Serikali yachoma moto nyaraka kuficha ufisadi madini

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,890
6,896
Zitt(2).jpg
10zittomakinda.jpg
Zitto afichua ufisadi madini
Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, ameshauri Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kukagua mapato katika sekta ya madini ya miaka 10 iliyopita, kutokana na jumla ya mapato yaliyolipwa na makampuni ya madini kwa serikali kubainika yalikuwa na tofauti ya Sh. bilioni 20. Zitto alisema kuwa kiasi ambacho wawekezaji walidai kuwa walilipa kama kodi kilikuwa pungufu ya Sh. bilioni 20 kulinganisha na kiasi kilichoelezwa na serikali.

Alitoa ushauri huo wakati akichangia mjadala wa bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha wa 2011/2012, bungeni, mjini hapa jana.
Alisema tofauti hiyo ilitokana na ripoti iliyotolewa na Taasisi iitwayo Extractive Industries Transparency Initiative (EITI) baada ya kukagua malipo yaliyofanywa na makampuni ya madini kwa serikali mwaka huo. Zitto alisema ushauri huo ni muhimu kutekelezwa kwani utasaidia kuepuka ugonjwa unaoikumba nchi ya Nigeria, ambako fedha zinalipwa kama mapato ya serikali, lakini zinaishia kuingia mifukoni mwa watu binafsi.

Alisema mamlaka husika ya serikali ilipoulizwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mashirika ya Umma (POAC, ambayo yeye (Zitto) ni mwenyekiti wake, ilidai kuwa nyaraka zinazohusiana na suala hilo zimechomwa moto.

Alisema baada ya ushuru wa mafuta ya taa kuongezwa kutoka Sh. 52 hadi 400.30, serikali inapaswa sasa kutoa agizo ushuru huo upelekwe kwa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ili ukasaidia umeme vijijini. Alisema wakati wa bajeti kulikuwa na malalamiko mengi yaliyotolewa na baadhi ya wabunge kuhusu misamaha ya kodi, lakini serikali ilishikilia msimamo wake kwamba, lazima misamaha hiyo iendelee. Hata hivyo, alisema kuna msamaha wa kodi uliotolewa na serikali, ambao anadhani serikali haikufikiria vizuri katika kuutoa. Alisema jambo hilo alilijadili vizuri kwenye Kamati ya Fedha na Uchumi na kwamba, alitarajia kuwa lingebadilishwa kwenye Bunge lilipokaa kama kamati ya matumizi, lakini haikufanyika.

Alisema Waziri Mkuu alikutana na makampuni ya kutafuta mafuta nchini wakamuomba kwamba, waondolewe kodi katika mafuta wanayotumia katika kutafuta mafuta kwa madai kwamba, jambo hilo litasaidia uwekezaji zaidi. Hata hivyo, alisema kwa sasa hivi kwenye eneo la utafutaji mafuta na gesi hakuna wa kushindana na Tanzania na pia serikali haiwezi kutoa vivutio kama ambavyo Kenya wanatoa, kwani wana makampuni manne yanayotafuta mafuta wakati Tanzania ina makampuni zaidi ya 22. Alisema pia Tanzania haiwezi kutoa vivutio kama Msumbiji wanavyotoa, kwani faida pekee waliyonayo (Msumbiji) ni gesi waliyoigundua, ambayo iko kusini mwa Mkoa wa Mtwara. Zitto alisema kitu, ambacho serikali inatakiwa kukifanya ni kuhakikisha kiwanda cha gesi (LNG plant) kinajengwa haraka iwezekanavyo kabla Msumbiji hawajafanya hivyo.

Alisema Tanzania haitakuwa na faida ya kutoa vivutio kwa mafuta ya makampuni, ambayo yanatafuta madini, kwani itapoteza fedha bila sababu ya msingi. "Na jambo hili ni la kuangalia kwa sababu kwenye mikataba yetu ya mafuta tuna vitu viwili; kuna kitu kinaitwa profit oil na coast oil. Coast oil maana yake ni kwamba kampuni ya mafuta ikishapata mafuta inatoa gharama zake zote, wanajilipa. Wakishajilipa zile gharama za mafuta yaliyoabaki ya ziada ndio tunayogawana,” alisema.

CHANZO: NIPASHE
 
Miaka michache kabla ya uchaguzi wa mwakajana tulishuhudia serikali kuchoma moto hati wa wapiga kura kwenye moja ya warehouse Pugu Road Dar na Mwenyekiti wa CUF Ibarahimu Lipumba kutonywa na watu na kishwa akaenda kushuhudia na akachukua vielelezo vichache kama ushahidi, na sijui kesi hiyo ilivyozimwa haijulikani.

Leo hii Mbunge Zito Kabwe anakuja na tuhuma dhiti ya serikali kuchoma moto nyaraka zinazohusu malipo ya mapato ya makampuni ya madini kwa serikali. Kuna siri gani inayofichwa isijulikane au pesa hizo zinaingia mifukoni mwa watu binafsi?
 
mimi siilaumu serikali ya CCm kwa kufanya huo umafia, nawalaumu watanzania wenzangu (including me) kwa ukondoo wetu!! hawa watu wanathubutu kufanya hivi kwa sababu wana uhakika wa 100% hawtafanywa kitu!!!
 
Wenyewe wanasema wajinga ndo waliwao
 
Jamani naomba kuuliza kuhusu utaratibu wa kumiliki siraha kisheria tz uko vipi? Haya mambo yanazidi kunichefua inabidi nitafute nyenzo then nianzishe kasheshe najua siku moja Tz itanikumbuka.

Haiwezekani watu wachome moto nyaraka muhimu then tunakaa kimya tunawaangalia na serikali haitoi majibu ya kuridhisha.
 
mimi siilaumu serikali ya CCm kwa kufanya huo umafia, nawalaumu watanzania wenzangu (including me) kwa ukondoo wetu!! hawa watu wanathubutu kufanya hivi kwa sababu wana uhakika wa 100% hawtafanywa kitu!!!

Nani atamfunga paka kengele? Unaona wawakilishi wenye uchungu na Tanzania yetu wanavyozomewa bungeni na wabunge wa magamba kwa kuwatibulia ulaji?
 
Hivi Tanzania hatuna sheria kuhusiana na hizi nyaraka za serikali zintakiwa kutunzwa kwa kipindi cha muda gani? Kama zipo basi waliohusika na kuchoma moto nyaraka hizi wapandishwe kizimbani haraka ili kujibu mashtaka mazito dhidi yao.
 
Jamani naomba kuuliza kuhusu utaratibu wa kumiliki siraha kisheria tz uko vipi? Haya mambo yanazidi kunichefua inabidi nitafute nyenzo then nianzishe kasheshe najua siku moja Tz itanikumbuka.

Haiwezekani watu wachome moto nyaraka muhimu then tunakaa kimya tunawaangalia na serikali haitoi majibu ya kuridhisha.

Ujasiri alio nao Zito si wa kawaida, uchache wa wabunge wa kambi ya upinzania ndio ngao ya serikali kujikinga makombora makali ya Chadema na kafulila wa NCCR
 
Hivi Tanzania hatuna sheria kuhusiana na hizi nyaraka za serikali zintakiwa kutunzwa kwa kipindi cha muda gani? Kama zipo basi waliohusika na kuchoma moto nyaraka hizi wapandishwe kizimbani haraka ili kujibu mashtaka mazito dhidi yao.

Sijajua kama kuna shiria inayoruhusu kuchoma nyaraka muhimu za serikali, mbona ziku za nyuma tulikukwa tunaambiwa faili liko ndani kwenye chumba cha giza hivyo wanahitaji tochi kumulika walitafute ili washughulikie mafao ya baba yangu?

Sasa TAKUKURU nini zaidi ya ushahidi wanaohitaji kwa shauri kama hili ambapo maofisa wa serikali wanachoma moto nyaraka muhimu ambazo ni vielelezo vya utendaji wa serikali?
 
Hivi Tanzania hatuna sheria kuhusiana na hizi nyaraka za serikali zintakiwa kutunzwa kwa kipindi cha muda gani? Kama zipo basi waliohusika na kuchoma moto nyaraka hizi wapandishwe kizimbani haraka ili kujibu mashtaka mazito dhidi yao.
Sheria zipo lakini zinafanya kazi tu kama mtuhumiwa ni mpinzani. angalia maguvu ya dola yanayotumika kushughulikia wapinzani! wezi na mafisadi wanatanua tu
 
Mbunge wa CCM anayetuhumiwa kwa njama za mauaji analindwa na bunge na vyombo vya sheria kutomchukulia sheria tofauti na shiria ndogo ya traffic inayomkabili Mbowe kuwekwa ndani wakati akiwa kwenye mikutano ya bunge.
 
Mbunge wa CCM anayetuhumiwa kwa njama za mauaji analindwa na bunge na vyombo vya sheria kutomchukulia sheria tofauti na shiria ndogo ya traffic inayomkabili Mbowe kuwekwa ndani wakati akiwa kwenye mikutano ya bunge.
 
Jamani naomba kuuliza kuhusu utaratibu wa kumiliki siraha kisheria tz uko vipi? Haya mambo yanazidi kunichefua inabidi nitafute nyenzo then nianzishe kasheshe najua siku moja Tz itanikumbuka.

Haiwezekani watu wachome moto nyaraka muhimu then tunakaa kimya tunawaangalia na serikali haitoi majibu ya kuridhisha.

Sheria ipo,lkn ni rahisi kutumia bomu kama ni jeshi la mtu moja,otherwise ni kuingia msituni kama gen Laurent Nkunda
 
Tanzania Tanzania! jamani hadi lini tutazidi kuwa vichwa vya wendawazim? Tunatakiwa tuingilie Kati jamani, tunawaangalia hawa watu hadi lini?
 
Kwanza kabisa wanaochimba madini kwa silimia tatu wafukuzwe kabisa. Hutana maslahi nao. Sasa hapa panahitajika maandamano ya kazi.

Zitt(2).jpg
10zittomakinda.jpg
Zitto afichua ufisadi madini
Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, ameshauri Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kukagua mapato katika sekta ya madini ya miaka 10 iliyopita, kutokana na jumla ya mapato yaliyolipwa na makampuni ya madini kwa serikali kubainika yalikuwa na tofauti ya Sh. bilioni 20. Zitto alisema kuwa kiasi ambacho wawekezaji walidai kuwa walilipa kama kodi kilikuwa pungufu ya Sh. bilioni 20 kulinganisha na kiasi kilichoelezwa na serikali.

Alitoa ushauri huo wakati akichangia mjadala wa bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha wa 2011/2012, bungeni, mjini hapa jana.
Alisema tofauti hiyo ilitokana na ripoti iliyotolewa na Taasisi iitwayo Extractive Industries Transparency Initiative (EITI) baada ya kukagua malipo yaliyofanywa na makampuni ya madini kwa serikali mwaka huo. Zitto alisema ushauri huo ni muhimu kutekelezwa kwani utasaidia kuepuka ugonjwa unaoikumba nchi ya Nigeria, ambako fedha zinalipwa kama mapato ya serikali, lakini zinaishia kuingia mifukoni mwa watu binafsi.

Alisema mamlaka husika ya serikali ilipoulizwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mashirika ya Umma (POAC, ambayo yeye (Zitto) ni mwenyekiti wake, ilidai kuwa nyaraka zinazohusiana na suala hilo zimechomwa moto.

Alisema baada ya ushuru wa mafuta ya taa kuongezwa kutoka Sh. 52 hadi 400.30, serikali inapaswa sasa kutoa agizo ushuru huo upelekwe kwa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ili ukasaidia umeme vijijini. Alisema wakati wa bajeti kulikuwa na malalamiko mengi yaliyotolewa na baadhi ya wabunge kuhusu misamaha ya kodi, lakini serikali ilishikilia msimamo wake kwamba, lazima misamaha hiyo iendelee. Hata hivyo, alisema kuna msamaha wa kodi uliotolewa na serikali, ambao anadhani serikali haikufikiria vizuri katika kuutoa. Alisema jambo hilo alilijadili vizuri kwenye Kamati ya Fedha na Uchumi na kwamba, alitarajia kuwa lingebadilishwa kwenye Bunge lilipokaa kama kamati ya matumizi, lakini haikufanyika.

Alisema Waziri Mkuu alikutana na makampuni ya kutafuta mafuta nchini wakamuomba kwamba, waondolewe kodi katika mafuta wanayotumia katika kutafuta mafuta kwa madai kwamba, jambo hilo litasaidia uwekezaji zaidi. Hata hivyo, alisema kwa sasa hivi kwenye eneo la utafutaji mafuta na gesi hakuna wa kushindana na Tanzania na pia serikali haiwezi kutoa vivutio kama ambavyo Kenya wanatoa, kwani wana makampuni manne yanayotafuta mafuta wakati Tanzania ina makampuni zaidi ya 22. Alisema pia Tanzania haiwezi kutoa vivutio kama Msumbiji wanavyotoa, kwani faida pekee waliyonayo (Msumbiji) ni gesi waliyoigundua, ambayo iko kusini mwa Mkoa wa Mtwara. Zitto alisema kitu, ambacho serikali inatakiwa kukifanya ni kuhakikisha kiwanda cha gesi (LNG plant) kinajengwa haraka iwezekanavyo kabla Msumbiji hawajafanya hivyo.

Alisema Tanzania haitakuwa na faida ya kutoa vivutio kwa mafuta ya makampuni, ambayo yanatafuta madini, kwani itapoteza fedha bila sababu ya msingi. "Na jambo hili ni la kuangalia kwa sababu kwenye mikataba yetu ya mafuta tuna vitu viwili; kuna kitu kinaitwa profit oil na coast oil. Coast oil maana yake ni kwamba kampuni ya mafuta ikishapata mafuta inatoa gharama zake zote, wanajilipa. Wakishajilipa zile gharama za mafuta yaliyoabaki ya ziada ndio tunayogawana," alisema.

CHANZO: NIPASHE
 
Tanzania Tanzania! jamani hadi lini tutazidi kuwa vichwa vya wendawazim? Tunatakiwa tuingilie Kati jamani, tunawaangalia hawa watu hadi lini?

Mzee Ruksa alishasema Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu kila taifa na matajiri waji kujifunza unyozi
 
mungu akuzidishie uhai, akutie nguvu zaidi,akuepushe na kila baya mh Zitto! mama angu ni ccm damu toka enzi za tanu,juzi kwa mara ya kwanza aliniambia mwanangu kama huyu mtoto atakuja gombea urais basi nitampa kura yangu,watu wanaanza kuelewa sasa kwamba kuna wazalendo wa kweli.
 
On a separate note: Kuna wakati REX attorneys waliteuliwa na Serikali kuishauri kwenye mambo ya ugawaji wa vitalu (tourism), na sheria ya madini i believe. Kwenye riport ya bunge (2007/2008) wamegusia tu. Nimetafuta the whole report for months now sijaipata. If anyone knows how or where to get the report please let me know. Thanks
 
mungu akuzidishie uhai, akutie nguvu zaidi,akuepushe na kila baya mh Zitto! mama angu ni ccm damu toka enzi za tanu,juzi kwa mara ya kwanza aliniambia mwanangu kama huyu mtoto atakuja gombea urais basi nitampa kura yangu,watu wanaanza kuelewa sasa kwamba kuna wazalendo wa kweli.

Inatia moyo ee hata wazee wameanza legea mioyo kwa mawazo ya damu mpya
 
Back
Top Bottom