Serikali yaanza kuajiri makada wa CCM bila kuwafanyia usaili

Hata mimi kadi ya chama ninayo wanipe huo utendaji basi

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu yaani huwezi kuamini haya mauzauza yanayofanyika ktk nchi hii. Kuna makada wengi tu wenye kadi lakini hawapati kazi kirahisi....wanachagua wale wenye roho mbaya ndio wanawapa ajira ili waende kutokomeza upinzani huko mashinani. Haya ndio malengo ya Rais katika mchakato wake wa kuufuta upinzani ifikapo 2020. Nchi hii imeoza kabisa.
 
Mfumo wa ajira serikalini umeingiliwa na CCM. Serikali sasa imeanza kuajiri watendaji wa Kata ambao ni makada wa CCM katika kata ambazo zinaongozwa na wapinzani au zile ambazo CCM walishinda kwa tundu la sindano. Mambo haya tulizoea kuyaona katika ngazi za juu za uongozi – wakurugenzi, wakuu wa wilaya na maofisa utumishi – lakini sasa ugonjwa huu umeshuka hadi mashinani.

Mwanzoni mwa mwezi huu wa pili, kamati za CCM ziliketi na kuteua makada ambao majina yao yalipelekwa TAMISEMI na kupangiwa vituo vya kazi kwenye Kata. Kibaya zaidi watendaji waliopo kwenye Kata walikopelekwa makada hao, wameondolewa na kupangiwa kazi zingine ndani ya halmashauri. Na wengi wa makada hao wana elimu ya cheti kutoka chuo cha CCM cha Kivukoni tofauti na matakwa ya kisheria ambayo yanataka mtendaji wa kata walau awe na digrii. Inasikitisha kuwaondoa watendaji walioenda shule na nafasi zao kuchukuliwa na makada mbumbumbu kwa misingi ya kisiasa.

Aidha, ikumbukwe kwamba kuna wahitimu wasiohesabika huko mitaani wenye elimu na ujuzi stahiki lakini serikali imewatelekeza na badala yake kuajiri makada wa chama. Hii nchi sasa inakoelekea ni Mungu tu ndiye anayejua. Nchi inarudishwa kwenye ukoloni. Wakati wa ukoloni waafrika walikuwa wakibaguliwa na wazungu kwa kupewa kazi za ovyo ovyo huku wazungu wakipewa kazi nzuri. Tangu mkoloni ang’olewe nchini Tanganyika, nchi hii haijawahi kushuhudia ubaguzi ktk ajira kama huu unaofanywa na serikali ya CCM ya awamu ya 5.

Ubaguzi huu unatia hasira sana. Hivi kweli CCM hawa makada mmekosa kuwatafutia kazi huko kwenye chama hadi mkaamua kuja kuwachomeka kwenye ajira pasipo kufanyiwa usairi wala nafasi hizo kutangazwa? Na kama mjuavyo, nafasi za utendaji wa Kata bado hazijatangazwa kwa kuwa bado serikali ipo kwenye zoezi la uhakiki. Iweje mseme mpo kwenye uhakiki na wakati huo huo mnachomeka makada wenu kazini na kuwaagiza wakurugenzi wawaingize kwenye payroll? What a shame!

Ndugu zangu nchi hii imeingiliwa na panya (CCM). Hawa sio wanyama wazuri hata kidogo. Hivi haya mambo ya ajabu mnayofanya katika nchi hii mnadhani wale watanzania wenye sifa ambao sio makada wa CCM watajisikiaje?

Ama kweli CCM ni ukoo wa panya—babu mwizi, baba mwizi, watoto wezi, wajukuu wezi, vitukuu wezi, vilembwe wezi na vining’ina wezi! Ukoo huu wa panya walikuwa wanasafiri katika boti la muhogo, lakini kwa sababu ya uroho wao, walianza kulitafuna boti! Kilichofuata ni ukoo mzima wa kizazi cha panya kuzama na kuangamia.

CCM wameanza kuitafuna nchi tangu mwaka 1961 lakini ukomo wao wa kutafuna rasilimali za nchi ni mwaka 2020 kwani hakuna mtanzania mwenye hamu ya kuongozwa na chama cha kifisadi kama CCM ambacho kimeshindwa kuboresha maisha na ustawi wa watanzania. Wananchi wamechoka kubebeshwa ‘magunia ya misumari’ ya bei ya juu ya chakula, mfumuko wa bei wa kutisha, elimu duni, maisha duni, ufisadi wa kutisha na matatizo lukuki yanayosababishwa na panya (CCM) hawa wasiokuwa na haya! Kizazi kizima cha CCM kinakaribia kuzama na kusahaulika kabisa katika ardhi ya Tanzania.

It’s a matter of time before CCM dynasty comes to an end, and that’s when magambas will apprehend the significance and power of the people. Desolately, CCM have been ignoring and looking down their noses at common Tanzanians for many years. Time has now come when citizens can no longer endure CCM’s tyranny and corrupt rule. Everybody is tired of living like a slave on a land endowed with an assortment of natural wealth which only benefits minority fisadis and a few elites in power while majority Tanzanians lead very miserable lives.

What comes around goes around. Let CCM go to hell for good because they have absolutely failed to uplift the living standards of millions of Tanzanians at the expense of a few fisadis whose gargantuan stomachs never fill up! And no one should be blamed for the hatred and grudge that majority people hold against CCM and their crooked government except fisadis themselves who, horrifically, decided to gnaw the cassava-made boat by which they were sailing!
Kwa hali kama hii, kuna kila dalili kuwa serikali ya CCM imekusudia kuwatumia watendaji (WEOs) hawa kupora kura za UKAWA. Upuuzi huu haukubaliki hata kidogo. Endapo CCM watajaribu kuiba kura kwa mtindo huu, lazima damu itamwagika.
 
Dawa yao ni kuwafutilia mbali hawa kupe kuanzia uchaguzi wa mwaka huu maana inaonekana wanathamini siasa zaidi ya kitu chochote. Tukiendelea kuwachekea hawa panya watatusumbua sana siku zijazo.
CCM ni waTanzania,
na wewe ni Mtanzania,
Hali ilivyo huko Bara ilikuwa hivyo Zanzibar miaka 15 nyuma na hatime CCM inapumulia GESI
Kilichobakia wanatumia Nguvu za Dola na Tume isiyokuw Huru kubadilisha matokeo. Si unamkumbuka Jecha alivyo ifanya CUF 2015.?
Sasa sijui Watanganyika wataendelea kusimulia tuu hali ilivyo na kulalamika au watachukua hatua stahiki?
Hao ni watu na Nyinyi ni watu,
Tofauti ni maamuzi ya kuamua kupambana na watu wanao kusudia kuwaangamiza watu wenzao kwa kisanduku cha kura au nguvu za Dola.
Ukiona SISIEMU WANATUMIA HILA NYINGI NA NGUVU KUBWA ,UJUWE HALI INAWABANA KATIKA ENEO HILO.
Kazeni msuli WaTanganyika , Haki yenu lazima igombaniwe kwa Jasho na damu.Mukizuba, Panya watamaliza nafaka.
 
Back
Top Bottom