Serikali yaishukia bodi ya TTCL, yaitaka kupambana kiushindani

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,698
Reaction score
2,262
TTCL.jpg
​

Dar es Salaam. Serikali imeaiambia bodi mpya ya wakurugenzi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kuacha kuremba, badala yake wajikite kwenye ubunifu huku wakijielekeza kwenye ushindani dhidi ya kampuni zingine za mawasiliano nchini.

“Nataka bodi mjue tunakwenda wapi katika kampuni hii, lakini pia tunahitaji kufanya kazi kwa juhudi kushindana na kampuni nyingine za simu,” alisema Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa alipokuwa akizindua bodi hiyo jana ambapo aliongeza kuwa; “Mhakikishe mapato makubwa yanatoka kwenye data, halikadhalika mnapaswa mjue nguvu yenu iko wapi maana tusipojibu maswali haya hatuwezi kufanya ushindani na kampuni nyingine.”

TTCL ambayo ilibaki nyuma kiushindani kwa muda mrefu, hivi sasa imeibuka kwa nguvu baada ya Serikali kuamua kuirejesha mikononi mwake kutoka kwenye ubia baina yake na Airtel.

Hata hivyo, Profesa Mbarawa alisema asingependa kuiona ikijivutavuta katika hali ya sasa ya soko la mawasiliano ambalo linahitaji ubunifu na mikakati mathubuti ili kuweza kumiliki soko.

Awali, akizungumza katika hafla hiyo, Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa TTCL, Omary Nundu alisema tangu ateuliwe wamefanya mambo mengi hadi sasa ikiwamo kuifufua kampuni hiyo, kushirikiana na wadau wengine wa mawasiliano pamoja na kuanzisha huduma ya utumaji na upokeaji wa fedha maarufu kama TTCL Pesa.

Nundu alisema mwaka 2016, TTCL ilipata Sh0.21 bilioni katika soko na mwaka huu wanatarajia kupata Sh0.3bilioni na kwamba wanatarajia faida ya zaidi ya Sh40 bilioni ifikapo 2022 baada ya makato ya kodi

Chanzo: Mwananchi
 
Wale SU wote wale ndio watabadilisha shirika? Albert Einsten hakukosea...it will be insane
 
Bado sana hao strategy zao mbovu sana. Watumiaji wengi wa simu wanatumia featurephone wenyewe wanakuja na 3G & 4G tu. Watasubiri sana.
Hapa hata mimi nakosoa watanzania wengi tuna simu ndogo ndogo za network ya 2G sasa wao wanataka smartphone tu. Lazima wakose wateja
 
Tatizo simu zao huwezi weka line yoyote ni zao tu
 
Hapa hata mimi nakosoa watanzania wengi tuna simu ndogo ndogo za network ya 2G sasa wao wanataka smartphone tu. Lazima wakose wateja
Kazi kweli kupenya kwenye soko, hili ni jipu lingine kabisa.
 
tatizo hawa watu wanaendssha shirika kisiasa zaidi bila ubunifu, 3G na 4G zinatoka wapi bila ubunifu? Haya ni mawazo ya kupigia picha kwa ajili ya magazeti. Fiber inaharibika wateja wanakaa wiki mbili bila huduma?
 
Dar es Salaam. Serikali imeaiambia bodi mpya ya wakurugenzi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kuacha kuremba, badala yake wajikite kwenye ubunifu huku wakijielekeza kwenye ushindani dhidi ya kampuni zingine za mawasiliano nchini.

“Nataka bodi mjue tunakwenda wapi katika kampuni hii, lakini pia tunahitaji kufanya kazi kwa juhudi kushindana na kampuni nyingine za simu,” alisema Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa alipokuwa akizindua bodi hiyo jana ambapo aliongeza kuwa; “Mhakikishe mapato makubwa yanatoka kwenye data, halikadhalika mnapaswa mjue nguvu yenu iko wapi maana tusipojibu maswali haya hatuwezi kufanya ushindani na kampuni nyingine.”

TTCL ambayo ilibaki nyuma kiushindani kwa muda mrefu, hivi sasa imeibuka kwa nguvu baada ya Serikali kuamua kuirejesha mikononi mwake kutoka kwenye ubia baina yake na Airtel.

Hata hivyo, Profesa Mbarawa alisema asingependa kuiona ikijivutavuta katika hali ya sasa ya soko la mawasiliano ambalo linahitaji ubunifu na mikakati mathubuti ili kuweza kumiliki soko.

Awali, akizungumza katika hafla hiyo, Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa TTCL, Omary Nundu alisema tangu ateuliwe wamefanya mambo mengi hadi sasa ikiwamo kuifufua kampuni hiyo, kushirikiana na wadau wengine wa mawasiliano pamoja na kuanzisha huduma ya utumaji na upokeaji wa fedha maarufu kama TTCL Pesa.

Nundu alisema mwaka 2016, TTCL ilipata Sh0.21 bilioni katika soko na mwaka huu wanatarajia kupata Sh0.3bilioni na kwamba wanatarajia faida ya zaidi ya Sh40 bilioni ifikapo 2022 baada ya makato ya kodi

Chanzo: Mwananchi
Kama hiyo bodi na wakurugenzi wamejaa wazee wa mawazo mgando, hayo maneno ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa. Yaani eti wamewaza sana na kuona kuleta huduma ya pesa kwenye simu huku hakuna watumiaji wa hizo line ndio wazo. Hovyo kabisa. Wana advantage ya kuliteka soko kwa data na speed ya kasi, lakini hawatumii hiyo opportunity, hadi halotel wamekuja na kuwapiga gap. Watoeni hao, wazee ndio chanzo cha majanga yote tuliyonayo na kuendelea kuwaweka hapo ni kutuendelea kuongeza majanga.
 
Ttcl wanatakiwa waangalie kampuni zingine zinatoaje huduma za mawasiliano...
Haiwezekani mmedhamiria kufufua kampuni alaf mnakuwa mnatoa huduma expensive na maeneo mengine havipatikan...
Inabid wakubali kujila kwa muda kama kampuni ya tigo walianzia kwa wanafunzi na kutoa offer nyingi sana ikawa affordable kwa watu wote mpaka watu wakaamua kumiliki sim mbili mbili ili tu aweke line ya tigo... mwisho wa siku watu wakaona tigo rahis wakaachana na mitandao mingine....
Ttcl wajifunze kitu hapa kama bodi inaendesha kampuni kizaman wapigwe chini watafutwe watu wachakatikaj na fast thinker....
Wajifunze airtel wana bando za 200
Hallotel wanabado la 100.. etc
Lkn hata wakiamua offer za kuongea usiku bure...
Internet bure usiku ndo kuwazoesha watu kidogo kidogo mana hakuna kitu kigumu kama kumhamisha mtu kutoka mtandao A kwenda B ni lazima kampuni ikubali kujila....hakuna kula bila ya kuliwa(mzee jk)
 
Bado sana hao strategy zao mbovu sana. Watumiaji wengi wa simu wanatumia featurephone wenyewe wanakuja na 3G & 4G tu. Watasubiri sana.
Nadhani wao mapato yao makubwa yanatokana na 'data services' labda ndo maana wameamua kukomaa na 3G na 4G. Hata hivyo bado safari ni ndefu sana
 
Haya mashirika ya Kiccm ccm yafe tu, ufisadi mtupu hakuna lolote.
 
waongeze coverage maana hapa dar yenyewe hawaja cover wanakimbilia ttclpesa fanyeni kimoja mkimaliza mje na kingine
 
Hapa hata mimi nakosoa watanzania wengi tuna simu ndogo ndogo za network ya 2G sasa wao wanataka smartphone tu. Lazima wakose wateja
Dunia ya Leo ni smartphones. Wakibaki na 2G mmmh! Let them move ahead with 4G.
Waingie ubia na kampuni kubwa ya kuuza smartphone kwa Bei nafuu ya kati.
 
Back
Top Bottom