Serikali yaanza kuajiri makada wa CCM bila kuwafanyia usaili

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
21,822
18,245
Mfumo wa ajira serikalini umeingiliwa na CCM. Serikali sasa imeanza kuajiri watendaji wa Kata ambao ni makada wa CCM katika kata ambazo zinaongozwa na wapinzani au zile ambazo CCM walishinda kwa tundu la sindano. Mambo haya tulizoea kuyaona katika ngazi za juu za uongozi – wakurugenzi, wakuu wa wilaya na maofisa utumishi – lakini sasa ugonjwa huu umeshuka hadi mashinani.

Mwanzoni mwa mwezi huu wa pili, kamati za CCM ziliketi na kuteua makada ambao majina yao yalipelekwa TAMISEMI na kupangiwa vituo vya kazi kwenye Kata. Kibaya zaidi watendaji waliopo kwenye Kata walikopelekwa makada hao, wameondolewa na kupangiwa kazi zingine ndani ya halmashauri. Na wengi wa makada hao wana elimu ya cheti kutoka chuo cha CCM cha Kivukoni tofauti na matakwa ya kisheria ambayo yanataka mtendaji wa kata walau awe na digrii. Inasikitisha kuwaondoa watendaji walioenda shule na nafasi zao kuchukuliwa na makada mbumbumbu kwa misingi ya kisiasa.

Aidha, ikumbukwe kwamba kuna wahitimu wasiohesabika huko mitaani wenye elimu na ujuzi stahiki lakini serikali imewatelekeza na badala yake kuajiri makada wa chama. Hii nchi sasa inakoelekea ni Mungu tu ndiye anayejua. Nchi inarudishwa kwenye ukoloni. Wakati wa ukoloni waafrika walikuwa wakibaguliwa na wazungu kwa kupewa kazi za ovyo ovyo huku wazungu wakipewa kazi nzuri. Tangu mkoloni ang’olewe nchini Tanganyika, nchi hii haijawahi kushuhudia ubaguzi ktk ajira kama huu unaofanywa na serikali ya CCM ya awamu ya 5.

Ubaguzi huu unatia hasira sana. Hivi kweli CCM hawa makada mmekosa kuwatafutia kazi huko kwenye chama hadi mkaamua kuja kuwachomeka kwenye ajira pasipo kufanyiwa usairi wala nafasi hizo kutangazwa? Na kama mjuavyo, nafasi za utendaji wa Kata bado hazijatangazwa kwa kuwa bado serikali ipo kwenye zoezi la uhakiki. Iweje mseme mpo kwenye uhakiki na wakati huo huo mnachomeka makada wenu kazini na kuwaagiza wakurugenzi wawaingize kwenye payroll? What a shame!

Ndugu zangu nchi hii imeingiliwa na panya (CCM). Hawa sio wanyama wazuri hata kidogo. Hivi haya mambo ya ajabu mnayofanya katika nchi hii mnadhani wale watanzania wenye sifa ambao sio makada wa CCM watajisikiaje?

Ama kweli CCM ni ukoo wa panya—babu mwizi, baba mwizi, watoto wezi, wajukuu wezi, vitukuu wezi, vilembwe wezi na vining’ina wezi! Ukoo huu wa panya walikuwa wanasafiri katika boti la muhogo, lakini kwa sababu ya uroho wao, walianza kulitafuna boti! Kilichofuata ni ukoo mzima wa kizazi cha panya kuzama na kuangamia.

CCM wameanza kuitafuna nchi tangu mwaka 1961 lakini ukomo wao wa kutafuna rasilimali za nchi ni mwaka 2020 kwani hakuna mtanzania mwenye hamu ya kuongozwa na chama cha kifisadi kama CCM ambacho kimeshindwa kuboresha maisha na ustawi wa watanzania. Wananchi wamechoka kubebeshwa ‘magunia ya misumari’ ya bei ya juu ya chakula, mfumuko wa bei wa kutisha, elimu duni, maisha duni, ufisadi wa kutisha na matatizo lukuki yanayosababishwa na panya (CCM) hawa wasiokuwa na haya! Kizazi kizima cha CCM kinakaribia kuzama na kusahaulika kabisa katika ardhi ya Tanzania.

It’s a matter of time before CCM dynasty comes to an end, and that’s when magambas will apprehend the significance and power of the people. Desolately, CCM have been ignoring and looking down their noses at common Tanzanians for many years. Time has now come when citizens can no longer endure CCM’s tyranny and corrupt rule. Everybody is tired of living like a slave on a land endowed with an assortment of natural wealth which only benefits minority fisadis and a few elites in power while majority Tanzanians lead very miserable lives.

What comes around goes around. Let CCM go to hell for good because they have absolutely failed to uplift the living standards of millions of Tanzanians at the expense of a few fisadis whose gargantuan stomachs never fill up! And no one should be blamed for the hatred and grudge that majority people hold against CCM and their crooked government except fisadis themselves who, horrifically, decided to gnaw the cassava-made boat by which they were sailing!
 
Sijui tufanyeje
Dawa yao ni kuwafutilia mbali hawa kupe kuanzia uchaguzi wa mwaka huu maana inaonekana wanathamini siasa zaidi ya kitu chochote. Tukiendelea kuwachekea hawa panya watatusumbua sana siku zijazo.

CCM ni ukoo wa panya—babu mwizi, baba mwizi, watoto wezi, wajukuu wezi, vitukuu wezi, vilembwe wezi na vining’ina wezi! Ukoo huu wa panya walikuwa wanasafiri katika boti la muhogo, lakini kwa sababu ya uroho wao, walianza kulitafuna boti! Kilichofuata ni ukoo mzima wa kizazi cha panya kuzama na kuangamia.

CCM wameanza kuitafuna nchi tangu mwaka 1961 lakini ukomo wao wa kutafuna rasilimali za nchi ni mwaka 2020 kwani hakuna mtanzania mwenye hamu ya kuongozwa na chama cha kifisadi kama CCM ambacho kimeshindwa kuboresha maisha na ustawi wa watanzania. Wananchi wamechoka kubebeshwa ‘magunia ya misumari’ ya bei ya juu ya chakula, mfumuko wa bei wa kutisha, elimu duni, maisha duni, ufisadi wa kutisha na matatizo lukuki yanayosababishwa na panya (CCM) hawa wasiokuwa na haya! Kizazi kizima cha CCM kinakaribia kuzama na kusahaulika kabisa katika ardhi ya Tanzania.

It’s a matter of time before CCM dynasty comes to an end, and that’s when magambas will apprehend the significance and power of the people. Desolately, CCM have been ignoring and looking down their noses at common Tanzanians for many years. Time has now come when citizens can no longer endure CCM’s tyranny and corrupt rule. Everybody is tired of living like a slave on a land endowed with an assortment of natural wealth which only benefits minority fisadis and a few elites in power while majority Tanzanians lead very miserable lives.

What comes around goes around. Let CCM go to hell for good because they have absolutely failed to uplift the living standards of millions of Tanzanians at the expense of a few fisadis whose gargantuan stomachs never fill up! And no one should be blamed for the hatred and grudge that majority people hold against CCM and their crooked government except fisadis themselves who, horrifically, decided to gnaw the cassava-made boat by which they were sailing!
 
Mzee mwandosya alisema tunamteua mtu ambaye hajawahi kushika nafasi yeyote katika chama, hata balozi wa nyumba kumi kumi wa ccm hivi tunategemea nini, sasa nadhani mnaanza kumuelewa mzee mwandosya, na bado ngoja uchaguzi mkuu ukaribie ndiyo mtaona vituko vikubwa sana ambavyo hamjawahi kuviona tangu nchi hii ipate uhuru, hizo ni mvua za rasharasha tu
 
Ndio, wakati huo huo huyo unaesema hajawahi kuwa hata balozi wa nyumba kumi amekuwa mbunge wa chama hicho hicho na waziri kwa miaka kibwena. Hivi unafikiria kwa kutumia viwiko???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu; hili jambo japo litaleta maumivu kwa muda fulani (mimi sitajihangaisha kupiga kura nikijaaliwa kuwa hai 2020 maana kura halali hazitahesabiwa) lakini at the end of the day litarahisisha ukombozi wa taifa letu.
 
Ni katika zama hizi tu, ambapo watu wamekwisha jifunza na wanaendelea na tabia ya kusema uongo kwa sauti ya juu pasipo na ushahidi kwa lile wanalolisema.

Hata hivyo, ikiwa ni kweli unayo haja ya kuwa kiongozi ndani ya jamhuri, hapana shaka kuwa CCM ndio chuo sahihi kwako. Kwa hiyo, ninaamini kuwa kuisemea vibaya CCM kwa upande wako ni kutokana na faida hiyo hiuo kubwa sana
 
Huu ni mkakati wa kuhakikisha wanashinda uchaguzi wa serikali za mitaa.

Alafu Lissu akiongea haya mambo utawasikia wanasema eti nchi inachafuliwa.

Kwa sasa ni bora kushirikiana hata na ibilisi kupambana na hawa watu.
 
Ni kweli kuna maafisa tarafa pia waliajiriwa hivyo hivyo.
Mfano mafisa tarafa wa tarafa ya nyamagana na tarafa ya ilemela mkoani mwanza.
Hawa ni makada na waliajiriwa bila kufanyiwa usaili wowote na sekretariet ya ajira
 
Hii kitu kuna sehemu nilikuta wanaiongelea hapa Iringa, sikuielewa vizuri, ila moja ya mambo yaliyoongelewa ni hilo la watu wanakuja wamepewa ajira toka tamisemi wanapewa kata ambazo zina watendaji halafu wale watendaji hawajapewa barua ya uhamisho wala kupangiwa kata nyingine matokeo yake wameibua migogoro, kata nyingi tu watu wameletwa kwa mtindo huo huku wale wa zamani wakiwa hawajapewa maagizo yoyote
 
Back
Top Bottom