Serikali yafuta ada elekezi shule binafsi

katika hili serikali iwe makini sana, ELIMU NI JANGA KWA TANZANIA HIVI SASA, shule za serikali kiukweli kuanzia ngazi ya msingi zinatoa elimu duni na sio za kutegemea kumkomboa mtoto au familia masikini. Hizo shule ambazo basi zinatoa Elimu nzuri ada nayo ni tatizo kubwa saaana, serikali kuna haja ya kusimamia hizi shule kwa ada kulingana na mazingira..
Tafuta hela umpeleke mwanao shule nzur, na serikali isimamie shule za private kwani wanatoa ruzuku ya kuziendesha?
Serikali ilikurupuka kutaka kupanga ada elekezi, hicho kitu hakiwezekani kabisa labda wawape walimu wa bure, umeme wa bure, maji ya bure na chakula ndio watafanikiwa, mfano shule kama FEZA kila mwaka wanapeleka wanafunzi wao kwenye mashindano ya kimataifa ili kuwajengea uwezo zaidi,sasa wewe ukurupuke ukawapangie ada wakati huchangii chochote kile?
Watu wakiona ni ghali waemde wanakostahili, wengi wetu hawatukupitia private kabisa na tulifanya vizur sana kuliko hata private, sasa serikali yetu iboteshe ili kila mtu ajichagulie mwenyewe na wakifanya hivyo huko private watashusha wenyewe bila kulazimishwa
 
Yan we boya kwel asa kama unaona elimu ya bure mbovu mpeleke mwanao kwenye ml hata 15 asa unalia nini si unazo!!!
Sasa wewe na yeye boya ni nani? Kama lugha nyepesi hiyo hujaelewa kwanini usijiite boya mwenyewe? Soma uelewe kabla hujamtukana mtu, ulichosema ndio alichokisema sema lugha ndio hujailewa kabisa.
 
Hii ni habari katika ukurasa wa mbele wa gazeti la Mtanzania la siku ya leo tarehe 05/01/2017.

Habari kamili:

SERIKALI imesisitiza kufutwa kwa mchakato wa kutangaza ada elekezi kwa shule zote binafsi na udhibiti wa ada hizo sasa utafanywa na Kamishna wa Elimu na Idara ya Ukaguzi.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo aliiambia MTANZANIA ofisini kwake jana kuwa baada ya kupokea maoni ya wazazi, walikaa kikao na Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii Mei mwaka jana ambapo waliamua suala la ada elekezi libaki mikononi mwa mzazi na mmiliki wa shule.

““Suala la ada elekezi lilikwishafutwa na Serikali katika tamko lilitolewa na Waziri wa Elimu yeye mwenyewe katika kikao cha Bunge kilichofanyika Mei 27 mwaka jana na kuamuru suala la ada elekezi lisijadiliwe tena,”alisema Dk Akwilapo.

Naibu Katibu Mkuu huyo alisema mzazi yeyote atakayetaka kumpeleka mtoto wake katika shule zisizokuwa za Serikali ni uamuzi wake kwa sababu atakuwa ameshakubaliana na ada iliyopangwa.

Alisema kwa sasa wizara hiyo imeboresha shule zote za Serikali ikiwa ni pamoja na kutoa elimu bure kwa wanafunzi wote.

TAMONGSCO wanena

Akizungumzia suala hilo, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Wamiliki na Mameneja wa Shule na Vyuo visivyo vya Serikali Tanzania (TAMONGSCO) Benjamin Mkonya alipongeza hatua hiyo, huku akisisitiza kuwa suala la ada elekezi ni sawa na suala la kifamilia.

“Suala la upandaji wa ada ni makubaliano baina ya mzazi na mmiliki. Waziri alisisitiza kuwa suala la ada kwa shule zisizokuwa za Serikali hataliingilia,”alisema Mkonya.

Alisema upandishwaji ada kwa shule zisizokuwa za Serikali inategemea na aina ya mahitaji anayoyapata mtoto shuleni na wakati mwingine wazazi wenyewe ndio hutoa oda ya namna mtoto anavyotaka aishi akiwa shuleni.

“Kama mtoto anapewa chakula kizuri, mahitaji mazuri shuleni ni sababu gani itakayosababishwa ashindwe kufaulu, kwa mzazi anayetaka mtoto wake apate elimu bora ni lazima atampeleka katika shule anayoona inafaa,”alisema Mkonya.

Akihitimisha mjadala wa bajeti ya wizara hiyo bungeni Mei mwaka jana, Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako alisema mchakato huo umefungwa baada ya kujadiliana na wamiliki wa shule na Kamati ya Bunge.

Kwa mujibu wa Profesa Ndalichako, usimamizi wa utoaji wa michango na ada holela katika shule hizo utashughulikiwa kwa mujibu wa sera, ambapo kutatakiwa kuwepo kwa kibali kwanza.

Alisema kutokana na hatua hiyo ya Serikali, ambayo inalenga kupata muda wa kutafakari suala hilo na kutafuta namna bora ya udhibiti, sasa hakutakuwa na ada elekezi ila michango itadhibitiwa.

Kabla ya tamko hilo, baadhi ya wabunge walipinga mchakato huo na kutaka Serikali kujikita katika kuboresha shule zake na kuachana na utoaji wa ada elekezi.

Chanzo: Mtanzania

My take:
Zile mbwembwe zimeishia wapi au zilikuwa ni mbio tu za sakafuni?
kuna shida hapa si bure..
 
Tafuta hela umpeleke mwanao shule nzur, na serikali isimamie shule za private kwani wanatoa ruzuku ya kuziendesha?
Serikali ilikurupuka kutaka kupanga ada elekezi, hicho kitu hakiwezekani kabisa labda wawape walimu wa bure, umeme wa bure, maji ya bure na chakula ndio watafanikiwa, mfano shule kama FEZA kila mwaka wanapeleka wanafunzi wao kwenye mashindano ya kimataifa ili kuwajengea uwezo zaidi,sasa wewe ukurupuke ukawapangie ada wakati huchangii chochote kile?
Watu wakiona ni ghali waemde wanakostahili, wengi wetu hawatukupitia private kabisa na tulifanya vizur sana kuliko hata private, sasa serikali yetu iboteshe ili kila mtu ajichagulie mwenyewe na wakifanya hivyo huko private watashusha wenyewe bila kulazimishwa
Nafikiri shida iliyopo ni serikali kuanzisha mchakato ambao hawana uhakika nao kama una tija au la! hapa ni kutuchanganya wananchi mara hivi mara vile...sasa najiuliza hivi ni wajibu wa serikali kuweka ada elekezi kama siyo nani aliwapa hii jeuri ya kusema hivyo! Tunahitaji serikali ifanye mambo yake kwa uhakika na kwa mantiki siyo kubabaisha kama hivi. Tunakosa mwelekeo
 
Hahahahahah! Walimuona 'Rais Dhaifu' Fwala sasa hivi wanarudi kule kule.

Ada
Kama ni 5M kwa nini Ulie lie wakati kuna Ada za
Laki 3
Kwa Mwaka?

Nilipinga humu kwny forum tangu awali kuwa ni Upumbavu
Hakuna aliye lialia ila serikali yenyewe ndio ilitaka kujipendekeza kwa kuingilia mifumo isiyo wahusu. sasa tunaona matokeo yake wanaonekana kama wao ndio wameshindwa. Next time wawe na approach nzuri
 
nia ya serikali ilikuwa nzuri kweka ada elekezi. tatizo nia nzuri pekee haitoshi. mi binafsi kwenye hili nimeipongeza serikali kuachana nalo.

libaki jukumu la mzazi mwenyewe, maana shule zipo nyingi. kuanzia za bure za serikali na za binafsi ambazo zina viwango tofauti tofauti.

ni sawa na maduka ya nguo, nguo yaweza kuwa na bei tofauti kulingana na duka uliloamua kwenda.

kwa hili mi naona serikali imefanya vizuri kuachana na stress zisizo za lazima. na maamuzi mazuri, binafsi sioni haja ya kubeza, japo nia ilikuwa nzuri, lakini ni complicated kiaina.
 
Siasi siasa, Kila jambo linafanywa kisiasa tu
 
Watoto wangu hawatosoma shule za kata fullstop.

Hii ni mbinu ya kuweka tabaka lao tu ndio liendelee kuwa watawala, CEO's and likes halafu sisi makabwela tuzalishe tabaka la wapiga debe na waokota chupa tupu za maji, hii haikubaliki, sipeleki mtoto wangu hata mmoja shule za umma.

Mimi nimesoma shule za umma na shuleni tulikuwa na watoto wa viongozi ma watoto wa wakurugenzi, tulikuwa tunashindana akili tu darasani, na si leo bogus Profesa kama Ndalichake akuaminishe eti mtoto wa shule ya msingi kiburugwa eti anaweza kushindanishwa na mtoto wa FEZA primary school.
hii ni sifa bainifu nyingine kua serikali haiwezi kudhibiti unyonyaji kutoka kwa mabepari. lilianza la sukari ,mafuta,umeme,sasa la upandishwaji wa ada kiholela kwa shule binafsi. tatizo kubwa hapa ni supernormal profit hakuna kingine.
kibaya zaidi wanaoitwa watetezi ndo wanufaika wenyewe yani wamiliki wa shule ni viongozi haohao. ambao pamoja na kutaka liwepo tabaka la kielimu pia wanataka kunufaika na faida kubea .
 
hahaha ukisoma comment za hao wanaoponda kusitishwa kuweka ada elekezi ndio hao hao walisema kuwa kusiwepo na ada elekezi na wengine walisema kuwepo na ada elekezi lakini mpango huo umesitishwa leo hii wale wale wanaanza kushangilia oooh wameshindwa ooooh wamenywea lakini kelele zilianzia kwa hao hao oooh tunatozwa ada kubwa haziendani na tunachopewa oooh. wanao faidika ni wenye shule wala serikali haipati hasara yeyote...endeleeni kushangilia
Lete ushahidi maana kumbukumbu zangu ni kua ulisema serikali inawajari wanyonge ...sasa vipi wanyonge wameisha
 
Hii ni habari katika ukurasa wa mbele wa gazeti la Mtanzania la siku ya leo tarehe 05/01/2017.

Habari kamili:

SERIKALI imesisitiza kufutwa kwa mchakato wa kutangaza ada elekezi kwa shule zote binafsi na udhibiti wa ada hizo sasa utafanywa na Kamishna wa Elimu na Idara ya Ukaguzi.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo aliiambia MTANZANIA ofisini kwake jana kuwa baada ya kupokea maoni ya wazazi, walikaa kikao na Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii Mei mwaka jana ambapo waliamua suala la ada elekezi libaki mikononi mwa mzazi na mmiliki wa shule.

““Suala la ada elekezi lilikwishafutwa na Serikali katika tamko lilitolewa na Waziri wa Elimu yeye mwenyewe katika kikao cha Bunge kilichofanyika Mei 27 mwaka jana na kuamuru suala la ada elekezi lisijadiliwe tena,”alisema Dk Akwilapo.

Naibu Katibu Mkuu huyo alisema mzazi yeyote atakayetaka kumpeleka mtoto wake katika shule zisizokuwa za Serikali ni uamuzi wake kwa sababu atakuwa ameshakubaliana na ada iliyopangwa.

Alisema kwa sasa wizara hiyo imeboresha shule zote za Serikali ikiwa ni pamoja na kutoa elimu bure kwa wanafunzi wote.

TAMONGSCO wanena

Akizungumzia suala hilo, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Wamiliki na Mameneja wa Shule na Vyuo visivyo vya Serikali Tanzania (TAMONGSCO) Benjamin Mkonya alipongeza hatua hiyo, huku akisisitiza kuwa suala la ada elekezi ni sawa na suala la kifamilia.

“Suala la upandaji wa ada ni makubaliano baina ya mzazi na mmiliki. Waziri alisisitiza kuwa suala la ada kwa shule zisizokuwa za Serikali hataliingilia,”alisema Mkonya.

Alisema upandishwaji ada kwa shule zisizokuwa za Serikali inategemea na aina ya mahitaji anayoyapata mtoto shuleni na wakati mwingine wazazi wenyewe ndio hutoa oda ya namna mtoto anavyotaka aishi akiwa shuleni.

“Kama mtoto anapewa chakula kizuri, mahitaji mazuri shuleni ni sababu gani itakayosababishwa ashindwe kufaulu, kwa mzazi anayetaka mtoto wake apate elimu bora ni lazima atampeleka katika shule anayoona inafaa,”alisema Mkonya.

Akihitimisha mjadala wa bajeti ya wizara hiyo bungeni Mei mwaka jana, Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako alisema mchakato huo umefungwa baada ya kujadiliana na wamiliki wa shule na Kamati ya Bunge.

Kwa mujibu wa Profesa Ndalichako, usimamizi wa utoaji wa michango na ada holela katika shule hizo utashughulikiwa kwa mujibu wa sera, ambapo kutatakiwa kuwepo kwa kibali kwanza.

Alisema kutokana na hatua hiyo ya Serikali, ambayo inalenga kupata muda wa kutafakari suala hilo na kutafuta namna bora ya udhibiti, sasa hakutakuwa na ada elekezi ila michango itadhibitiwa.

Kabla ya tamko hilo, baadhi ya wabunge walipinga mchakato huo na kutaka Serikali kujikita katika kuboresha shule zake na kuachana na utoaji wa ada elekezi.

Chanzo: Mtanzania

My take:
Zile mbwembwe zimeishia wapi au zilikuwa ni mbio tu za sakafuni?
Serikali imewatega wazazi.
 
shule za serikali zimeboreshwa nini....? majengo? madawati? walimu wamelipwa madeni yao? walimu wamepigwa msasa....? au elimu bure ndio kuboresha.....?
Mkuu kuna magazeti yalifikia kuandika eti shule binafsi kufungwa eti kutokana na kukosa wanafunzi baada serikali kuboresha shule zake.nilicheka kwa dharau sanaaa,kwa uzuzu huu taifa litazidi kuangamia.
 
hahaha ukisoma comment za hao wanaoponda kusitishwa kuweka ada elekezi ndio hao hao walisema kuwa kusiwepo na ada elekezi na wengine walisema kuwepo na ada elekezi lakini mpango huo umesitishwa leo hii wale wale wanaanza kushangilia oooh wameshindwa ooooh wamenywea lakini kelele zilianzia kwa hao hao oooh tunatozwa ada kubwa haziendani na tunachopewa oooh. wanao faidika ni wenye shule wala serikali haipati hasara yeyote...endeleeni kushangilia
Kinacho tushangaza tulio wengi ni kile ambacho ulimwengu alikiita no serikali ya mkurupukooo.walikurupuka kuja na hiyo sera ya ada elekezi.sasa ushamba wa uongozi umeanza kuwatoka wanafanya waliyotakiwa kufanya.
 
Ndalichako ndiye Waziri mbovu zaidi wa Elimu tangu Taifa hili livumbuliwe na wazungu
 
Umeshaambiwa makubaliano yamefikiwa baada ya majadiliano na kamati ya bunge sasa wengine wanaponda mlitakaje
 
Back
Top Bottom