Aniko
JF-Expert Member
- Jan 3, 2016
- 1,766
- 958
Mmh kwakweliMV Dar Es Salaam maarufu kama Meli Chakavu, ilinunuliwa na Waziri wa Ujenzi wa kipindi hicho, Mh. Magufuli, kwa fedha za wapiga kura na Walipa kodi wa Tanzania, kiasi cha Tsh bilioni 7.9, Pamoja na kununuliwa kwa kiasi hicho cha fedha, meli hiyo ni mbovu hivyo kushindwa kufanya kazi kwa viwango vilivyokusudiwa. Inaelea Elea kwenye Bahari ya Hindi bila kurudisha gharama za Fedha za wapiga kura na Walipakodi wa Tanzania.
Uuzwaji wa nyumba za Umma kwa bei chee, nao ulifanywa na Mh. Magufuli. Nyumba hizo ni mali za wapiga kura na walipakodi wa Tanzania.
Kwa sababu yeye sasa ni raia namba moja, Basi atumbuliwe kwa Ufisadi huu.