uendeshaji wa kesi! Serikali inawatumia mawakili na kuwalipa pesa nyingi wakati mwisho wa hukumu ni hasara tupu bora kama hatuna uhakika wa kushughulikia ufisadi bora kuwaacha tu maana hakuna nia njema.
 
Ila ile adhabu haa mahakama jamani! Mwizi wa kuku anakula miaka malinzi anapeta mtaani aliyechezea mpira wa nchi hii kweli! Bora serikali ikate hiyo rufaa
 
Ila ile adhabu haa mahakama jamani! Mwizi wa kuku anakula miaka malinzi anapeta mtaani aliyechezea mpira wa nchi hii kweli! Bora serikali ikate hiyo rufaa
Je alikutwa na hatia kwenye makosa yapi ? yale ya uhujumu uchumi na utakatishaji pesa yalishindwa kuthibitishwa , sasa hukumu isingeweza kutolewa kutokana na hati ya mashitaka pekee
 
Serikali imewasilisha nia ya kukata rufaa Mahakama Kuu, kupinga hukumu na adhabu iliyotolewa na Mahakama ya Kisutu, dhidi ya aliyekuwa rais wa zamani wa TFF, Jamal Malinzi na katibu wake, Celestine Mwesigwa
Kama ameshindikana akiwa ndani ndio atawezekana akiwa nje?!!

Tumuache Jamal adhabu aliyopewa na Fifa inamtosha!
 
Huyu mzee kama kumnyoosha washamnyoosha wamuache tu apumzike sidhan kama atatamani kusikia habar za soka la bongo tena katika maisha yake.

Ni kweli upo sahihi...ila wasiwasi wangu ni kwa wale ndani ya TFF 'waliomchongea' mwenzao...upo usemi wa malipo ni hapa hapa duniani...lets wait and see...
 
Tatizo sio Malinzi tatizo ni sheria zetu mbovu.

Yaani makosa ya uhujumu uchumi wa mamilioni faini yake laki 5? are we serius kweli?

Mwanasheria mkuu yupo ofisi, jaji mkuu offisini, waziri wa katiba na sheria yupo ofisini.

Yaani fine haitoshi hata garama ya uendeshaji wa kesi! Serikali inawatumia mawakili na kuwalipa pesa nyingi wakati mwisho wa hukumu ni hasara tupu bora kama hatuna uhakika wa kushughulikia ufisadi bora kuwaacha tu maana hakuna nia njema.
Wale mawakili wa serikali ni waajiriwa, hulipwa hata wasipoenda mahakamani.
Kule huenda tu kutimiza wajibu.

Unaweza kukuta aliyekata rufaa ni mwanafunzi wa law school ana practice argument skills zake na siyo serikali.

Tanzania mahakama ni za ccm na serikali yao, yeyote mwenye mlengo tofauti na mwenyekiti wao lazima wanamtia adabu.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom