Serikali imeiagiza Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) kuzifanyia uchunguzi wa kina asasi zisizo za kiserikali (NGO`s) zinazosamehewa kodi kwa kuwa baadhi yao zinafanya biashara.
Aidha, imeiagiza Mamlaka hiyo kulegeza masharti ya kutoa vibali kwa wawekezaji wapya ili kuwavutia kuwekeza ikiwa ni njia ya kuongeza walipa kodi.
Maagizo hayo yalitolewa na Rais Jakaya Kikwete jana jijini Dar es Salaam wakati akifunga maadhimisho ya pili ya Siku ya Walipa Kodi nchini iliyoandaliwa na TRA.
Akizungumzia misamaha ya kodi inayotolewa kwa baadhi ya asasi hapa nchini kama vile vituo vya kulelea watoto yatima, Rais alisema kuna haja ya kuzichunguza kwa kina na zile zinazofikiriwa kupewa.
Alisema nyingi ya asasi hizo zinafanya biashara kwa kuwatumia watoto yatima badala ya kutoa huduma.
Alitoa mfano wa asasi moja ya kulelea watoto yatima ya Manyoni mkoani Singida kwamba ilipata msamaha lakini iliagiza tani nyingi za sukari kutoka nje na badala ya kuwahudumia watoto hao, ilikutwa Makambako ikitafutiwa wateja.
Kuhusu wawekezaji, Rais Kikwete lisema kumekuwa na urasimu wa kuwasajili wawekezaji, hali inayowakatisha tamaa na kusababisha kuwepo kwa upungufu wa idadi ya walipa kodi wakubwa.
Mamlaka hiyo imetakiwa kupanua wigo wa kuwavutia wawekezaji na kupunguza vikwazo vya kuanzisha biashara nchini.
Rais Kikwete alisema pamoja na Mamlaka hiyo kuongeza idadi ya mapato inayokusanya, lakini isibweteke kwani bado mapato hayo hayatoshi kwa serikali kufikisha huduma za kijamii kwa Watanzania.
`Pesa ya serikali sitaki ichezewe kabisa, fedha hiyo ni kwa ajili ya kupeleka maendeleo kwa wananchi, lazima mhakikishe kila senti ya mlipa kodi inafanya kazi iliyokusudiwa.
Kwa hili sina mchezo,` alisema na kuongeza
Aidha, ameiagiza pia mamlaka hiyo kuharakisha kurasimisha mali za wanyonge ili ziweze kutambulika kisheria na kumfanya aweze kutumia rasilimali yake kukopa kwenye benki na taasisi nyingine za kifedha.
Awali mwakilishi wa walipa kodi nchini Bw. Elisante Muro, alisema TRA imeboresha huduma zake kiasi kwamba hata walipa kodi hawaoni kufanya hivyo kama kero.
Aliipongeza kwa kufanya kazi kwa haraka hasa ya kuondoa mizigo bandarini, lakini akaishauri TRA kushirikiana na asasi nyingine ili kuharakisha zaidi utoaji wa mizigo ya wateja.
Aliiomba serikali kuongeza muda wa kodi inayolipwa hadi miaka mitano, badala ya kila mara kupandisha kodi, hali aliyosema inawadhoofisha wafanyabiashara na biashara zao.
Mwakilishi huyo pia aliomba Kodi ya ongezeko la Thamani (VAT) ipunguzwe kutoka asilimia 20 hadi 15.5 ili viwango hivyo vilingane na vya nchi jirani.
Naye Kamishna Mkuu wa TRA, Bw. Harry Kitilya, alisema mfumo wa ukusanyaji kodi umeboreshwa kiasi kwamba walipa kodi wamekuwa rafiki wa TRA tofauti na zamani inafikia hata wafanyabiashara kufungiwa biashara zao.
Waziri wa Fedha Bi. Meghji alisema, TRA imetia fora kwa ukusanyaji wa mapato yaliyofikia Sh. bilioni 320 kwa mwezi Septemba mwaka huu.
Hata hivyo, alisema kwamba wanatarajia kuvunja rekodi ya ukusanyaji katika miezi ya Desemba mwaka huu, Machi na Juni mwakani.
Aidha Rais pia alitoa tuzo kwa kampuni zilizoshinda kwa kulipa kodi.
Vigezo vilivyoshindaniwa ni kwa mfanyabiashara anayetunza kumbukumbu vizuri, kiwango cha kodi, ulipaji mzuri usio na usumbufu, uaminifu wa kulipa kwa wakati na uwasilishaji kodi muda muafaka.
Aidha mfanyabiashara mwenye kesi na TRA mahakamani au anafanyiwa uchunguzi wa masuala ya kodi, hakuwa na sifa ya kuingia katika ushindani huo.
Washindi kumi wa kitaifa walitajwa kuwa ni Benki ya CRDB, kiwanda cha sukari cha Kilombero, Benki ya NBC, Benki ya NMB, Songas, benki ya Standard Charter, kampuni ya Sigara (TCC), TANESCO, Mamlaka ya Bandari Tanzania, na Kiwanda cha Saruji cha Wazo.
SOURCE: Nipashe
Tuma Maoni Yako
Aidha, imeiagiza Mamlaka hiyo kulegeza masharti ya kutoa vibali kwa wawekezaji wapya ili kuwavutia kuwekeza ikiwa ni njia ya kuongeza walipa kodi.
Maagizo hayo yalitolewa na Rais Jakaya Kikwete jana jijini Dar es Salaam wakati akifunga maadhimisho ya pili ya Siku ya Walipa Kodi nchini iliyoandaliwa na TRA.
Akizungumzia misamaha ya kodi inayotolewa kwa baadhi ya asasi hapa nchini kama vile vituo vya kulelea watoto yatima, Rais alisema kuna haja ya kuzichunguza kwa kina na zile zinazofikiriwa kupewa.
Alisema nyingi ya asasi hizo zinafanya biashara kwa kuwatumia watoto yatima badala ya kutoa huduma.
Alitoa mfano wa asasi moja ya kulelea watoto yatima ya Manyoni mkoani Singida kwamba ilipata msamaha lakini iliagiza tani nyingi za sukari kutoka nje na badala ya kuwahudumia watoto hao, ilikutwa Makambako ikitafutiwa wateja.
Kuhusu wawekezaji, Rais Kikwete lisema kumekuwa na urasimu wa kuwasajili wawekezaji, hali inayowakatisha tamaa na kusababisha kuwepo kwa upungufu wa idadi ya walipa kodi wakubwa.
Mamlaka hiyo imetakiwa kupanua wigo wa kuwavutia wawekezaji na kupunguza vikwazo vya kuanzisha biashara nchini.
Rais Kikwete alisema pamoja na Mamlaka hiyo kuongeza idadi ya mapato inayokusanya, lakini isibweteke kwani bado mapato hayo hayatoshi kwa serikali kufikisha huduma za kijamii kwa Watanzania.
`Pesa ya serikali sitaki ichezewe kabisa, fedha hiyo ni kwa ajili ya kupeleka maendeleo kwa wananchi, lazima mhakikishe kila senti ya mlipa kodi inafanya kazi iliyokusudiwa.
Kwa hili sina mchezo,` alisema na kuongeza
Mheshimiwa Waziri (Waziri wa Fedha, Bi. Zakia Meghji) usichelee kuniambia mahala penye tatizo, kama mtu anakuzidi kimo, mimi hakuna anayenizidi,
Rais alisisitiza.�Aidha, ameiagiza pia mamlaka hiyo kuharakisha kurasimisha mali za wanyonge ili ziweze kutambulika kisheria na kumfanya aweze kutumia rasilimali yake kukopa kwenye benki na taasisi nyingine za kifedha.