hamada umelewa
JF-Expert Member
- Dec 17, 2017
- 567
- 985
Unampongeza mtu aliyetengeneza tatizo akaja kuliondoa mwenyewe? MF mtu anakulisha sumu, baada ya kuzidiwa anakupeleka hospitali unatibiwa je, ukipona unatakiwa umshukuru kwa kukupeleka hospitali au umsitaki kwa kukulisha sumu? Pili kama wataondoa hizo tozo za miamala ya kielektroniki pia watuonyeshe walizozikusanya kwa miaka miwili zilifanya kazi gani maana walitwambia ni kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na zahanati lakini mpaka sasa shule nyingi zina upungufu mkubwa wa vyumba vya madarasa mpaka watoto wanasomea chini ya miti.Kupitia muswada wa marekebisho ya sheria ya fedha na kodi.
Kodi na Tozo ambazo si rafiki katika mazingira ya kibiashara zimeondolewa na kufutwa kabisa.
Kodi ya Store ni miongoni mwa kodi zilizoleta mtafaruku hadi kusababisha mgomo kwa wafanyabiashara wa mkoa wa kikodi Kariakoo.
Tozo nyingine zilizopendekezwa kuondolewa ni pamoja na Tozo za miamala pamoja na ushuru wa vitenge kupunguzwa.
Tunampongeza Rais Samia na serikali yake ameonyesha usikivu zaidi katika kuijenga nchi. Mama yuko kazini.
Pia soma
- Mgomo mkubwa Soko la Kariakoo: Maduka yamefungwa, Mei 15, 2023
- UPDATE: Mgomo waendelea Kariakoo kwa Siku ya 3, Wafanyabiashara wataka Mkutano wa Wazi na Majaliwa
- Mgomo wa Kariakoo; Serikali Iwasikilize Wafanyabiashara
- Mwendelezo wa Mgomo, Kiongozi wa Wafanyabiashara Kariakoo adai kuna kikundi kina maslahi binafsi
- Waziri Mkuu Majaliwa aibukia Kariakoo, azungumza na wa fanyabiashara
- Waziri Mkuu Kassim Majaliwa afika Kariakoo. Aagiza task force za TRA kusitisha shughuli zake haraka