Serikali yafuta ada elekezi shule binafsi

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,013
144,371
Hii ni habari katika ukurasa wa mbele wa gazeti la Mtanzania la siku ya leo tarehe 05/01/2017.

Habari kamili:

SERIKALI imesisitiza kufutwa kwa mchakato wa kutangaza ada elekezi kwa shule zote binafsi na udhibiti wa ada hizo sasa utafanywa na Kamishna wa Elimu na Idara ya Ukaguzi.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo aliiambia MTANZANIA ofisini kwake jana kuwa baada ya kupokea maoni ya wazazi, walikaa kikao na Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii Mei mwaka jana ambapo waliamua suala la ada elekezi libaki mikononi mwa mzazi na mmiliki wa shule.

““Suala la ada elekezi lilikwishafutwa na Serikali katika tamko lilitolewa na Waziri wa Elimu yeye mwenyewe katika kikao cha Bunge kilichofanyika Mei 27 mwaka jana na kuamuru suala la ada elekezi lisijadiliwe tena,”alisema Dk Akwilapo.

Naibu Katibu Mkuu huyo alisema mzazi yeyote atakayetaka kumpeleka mtoto wake katika shule zisizokuwa za Serikali ni uamuzi wake kwa sababu atakuwa ameshakubaliana na ada iliyopangwa.

Alisema kwa sasa wizara hiyo imeboresha shule zote za Serikali ikiwa ni pamoja na kutoa elimu bure kwa wanafunzi wote.

TAMONGSCO wanena

Akizungumzia suala hilo, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Wamiliki na Mameneja wa Shule na Vyuo visivyo vya Serikali Tanzania (TAMONGSCO) Benjamin Mkonya alipongeza hatua hiyo, huku akisisitiza kuwa suala la ada elekezi ni sawa na suala la kifamilia.

“Suala la upandaji wa ada ni makubaliano baina ya mzazi na mmiliki. Waziri alisisitiza kuwa suala la ada kwa shule zisizokuwa za Serikali hataliingilia,”alisema Mkonya.

Alisema upandishwaji ada kwa shule zisizokuwa za Serikali inategemea na aina ya mahitaji anayoyapata mtoto shuleni na wakati mwingine wazazi wenyewe ndio hutoa oda ya namna mtoto anavyotaka aishi akiwa shuleni.

“Kama mtoto anapewa chakula kizuri, mahitaji mazuri shuleni ni sababu gani itakayosababishwa ashindwe kufaulu, kwa mzazi anayetaka mtoto wake apate elimu bora ni lazima atampeleka katika shule anayoona inafaa,”alisema Mkonya.

Akihitimisha mjadala wa bajeti ya wizara hiyo bungeni Mei mwaka jana, Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako alisema mchakato huo umefungwa baada ya kujadiliana na wamiliki wa shule na Kamati ya Bunge.

Kwa mujibu wa Profesa Ndalichako, usimamizi wa utoaji wa michango na ada holela katika shule hizo utashughulikiwa kwa mujibu wa sera, ambapo kutatakiwa kuwepo kwa kibali kwanza.

Alisema kutokana na hatua hiyo ya Serikali, ambayo inalenga kupata muda wa kutafakari suala hilo na kutafuta namna bora ya udhibiti, sasa hakutakuwa na ada elekezi ila michango itadhibitiwa.

Kabla ya tamko hilo, baadhi ya wabunge walipinga mchakato huo na kutaka Serikali kujikita katika kuboresha shule zake na kuachana na utoaji wa ada elekezi.

Chanzo: Mtanzania

My take:
Zile mbwembwe zimeishia wapi au zilikuwa ni mbio tu za sakafuni?
 
Hii ni habari katika ukurasa wa mbele wa gazeti la Mtanzania la siku ya leo tarehe 05/01/2017.

My take:
Zile mbwembwe zimeishia wapi au zilikuwa ni mbio tu za sakafuni?
nYIE SI NDIO MLIKUWA vinara KUPINGA hili?????SASA HII NI PROVE MOJAWAPO YA KUWA SERIKALI HII NI SIKIVU..mmesikilizwa mnaanza kuhamisha GIA angani tena......Tatzo nyie VIJANA wa bavicha mmelelewa katika MALEZI YA KINAFIKI MNO NA NDIMI MBILI na hao BABA ZENU huko Chamani maana HAMNA MSIMAMO KABSA YA KILE MNACHOKIPIGANIA...MMESIKILIZWA MNAANZA KUJA kubeza TENA......
 
Watoto wangu hawatosoma shule za kata fullstop.

Hii ni mbinu ya kuweka tabaka lao tu ndio liendelee kuwa watawala, CEO's and likes halafu sisi makabwela tuzalishe tabaka la wapiga debe na waokota chupa tupu za maji, hii haikubaliki, sipeleki mtoto wangu hata mmoja shule za umma.

Mimi nimesoma shule za umma na shuleni tulikuwa na watoto wa viongozi ma watoto wa wakurugenzi, tulikuwa tunashindana akili tu darasani, na si leo bogus Profesa kama Ndalichake akuaminishe eti mtoto wa shule ya msingi kiburugwa eti anaweza kushindanishwa na mtoto wa FEZA primary school.
 
Watoto wangu hawatasoma shule za Kata, tena nafikiria hata vyuo watasoma UK au USA
 
Walikuwa wanamhamisha faru joni.
Kesha hama na mpaka sasa hajulikani aliko
Hii ni habari katika ukurasa wa mbele wa gazeti la Mtanzania la siku ya leo tarehe 05/01/2017.

Habari kamili:

SERIKALI imesisitiza kufutwa kwa mchakato wa kutangaza ada elekezi kwa shule zote binafsi na udhibiti wa ada hizo sasa utafanywa na Kamishna wa Elimu na Idara ya Ukaguzi.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo aliiambia MTANZANIA ofisini kwake jana kuwa baada ya kupokea maoni ya wazazi, walikaa kikao na Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii Mei mwaka jana ambapo waliamua suala la ada elekezi libaki mikononi mwa mzazi na mmiliki wa shule.

““Suala la ada elekezi lilikwishafutwa na Serikali katika tamko lilitolewa na Waziri wa Elimu yeye mwenyewe katika kikao cha Bunge kilichofanyika Mei 27 mwaka jana na kuamuru suala la ada elekezi lisijadiliwe tena,”alisema Dk Akwilapo.

Naibu Katibu Mkuu huyo alisema mzazi yeyote atakayetaka kumpeleka mtoto wake katika shule zisizokuwa za Serikali ni uamuzi wake kwa sababu atakuwa ameshakubaliana na ada iliyopangwa.

Alisema kwa sasa wizara hiyo imeboresha shule zote za Serikali ikiwa ni pamoja na kutoa elimu bure kwa wanafunzi wote.

TAMONGSCO wanena

Akizungumzia suala hilo, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Wamiliki na Mameneja wa Shule na Vyuo visivyo vya Serikali Tanzania (TAMONGSCO) Benjamin Mkonya alipongeza hatua hiyo, huku akisisitiza kuwa suala la ada elekezi ni sawa na suala la kifamilia.

“Suala la upandaji wa ada ni makubaliano baina ya mzazi na mmiliki. Waziri alisisitiza kuwa suala la ada kwa shule zisizokuwa za Serikali hataliingilia,”alisema Mkonya.

Alisema upandishwaji ada kwa shule zisizokuwa za Serikali inategemea na aina ya mahitaji anayoyapata mtoto shuleni na wakati mwingine wazazi wenyewe ndio hutoa oda ya namna mtoto anavyotaka aishi akiwa shuleni.

“Kama mtoto anapewa chakula kizuri, mahitaji mazuri shuleni ni sababu gani itakayosababishwa ashindwe kufaulu, kwa mzazi anayetaka mtoto wake apate elimu bora ni lazima atampeleka katika shule anayoona inafaa,”alisema Mkonya.

Akihitimisha mjadala wa bajeti ya wizara hiyo bungeni Mei mwaka jana, Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako alisema mchakato huo umefungwa baada ya kujadiliana na wamiliki wa shule na Kamati ya Bunge.

Kwa mujibu wa Profesa Ndalichako, usimamizi wa utoaji wa michango na ada holela katika shule hizo utashughulikiwa kwa mujibu wa sera, ambapo kutatakiwa kuwepo kwa kibali kwanza.

Alisema kutokana na hatua hiyo ya Serikali, ambayo inalenga kupata muda wa kutafakari suala hilo na kutafuta namna bora ya udhibiti, sasa hakutakuwa na ada elekezi ila michango itadhibitiwa.

Kabla ya tamko hilo, baadhi ya wabunge walipinga mchakato huo na kutaka Serikali kujikita katika kuboresha shule zake na kuachana na utoaji wa ada elekezi.

Chanzo:Mtanzania

My take:
Zile mbwembwe zimeishia wapi au zilikuwa ni mbio tu za sakafuni?
 
nYIE SI NDIO MLIKUWA vinara KUPINGA hili?????SASA HII NI PROVE MOJAWAPO YA KUWA SERIKALI HII NI SIKIVU..mmesikilizwa mnaanza kuhamisha GIA angani tena......Tatzo nyie VIJANA wa bavicha mmelelewa katika MALEZI YA KINAFIKI MNO NA NDIMI MBILI na hao BABA ZENU huko Chamani maana HAMNA MSIMAMO KABSA YA KILE MNACHOKIPIGANIA...MMESIKILIZWA MNAANZA KUJA kubeza TENA......
Sasa tamko rasmi lilikuwa la nini wakati ilikuwa ni proposal tu?...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom