Serikali yadai watanzania hawapendi kula nyama

Serikali yadai watanzania hawapendi kula nyama

MakinikiA

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2017
Posts
5,801
Reaction score
8,152

Katibu Mkuu wa Wizara ra Mifugo na Uvuvi, Dkt. Elisante Ole Gabriel amesema kila Mtanzania anatakiwa kula kilo 50 za nyama kwa mwaka ili kuwafanya wawe na afya bora, pamoja na kuwataka Watanzania kuongeza zaidi suala la ulaji wa nyama.


Katibu Mkuu Elisante Ole Gabriel ametoa kauli hiyo wakati alipotembelea Makao Makuu Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) jijini Dodoma, ambapo amesema kwa mujibu wa Shirika la Chakula Duniani (FAO), kila Mtanzania anakula kilo 15 tu kwa mwaka jambo ambalo si toshelezi.

"Mtazamo wetu kama Wizara, NARCO itumie fursa hii ya ya soko la nyama hapa Tanzania kwa ajili ya kuuza na kuhamasisha watanzania kula nyama, takwimu za Shirika la Chakula Duniani zimeonesha Watanzania wengi ni wavivu kula nyama.", amesema Ole Gabriel.

"Takwimu zinaonesha kila Mtanzania anatakiwa kula nyama kilo 50 kwa mwaka, lakini Watanzania ni wavivu kula nyama ndiyo maana takwimu zinaonesha kila Mtazania anakula kilo 15 kwa mwaka, kwa hiyo muhimu sana NARCO wakatumia fursa hii" ameongeza.
 
Mkuu wetu sio hatupendi kula nyama , tatizo ni shekeli ya kununua nyama.
 
Watanzania ni wavivu kula nyama ndiyo maana takwimu zinaonesha kila Mtazania anakula kilo 15 kwa mwaka, kwa hiyo muhimu sana NARCO wakatumia fursa hii" ameongeza.

Suala hapa ni uvivu au uwezo? Maana hata hiyo kilo 15 mliosema kila Mtanzania anakula sijui wameitoa wapi?
 
Hizi kauli za kipuuzi niliwahi kuzikuta kwenye Kitabu flani kati ya Man of the People au an Enemy of the People
 
Ukichanganya nyama zote au ng;ombe tu maana ukichanganya zote namba zinapanda na kuzidi kilo 50
 
Mara ya mwisho kula nyama ya Ng'ombe ilikuwa 2014 mpaka leo sijakula tena .

Nakula sana Samaki na Kuku niliamua kubadilisha mfumo wa maisha baada ya stori nyingi kuhusu nyama nyekundu. Though my family( wife , children and siblings) is still eating red meat sikutaka kuwa jiwe(JPM) niliwashauri ila hawakunielewa.

Isitoshe gharama ya nyama kwa familia za watanzania walio wengi ni kubwa sana i guess kila ya nyama kwenye butcher za wagogo ni almost Tsh 6000/kg so itakuwa ngumu sana kwa familia inayoishi kwenye uchumi wa chini ya dollar moja kuweza kumudu hizi gharama halafu ukizingatia hawa ndio majority ya watanzania.
 
Hizo Takwimu wamezitoa wapi? Huwa nakula nyama mwisho wa mwezi tu tena nanunua kilo tunakula familia mzima watu 6.

Ukipiga hesabu hata kilo 5 sifikishi.
 
Watanzania ni wavivu kula nyama ndiyo maana takwimu zinaonesha kila Mtazania anakula kilo 15 kwa mwaka, kwa hiyo muhimu sana NARCO wakatumia fursa hii" ameongeza.

Suala hapa ni uvivu au uwezo? Maana hata hiyo kilo 15 mliosema kila Mtanzania anakula sijui wameitoa wapi?
[emoji23][emoji23]kilo 15 tu
 
Hizi takwimu wanapataje maana hata maziwa pia takwimu zionesha ni wavivu kunywa?
 
Back
Top Bottom