Serikali yajibu Hoja za Kivuko cha MV Dar es Salaam na Uuzwaji wa Nyumba Zake

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
15,999


Serikali imejibu hoja za upinzani kuhusu uuzwaji wa nyumba za Serikali na kutetea ununuzi wa kivuko cha MV Dar es Salaam ambacho kilitakiwa kufanya safari zake kati ya Dar na Bagamoyo.

Hoja hizo ziliibuliwa katika hotuba ya Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani kwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, James Mbatia akitaka kutekelezwa kwa azimio la Bunge la urejeshwaji wa nyumba hizo serikalini lililotolewa Aprili 2008.

Pia, ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ilibainisha upungufu katika kivuko cha MV Dar es Salaam ambao ni kutolipiwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), kutokuwa na kasi kadri ya mkataba na kutokuwapo hati ya makabidhiano.

Hoja hizo za upinzani zilijibiwa juzi jioni na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa ambaye alisema hakuna taratibu zozote zilizokiukwa wakati wa ununuzi wa kivuko hicho ambacho kwa zaidi ya mwaka hakijaanza kazi.

Alisema wizara ilipata taarifa ya CAG ambayo ilibainisha upungufu kadhaa ikiwa ni pamoja na kivuko hicho kununuliwa kwa Dola za Marekani 4.9 milioni (Sh7.9 bilioni) bila kulipiwa VAT, lakini akasisitiza kwamba hakukuwa na ukiukwaji wowote wa taratibu za ununuzi.

“Ni kweli kivuko kina mapungufu ikiwamo kasi ndogo, lakini hakuna ukiukwaji wowote wa taratibu wakati wa ununuzi. Temesa ilitangaza zabuni na baada ya maombi kupitiwa, kampuni ya MS Jones Gram Hansen ilishinda zabuni hiyo kwa kuwa na bei nafuu,” alisema Profesa Mbarawa.

Alisema baada ya kivuko kuletwa nchini Desemba 2014, kilifanyiwa majaribio na kubainika kwamba hakikuwa na kasi ya kuridhisha. Alisema makubaliano yalikuwa ni kujenga kivuko chenye kasi ya nots20, lakini hicho kilikuwa na kasi ya nots 15.7.

Kutokana na hali hiyo, alisema Serikali ilimtaka mkandarasi kurekebisha kasoro hiyo kwa gharama zake na kuwa ameshawasilisha andiko juu ya namna atakavyoifanya kazi hiyo.

“Mpaka sasa mzabuni huyo hajalipwa asilimia 10 ya malipo yaliyokubaliwa mpaka pale atakapokamilisha kazi hiyo. Kwa hiyo, taratibu zote zilifanyika kwa mujibu wa sheria,” alisema.

Kuhusu nyumba, Profesa Mbarawa alisema Serikali iliidhinisha mpango huo Aprili 24, 2008 baada ya kupata ridhaa ya Bunge ilipopeleka suala hilo kujadiliwa.

“Suala la uuzwaji wa nyumba za Serikali, pia taratibu zilifuatwa. Serikali ilileta mpango huo bungeni na kupata ridhaa ya wabunge wote. Kwa hiyo, niwaambie tu wabunge kwamba suala hili lilipata baraka zao,” alisema waziri huyo.

Uuzwaji wa nyumba za Serikali na ununuzi wa kivuko cha Mv Dar es Salaam vilifanyika wakati Rais John Magufuli akiwa waziri wa ujenzi kwa nyakati tofauti.

Kambi ya upinzani imekuwa ikisisitiza kwamba kuna ukiukwaji wa sheria uliofanyika wakati wa uuzaji wa nyumba na ununuzi wa kivuko hicho. Hata hivyo, Serikali imeshikilia msimamo wake kwamba sheria zilifuatwa.
 
viongozi%2Bmbali%2Bmbali%2Bwakipata%2Bkikombe%2Bcha%2Bbabu%2Bloliondo.jpg


Viongozi wetu hawana budi kurudi kwa babu kupata kikombe cha pili.
 
Hapa naona haijatolea majibu, bali inajidhalilisha.
Kumbuka ishu ya Lugumi, walipo ona uovu huo umefichuliwa baadya kubainika ni vituo 14 tu vya polisi ndivyo vimefungwa mashine haraka sana wakaenda kufuata nyingine ili mwisho wa siku waje watuamimishe kuwa mchakato wa kuzitengeneza ulikuwa bado unaendelea. Tulishapigwa!
 
Swala siyo speed ila swala ni thamani ya kivuko hicho, kimetengenezwa mwaka 1978 kimenunuliwa 8 billions lakini bakharesa kanunua kivuko kipya cha mwaka 2015 kwa ukubwa kama ule na cha kisasa kwa 9 billions
Kaisome na kuielewa sheria ya manunuzi ya umma ndo uje ufananishe manunuzi ya bakhresa na serikali

Sio kila Muda ni kuzungusha mikono tu mkuu
 
Swala siyo speed ila swala ni thamani ya kivuko hicho, kimetengenezwa mwaka 1978 kimenunuliwa 8 billions lakini bakharesa kanunua kivuko kipya cha mwaka 2015 kwa ukubwa kama ule na cha kisasa kwa 9 billions
 
tunataka nyumba za serikali zirudishwe.period.Hizo nyumba sio mali za watu binafsi bali mali ya wananchi.Watu walijiuzia kama pipi, kwa milioni 20 ,akiwemo raisi magufuli kukwapua nyumba mbili .
hizi double standard zitaisha lini,kila mtu lazim awajibike sio kutaka watu fulani kuwajibika.Hili ni kosa na uonevu wa hali a juu.Ni wakati sasa wananchi kufungua kesi mahakamani maana haitendi haki kwa wananchi wake.
leo kuna watu wangapi hawana sehemu nzuri ya kukaa,wanapanga kwa shida.
vijana wetu wanamaliza shule,wanapata kazi,hawana ndoto hata ya kununa nyumba kutokana na mabei makubwa huku wakihangaika kulipa kodi za nyumba halafu wajanja fulani wanajiuzia nyumba kwa bei rahisi mil 20?


leo hii,hawa vijana kama wangekuwa na nafasi ya kununua nyuma milion 20 sidhani kama wangeshindwa kwa bei hio?
kama Magufuli anajifanya kuhubiri haki,basi tuanze na hili.otherwise,she can shut the hell up kuhusu haki na ufisadi.
 
Wakati wabunge wanafanya mauzi ya kuza nyumba za serikali miaka 15 ilio pita ccm ndio ilikua anaongoza bunge kambi ya upinzani ilikua sio kama ya sasa kuna watu mahiri wenye maono tufauti na wabunge wa ccm
 
Swala hapa ni uuzaji huo ulizingatia mashariti yaliyokubaliwa?Waliouziwa ndio walistahili?Waliozinunua wamezingatia mashariti ya mkataba wa mauziano?Kwanini serikali haikusimamia kuona mikataba ya ununuzi wa nyumba hizi unazingatiwa?Wajibu huu ulikuwa ni wa nani kama sio serikali?Serikali ilifumbia macho ukiukwaji wa taratibu za uuzaji wa nyumba hizi kwa maslahi ya nani?

Alafu mbona hii serikali inawafuatilia waliokiuka mikataba ya ubinafsishaji wa mali za umma lakini iko kimya kabisa kuhusu swala la wale waliokiuka mikataba ya ununuzi wa nyumba za serikali kama vile kuuziwa watu wasiostahili?

Kama mnanyang'anya walioshindwa kuendeleza viwanda ama kwa kuvitekeleza au kuvibadilishia matumizi kinyume na mkataba ni kwanini na hawa waliokiuka mikataba ya ununuzi/uuzaji wa nyumba za serikali nao wasinyang'anywe kwa kwenda kinyume na mkataba?Mnamdanganya nani hapa?!

Majibu mepesi kwa maswli magumu!!

Niombenii!!!!Kweli?!!
 
Swala siyo speed ila swala ni thamani ya kivuko hicho, kimetengenezwa mwaka 1978 kimenunuliwa 8 billions lakini bakharesa kanunua kivuko kipya cha mwaka 2015 kwa ukubwa kama ule na cha kisasa kwa 9 billions
 
Pamoja na tuhuma zinazotolewa kuhusu nyumba za serikali, (kivuko hazina uzito wowote), Mazuri anayoyafanya Rais kwa sasa yanazidi mabaya yanayotajwa. hivyo maovu yote aliyoyafanya huko nyuma tumsamehe katika jina la Tanzania.
Hata hivyo, kama atafanya ufisadi akiwa madarakani kama Rais, basi dhambi hiyo itamuandama milele.
 
Suala hapo ni kuwa tumeuziwa kivuko kibovu,chakavu na kwa bei kubwa!Jamani hivi ununue gari unayotegemea ikimbie 120km/hr halafu badala yake ikawa inatembea 90km/hr,halafu unaambiwa fundi atakuja kurekebisha!Hapo jua tu engine mbovu,imechoka!Hii nchi ya kifala sana
 
Pamoja na tuhuma zinazotolewa kuhusu nyumba za serikali, (kivuko hazina uzito wowote), Mazuri anayoyafanya Rais kwa sasa yanazidi mabaya yanayotajwa. hivyo maovu yote aliyoyafanya huko nyuma tumsamehe katika jina la Tanzania.
Hata hivyo, kama atafanya ufisadi akiwa madarakani kama Rais, basi dhambi hiyo itamuandama milele.


Tena ukizingatia ni mtakatifu
 
Back
Top Bottom