Sizani kama atapewa bure, hapa kilichokosekana ni namna ya kuwakilisha hoja lakini there's no way kwamba atapewa bure! Nazani kilichopo ni namna ya kupunguza gharama manake nimeshitushwa kwamba kiwanda kinahitaji 70 MW....huu ni umeme mwingi mno....ambae kwa mazingira ya Tanzania unaweza kukuta ni umeme unaotumika karibu mikoa miwili!!
So, nazani katika harakati za kupunguza gharama za uzalishaji, inawezekana ndio sababu ya Dangote kutaka raw material (gas) na kuzalisha umeme wake yenyewe!
Vyovyote iwavyo, jambo la msingi ni kwamba kama atapewa gas basi ainunue gasi hiyo na sio kupewa bure ingawaje sioni ni namna gani atapewa bure!!!
Pamoja na hayo, hofu yangu ni kwamba GAS atatumia lakini NISHATI atakayotumia atatumia at Zero or very small cost! HOW? Ni kwamba ananunua gas kwa bei ya chini kisha anazalisha umeme! 70MW ya produced electricity anaitumia kwenye kiwanda chake na kiasi kinachobaki kinaingizwa kwenye grid ya taifa!
Kimsingi, hicho kiasi sio kwamba kitaingizwa kwenye GRID kama msaada bali atakiuza kwa husika ambao watakiingiza kwenye gridi! So, kuna uwezekano mkubwa kabisa kwamba pesa atakazopata kwa kutuuzia umeme wa gas tuliyomuuzia kwa bei ya chini; pesa hiyo ikawa na uwezo wa ku-recover zile 70MW anazotumia mwenyewe pamoja na umeme aliouza na hivyo kuwa ni kama anatumia bure! It's like mtu mwenye shida na suruali 100 kisha ananunua pamba ya kutengeneza suruali 500, kisha zile 400 anakuuzia mwenyewe wakati gharama za kuzalisha suruali 500 (say) sh. 1000 na pamba alinunua kwa sh. 500 na hivyo kutumia sh.1,500/= wakati suruali moja anauza sh. 5 na hivyo suruali zake 400 anazokurudishia mwenyewe anakuta zimemuingizia sh. 2000 na hivyo kupata faida ya sh.500 na suruali 100 za bure!!!
WAJINGA NDIO WALIWAO!