Leo nimeingia kwenye ofisi moja kudai malipo,na nilikuwa nishataarifiwa kuwa malipo yapo tayari baada ya wiki niende,ile wiki imetimia leo,nikatia timu saa tatu asubuhi ya leo hii, majibu niliyoyapata ni haya,kwa kuwa jamaa nafahamiana nae akanipa ukweli.. nanukuu.. Mkuu wangu kweli nilikupa taarifa uje baada ya wiki lkn hali imebadilika hafla,angalia huu waraka wa serikali unatwambia tusifanye malipo ya aina yoyote,na pesa yote irudi kwa ajili ya shughuli maalum. mwisho wa kunukuu. jamaa akanipa kidogo za ndani akaniambia ccm hawakutegemea hali kama itakuwa ngumu hivi,sasa wameamua kuchukua nguvu za ziada kwani hawana tena uhakika wa kushinda kama walivotegemea. jamani pesa zetu hizoooooooooo