Serikali yagoma kuongeza posho za wanafunzi Urusi
Na Andrew Msechu
SERIKALI imegoma kulipa posho zinazodaiwa na wanafunzi wa Tanzania waliopo katika Chuo Kikuu cha Lumumba mjini Moscow nchini Urusi, waliovamia ubalozi wa Tanzania nchini humo Jumanne wiki hii, kwa maelezo kwamba madai yao si sahihi.
Wanafunzi hao waliopo mwaka wa maandalizi ya lugha katika chuo hicho wanadai kuwa, walitakiwa kulipwa fedha za miezi ya Agosti, Septemba na Oktoba mara baada ya kuwasili chuoni hapo Septemba mwaka jana, lakini hawakulipwa ila walilipwa kuanzia Novemba mwaka jana.
Taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ilikanusha madai ya wanafunzi hao na kusema kuwa, si sahihi na haitambui; na kuwa hawatastahili malipo hayo kwa kuwa walitakiwa kuripoti chuoni hapo Novemba mwaka jana na si Agosti kama wanavyodai.
Taarifa ya wizara hiyo ilieleza jana kuwa, madai hayo si sahihi na kuwa wanafunzi hao walilipwa fedha zao zote za posho tangu Novemba 2007 hadi Septemba 2008 kwa mujibu wa taratibu zilizopangwa na wizara hiyo.
Aidha, taarifa hiyo ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ilieleza kuwa tayari Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu nchini (Helsb), imeshaagizwa kuwalipa wanafunzi hao posho zao za mwaka 2008/09 kuanzia Oktoba mwaka huu.
揌atua zote za kuwashauri wanafunzi hao kuondoka ubalozini hapo zimeendelea kwa siku mbili mfululizo bila mafanikio,?ilieleza taarifa hiyo.
Iliongeza kuwa, wizara hiyo kwa kushirikiana na ubalozi wa Tanzania mjini Moscow, inaendelea na juhudi za kuwashauri wanafunzi hao ili warejee kwenye vyuo vyao kwa ajili ya kuendelea na masomo.
Wanafunzi hao wameendelea kukaa katika ubalozi huo wa Tanzania wakidai kuwa hawataondoka hadi hapo watakapopatiwa posho zao au kupata majibu ya kina yanayoweza kuondoa utata uliopo katika malipo ya posho hizo.
Mwaka jana, Serikali iliwakana wanafunzi wa Tanzania waliokuwa wakisoma nchini Ukraine ambao pia walikuwa wakidai malipo ya posho na ada kutoka Helsb, ikidai kuwa walikwenda kwa utaratibu usiokubalika.
Hatua hiyo ilizua mtafaruku mkubwa kupitia iliyokuwa Wizara ya Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu wakati huo, chini ya aliyekuwa waziri wake, Prof Peter Msolla na wazazi wa wanafunzi hao, suala lililosababisha vyama vya siasa na vya kiraia kuingilia kati.